Tarehe alizoteswa Ulimboka, Mambo ya Kova na Mistari ya Biblia inavyosema (26:6:12) (27/6/'12)

Mtumishi Ta Muganyizi, Mungu aikuze na kuiongeza hekima yako. Akupe kibali machoni pake na wanadam. Amen
 
Asante mkuu kwa kufunuliwa na kutuletea ukweli mtu , na mara nyingi mtenda haki mbele za mungu na wanadamu , huishi kwenye mateso makubwa ya jeshi la shetani (serikari na jeshi la kova) lakini siku zao si nyingi watalia na kusaga meno
 
Wakristo Tanzania tumieni biblia vema, mnaongoza kwa ujinga wa kutojua maandiko..
 
Asante ndugu, nimekupata ingawa sipo upande huo kiimani ila andiko ni letu sote hata waliomfanyia unyama ule Dr. Uli wamelisoma.

Kiongozi kibogo, unaweza kutusadia kwa upande wako, maneno ya siku hiyo yanasemaje? Inawezekana (kwa wale wanaomini mungu) kukawa na message kubwa sana toka kwenye vitabu vya dini mbalimbali.

Ta Muganyizi, Nimesoma zaburi 27:12 kwa kiingereza unapata maana vizuri sana nadhani kuliko hata kwenye kiswahili. Inasema hivi: "Don't abondon me to my enemies, who attack me with lies and threats".
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ta Muganyizi, kama ingewezekana huu ujumbe ungemfikia mpa ACp Msangi na Usalama wa taifa wote ili watafakari huu ujumbe wa neno la Mungu
 
Last edited by a moderator:
Ndio mkuu kwasababu Tanzania inaongoza kwakuwa na "bad christians"

Wanatumia biblia vibaya, hawaisomi, mfano ni hii thread

acha kuropoka wewe, huo ujumbe umekwenda shule wale Pro CCM na wapambe wa Kikwete roho zinawauma kwa husuda na wivu mbona kule Zanzibar wale magaidi wa uamsho wanavyoitumia Quaran wanatumia vizuri? nyinyi na dini lenu ni watu wa kuzimu tu maana mnapenda shari na ugomvi usio kua na maana
 
Ndio mkuu kwasababu Tanzania inaongoza kwakuwa na "bad christians"

Wanatumia biblia vibaya, hawaisomi, mfano ni hii thread

1. What's bad christian?

2. Inaongoza kwa vigezo gani? How do you measure?

3. Wanatumia biblia vibaya, kumbe vizuri ingetakiwaje?
 
Ukisoma Kitabu cha Ayubu sura 26 : 6 mstari huu unasema hivi......



"Mauti iko wazi mbele za Mungu,
uharibifu haukufunikwa"

Then ukisoma Kitabu hichohicho cha Ayubu 27 : 12 mstari unasema hivi....

"Ninyi nyote mmeona hili wenyewe.
Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana?"

Mstari wa 26 :6 ulitumiwa na mtesaji wa Dr. Ulimboka kwa kuhalalisha kitendo chake cha kuumiza wengine kwa kuwa mauti iko wazi mbele za Mungu.

Mstari wa 27 : 12 ndo kelele tunazopigiana ya kumtafuta muuaji au mtesaji wakati Mungu ameshatuwekea wazi.....serikali inaona utata.


Tukiingia Zaburi 26 : 6 inasema " Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia, na kuizunguka madhabahu yako, Ee BWANA"

Mstari hapo juu umetumiwa leo na Gwajima kuuthibitishia umma kuwa serikali wazushi wasilitumie kanisa lake kuhalalisha au kukwepesha maovu yake.

Ukisoma zaburi 27 : 6 inasema " Na sasa kichwa changu kitainuka juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake;Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA"

Maneno haya kwa sasa anayataumia Dr Ulimboka maana adui zake wote wako wanaparanganyika kwa kujichanganya na anamalizia kwa mstari wa 12 zaburi ya 27 inasema " Usinitie katika nia ya watesi wangu; maana mashahidi wa uongo wameniondokea, Nao watoao jeuri kama pumzi"

Maneno haya bado yanasemwa na Ulimboka na wahanga wengine waliopona katika udhalimu wa serikali ya Jakaya Kikwete. Hakika baba rizone wa maajabu yeye yuko nje ya nchi anakula baga na kubembea wasaidizi wake hapa wanaharibu na kuiaibisha nchi.

Mungu alivyokuwa mkuu serikali ya Kenya imesema haiwezi kukubali udhalilishwaji katika mataifa mengine kwa wananchi wake kuja kufanya uhalifu nchi jirani wako wanafuatilia na watatoa tamko muda si mrefu.

Ukisoma mithali 26 : 6 inasema " Apelekaye ujumbe kwa mkono wa upumbavu, hujikata miguu na kunywa hasara" hii ni ile ya bwana yule aliyempigia simu Ulimboka na kuwaita wale wauaji akidhani kuwa hawataonana tena kumbe mtu hajafa.

Mithali hiyohiyo ya 26 : 12 inasuliza hivi " Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadahli kumtumaini mpumbavu kuliko yeye"

Yaani kwa watu wenye kufuatilia ukifuatilia mistari hiyo ya 26 na 27 ambazo ni tarehe za mateso ya Ulimboka na Mistari na mistari ya 6 na 12 ambayo ni mwezi na mwaka utaona maajabu ya kinachoendelea. Mfano tukiangalia mithali 27 : 6 unasema " Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; bali kubusu kwa adui ni kwingi sana" pia mstari wa 12 unasema " Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha bali wajinga huendelea mbele wakaumia"

Yaani maneno yote yanaonesha nani mjinga na ni kwanini wasinyamaze. Kubusu kwingi kwa adui ni hizo jitihada za akina Kova kujifanya wanafuatilia suala la Ulimboka wakati wahusika ni wao wenyewe. Serikali wajinga wanasonga mbele na wataumia.

Huu ndio mtazamo wangu wa tarehe husika na matukio yaliyotokea.

Nimependa ubunifu wako kaka,nimevua kofia kwako.Nilikuwa kwenye ibada ya leo lakini hakika nisingeweza kutoa tafsiri bunifu namna hii

You have blessed my day with joy
 
Ustaadhi, asalam aleykum, sijakusoma kitambo sasa, au ulikuwa kwenye ile kamati yetu ya kufuatilia mabwepande?
Sheikh wangu humu ndani huwa wanapenda sana kudhalilisha Uislaam, sasa 'monitor' wamenifungia 'surveillance' hawachezi mbali na mimi, ingawa mada wanaziona jinsi zinavyoletwa ! Hawezi kuizimz nuru ya SWT !
 
Back
Top Bottom