Aisee kumbe sasa najua kuwa Jambo Forum inatumika vibaya kuwachafua watu ambao kwa hakika wanajitoa kuitumikia nchi kwa uaminifu. Na pengine THE BOSS analake jambo.
Tarimba alianza kufanya kazi Bahati Nasibu, na shirika hilo lilivunjwa rasmi tarehe 30 Juni, 2003. Yeye na wenzake wote wakawa wameachishwa kazi.
Wakati huo ikaanzishwa Gaming Board of Tanzania, 1, Julai, 2003. Akapata ajira ya muda pale hadi March 2004 alipoteuliwa na Rais Mkapa. Ajira yake kwa mujibu wa sheria ni ya mkataba wa miaka mitano. Ilipomalizika na kutathminiwa na kuonekana kufaa, akapewa ajira nyingine. Kwa ushahidi huu, jamaa na perform na ndiyo maana yupo.
Yeye si Mwenyekiti, ni Mkurugenzi Mkuu, he is good in gaming matters.
Gaming Board imepata mafanikio makubwa chini yake. Ni taasisi ya kwanza kulipa serikalini mgao wa Serikali kabla hata ya sheria ya kuchangia Bajeti ya Serikali kupitishwa.
Gaming Board inakaguliwa na CAG na kwa miaka 10 tangu ianzishwe imekuwa ikipata hati safi. Tarimba amekuwa Gaming Board kwa miaka 10 na si miaka 20.
Katika Bunge na Bajeti, Taasisi hii ilisifiwa Bungeni na Kamati ya Bunge ya Uchumi na Biashara kwa utendaji wake.
Kama tunaweza kupata watu waaminifu namna hii shida yetu ipo wapi? The Boss lazima utakuwa na shida binafsi na huyu Bwana.
We need more Tarimbas like him!! Keep it up