Tarime wamkataa DC

Pinokyo Jujuman

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
552
104
Madiwani wa Tarime wamemkataa DC, Mh. Henjele; wakiwa kwenye mkutano wao Madiwani wote 49 wamepinga kuendelea kufanya kazi na DC huyo kulingana na mapungufu makubwa aliyo yaonyesha wakati wa utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kushindwa kutatua migogoro iliyopo wilayani hapo.
Kulingana na mkanganyiko huo Madiwani hao wamemtaka mkuu wa Mkoa wa Mara Mh. Tupa akutane nao ili waweze kumkabidhi DC wake na kwamba wao hawawezi kufanya naye kazi.

My: Muda wa propaganda umepita; Viongozi someni alama za nyakati
 
jamani hii nimeipenda wilaya zingine ziige mfano huu si kuletewa tu mtu ambaye ameshaharibu sehemu fulani kilombero na nyinyi muige wanatarime kumkataa huyo fisadi mkuu wa wilaya jamani tubadilike M4C
 
Kaaaaaazi kweli kweli.
Huyu DC ni mtata sana, aliripotiwa kuzua vurugu na kumpiga dada yake mangumi baada ya huyo dada na wanafamilia wengine kumkatalia DC huyo kuuza nyumba ya urithi. Nadhani kesi yake ilikuwa mahakamani sina taarifa kama ilishakwisha ama vp. Labda wajuzi wa maswala ya kimahakama watujuze.
 
Nimeipenda sana hii,huu uwe mfano kwa madiwani wengine na hata zaidi sisi wananchi kutoa mashinikizo kwa hawa madiwani wetu kuwakataa hawa maDC,kwanza muda wa kufanya
starehe umebaki kidogo sana wa kupeana hvyo vyeo
 
Watu kama hao ni hiyo ndo dawa yao BUT......MAOVU YAO YAWEKWE HADHARANI NA SIO KUMPELEKEA MKUU WA MKOA
 
hahahaha.... hivi hii serikali haioni kuwa wamefikia ukingoni
"maumivu ya kichwa huanza polepole....."
 
Madiwani wa Tarime wamemkataa DC, Mh. Henjele; wakiwa kwenye mkutano wao Madiwani wote 49 wamepinga kuendelea kufanya kazi na DC huyo kulingana na mapungufu makubwa aliyo yaonyesha wakati wa utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kushindwa kutatua migogoro iliyopo wilayani hapo.
Kulingana na mkanganyiko huo Madiwani hao wamemtaka mkuu wa Mkoa wa Mara Mh. Tupa akutane nao ili waweze kumkabidhi DC wake na kwamba wao hawawezi kufanya naye kazi.

My: Muda wa propaganda umepita; Viongozi someni alama za nyakati

Huyu DC HENJWELE ndiye alimpiga mdogo wake kwa kutaka kutapeli nyumba maeneo ya TEGETAA ANA KESI YA KUJIBU anapewaje ukuu wa wilaya wakati ni MDHALILISHAJI MKUBWA? Mkuu wa Kaya huenda hakujua skendo hii, naomba kupitia hapa aelewe.
 
Nyie mnakuwa kama vile hamumjui Mkulu alivyo na kiburi inapofikia kuondoa watendaji wake aliowachagua?...Mmesahau ya Jairo na Waziri wa Afya? JK hatobatilisha uamuzi wake huo, na atamwambia huyo jamaa kuwa ni UPEPO TU, UTAPITA!. na huyo jamaa kwa kiburi atawajibu kuwa sihamishwi Ng'ooo!
 
viva Tarime, chezeya mkurya wewe. hongera wanatarime mna msimamo sana na hamtaki kupelekesha.
 
Madiwani wa Tarime wamemkataa DC, Mh. Henjele; wakiwa kwenye mkutano wao Madiwani wote 49 wamepinga kuendelea kufanya kazi na DC huyo kulingana na mapungufu makubwa aliyo yaonyesha wakati wa utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kushindwa kutatua migogoro iliyopo wilayani hapo.
Kulingana na mkanganyiko huo Madiwani hao wamemtaka mkuu wa Mkoa wa Mara Mh. Tupa akutane nao ili waweze kumkabidhi DC wake na kwamba wao hawawezi kufanya naye kazi.

My: Muda wa propaganda umepita; Viongozi someni alama za nyakati

Usilolijua ni kama usiku wa kiza.

Hata siku moja DC hawezi kufanya kazi na Madiwani kwa mujibu wa taratibu na kaanua kza Tamisemi huko Tanzania.

Madiwani wanafanya kazi na Mkurugenzi mtendaji wa wilaya (DED) na hata katika baraza la madiwani , DED ndio anakuwa katibu wao. Kwani DED ndio anayetekeleza yale yanayokubaliwa na baraza hilo na kutolea taarifa mambo mbalimbali yanayohusu wilaya ile kupitia kwa wataalamu wake.

Mkuu wa wilaya yupo katika category nyingine kabisa.

Nitakusaidia kidog kujua anaofanya nao kazi DC ni DAS, DIO/DSO, Mshauri wa mgambo wa wilaya, OCD, Mkuu wa gereza wa wilaya, Mkuu wa kikosi chochote cha Jeshi (CO) katika wilaya hiyo. Au kwa kifupi wale wote wanaingia katika kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya husika.

DED na wataalamu wake ambao ni wakuu wa idara mbalimbali katika halmashauri kama ujenzi, elimu, afya, kilimo n.k hawa ndio wanafanya kazi na madiwani.

Nilifanya kazi siku nyingi sana TZ lakin naona kabisa hizo za madiwani na DC ni sawa na mbingu na ardhi.

Nafikiri habari hii haina usahihi kabisa. Mwandishi hajui alinenalo.

Nimeipenda sana hii, kila wilaya wakiwa wakali kama madiwani wa Tarime, hii nchi inaweza kuanza kurudi kwenye mstari unaotakiwa, vile vile itaondoa makunyanzi ya Rais kuteuo hovyo hovyo, ili mladi DC ni mwana ccm... Hongereni madiwani...
 
kweli nchi yetu naona ukombozi uko karibu sana .Tarime oyeeeeeeeeee! huku ndiko kukomaa nakuona nini tufanye sio kuchanguliwa bongo lala na sisi tunakubaliana naomba na wilaya zingine ziinge fukuza hao vichwa maji. maendeleeo mbeleee!
 
Back
Top Bottom