Tarehe alizoteswa Ulimboka, Mambo ya Kova na Mistari ya Biblia inavyosema (26:6:12) (27/6/'12)

Hoja ni subjective..did you knew?

Duh hii grammar "did you knew?", nilidhani ingekuwa "did you know?" Ingependeza.
Usikasirike JF ni zaidi ya shule. Nimejifunza mengi.


Ta Muganyizi. Hii talanta ulopewa uitumie kutufungua sisi tulozingiriwa na maovu ya dunia hii.
Asante kwa neno zuri
 
Last edited by a moderator:
Hoja ni subjective..did you knew?

Duh hii grammar "did you knew?", nilidhani ingekuwa "did you know?" Ingependeza.
Usikasirike JF ni zaidi ya shule. Nimejifunza mengi.


Ta Muganyizi. Hii talanta ulopewa uitumie kutufungua sisi tulozingiriwa na maovu ya dunia hii.
Asante kwa neno zuri
 
Last edited by a moderator:
TA MUGANYIZI!
Naona unaanza mazoezi ya kufungua kanisa la UKWELI NA UHAKIKA KWA NYAKATI HIZI ZA MAHANGAMIZI YA CCM KWA WANANCHI WASIO NA HATIA....

Ukisoma Kitabu cha Ayubu sura 26 : 6 mstari huu unasema hivi......



"Mauti iko wazi mbele za Mungu,
uharibifu haukufunikwa"

Then ukisoma Kitabu hichohicho cha Ayubu 27 : 12 mstari unasema hivi....

"Ninyi nyote mmeona hili wenyewe.
Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana?"

Mstari wa 26 :6 ulitumiwa na mtesaji wa Dr. Ulimboka kwa kuhalalisha kitendo chake cha kuumiza wengine kwa kuwa mauti iko wazi mbele za Mungu.

Mstari wa 27 : 12 ndo kelele tunazopigiana ya kumtafuta muuaji au mtesaji wakati Mungu ameshatuwekea wazi.....serikali inaona utata.


Tukiingia Zaburi 26 : 6 inasema " Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia, na kuizunguka madhabahu yako, Ee BWANA"

Mstari hapo juu umetumiwa leo na Gwajima kuuthibitishia umma kuwa serikali wazushi wasilitumie kanisa lake kuhalalisha au kukwepesha maovu yake.

Ukisoma zaburi 27 : 6 inasema " Na sasa kichwa changu kitainuka juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake;Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA"

Maneno haya kwa sasa anayataumia Dr Ulimboka maana adui zake wote wako wanaparanganyika kwa kujichanganya na anamalizia kwa mstari wa 12 zaburi ya 27 inasema " Usinitie katika nia ya watesi wangu; maana mashahidi wa uongo wameniondokea, Nao watoao jeuri kama pumzi"

Maneno haya bado yanasemwa na Ulimboka na wahanga wengine waliopona katika udhalimu wa serikali ya Jakaya Kikwete. Hakika baba rizone wa maajabu yeye yuko nje ya nchi anakula baga na kubembea wasaidizi wake hapa wanaharibu na kuiaibisha nchi.

Mungu alivyokuwa mkuu serikali ya Kenya imesema haiwezi kukubali udhalilishwaji katika mataifa mengine kwa wananchi wake kuja kufanya uhalifu nchi jirani wako wanafuatilia na watatoa tamko muda si mrefu.

Ukisoma mithali 26 : 6 inasema " Apelekaye ujumbe kwa mkono wa upumbavu, hujikata miguu na kunywa hasara" hii ni ile ya bwana yule aliyempigia simu Ulimboka na kuwaita wale wauaji akidhani kuwa hawataonana tena kumbe mtu hajafa.

Mithali hiyohiyo ya 26 : 12 inasuliza hivi " Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadahli kumtumaini mpumbavu kuliko yeye"

Yaani kwa watu wenye kufuatilia ukifuatilia mistari hiyo ya 26 na 27 ambazo ni tarehe za mateso ya Ulimboka na Mistari na mistari ya 6 na 12 ambayo ni mwezi na mwaka utaona maajabu ya kinachoendelea. Mfano tukiangalia mithali 27 : 6 unasema " Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; bali kubusu kwa adui ni kwingi sana" pia mstari wa 12 unasema " Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha bali wajinga huendelea mbele wakaumia"

Yaani maneno yote yanaonesha nani mjinga na ni kwanini wasinyamaze. Kubusu kwingi kwa adui ni hizo jitihada za akina Kova kujifanya wanafuatilia suala la Ulimboka wakati wahusika ni wao wenyewe. Serikali wajinga wanasonga mbele na wataumia.

Huu ndio mtazamo wangu wa tarehe husika na matukio yaliyotokea.
 
Kitendo cha Dr. Ulimboka kutoka msituni na kujisogeza mpaka barabrani akaonekana kwa mpita njia na kupewa msaada na mpaka sasa yupo hai nakubaliana kabisa na haya uliyoaandika kwamba Mungu yupo kazini na anafanya kazi yake barabara, kwa kweli serikali ijiandae kwani hawawezi kukwepa hili.
 
Kama kuna jambo nimesoma likaniingia kwa hisia kali sana ni huu ujumbe wako. Asante sana na nilivyounganisha matukio juu ya hili jambo imani yangu imezidi kuwa imara sana juu ya jambo hili. Kuna jambo zuri huko mbele tulitegemee na hii yote ni kwa nguvu za Mungu wetu aliye hai na mwenye uweza wa ajabu.
 
Kama kuna jambo nimesoma likaniingia kwa hisia kali sana ni huu ujumbe wako. Asante sana na nilivyounganisha matukio juu ya hili jambo imani yangu imezidi kuwa imara sana juu ya jambo hili. Kuna jambo zuri huko mbele tulitegemee na hii yote ni kwa nguvu za Mungu wetu aliye hai na mwenye uweza wa ajabu.

Usife moyo endelea kuamini na tutashinda
 
Back
Top Bottom