Tarehe alizoteswa Ulimboka, Mambo ya Kova na Mistari ya Biblia inavyosema (26:6:12) (27/6/'12) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tarehe alizoteswa Ulimboka, Mambo ya Kova na Mistari ya Biblia inavyosema (26:6:12) (27/6/'12)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Jul 15, 2012.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Ukisoma Kitabu cha Ayubu sura 26 : 6 mstari huu unasema hivi......  "Mauti iko wazi mbele za Mungu,
  uharibifu haukufunikwa"

  Then ukisoma Kitabu hichohicho cha Ayubu 27 : 12 mstari unasema hivi....

  "Ninyi nyote mmeona hili wenyewe.
  Ni ya nini basi mazungumzo haya yasiyo na maana?"

  Mstari wa 26 :6 ulitumiwa na mtesaji wa Dr. Ulimboka kwa kuhalalisha kitendo chake cha kuumiza wengine kwa kuwa mauti iko wazi mbele za Mungu.

  Mstari wa 27 : 12 ndo kelele tunazopigiana ya kumtafuta muuaji au mtesaji wakati Mungu ameshatuwekea wazi.....serikali inaona utata.


  Tukiingia Zaburi 26 : 6 inasema " Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia, na kuizunguka madhabahu yako, Ee BWANA"

  Mstari hapo juu umetumiwa leo na Gwajima kuuthibitishia umma kuwa serikali wazushi wasilitumie kanisa lake kuhalalisha au kukwepesha maovu yake.

  Ukisoma zaburi 27 : 6 inasema " Na sasa kichwa changu kitainuka juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake;Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA"

  Maneno haya kwa sasa anayataumia Dr Ulimboka maana adui zake wote wako wanaparanganyika kwa kujichanganya na anamalizia kwa mstari wa 12 zaburi ya 27 inasema " Usinitie katika nia ya watesi wangu; maana mashahidi wa uongo wameniondokea, Nao watoao jeuri kama pumzi"

  Maneno haya bado yanasemwa na Ulimboka na wahanga wengine waliopona katika udhalimu wa serikali ya Jakaya Kikwete. Hakika baba rizone wa maajabu yeye yuko nje ya nchi anakula baga na kubembea wasaidizi wake hapa wanaharibu na kuiaibisha nchi.

  Mungu alivyokuwa mkuu serikali ya Kenya imesema haiwezi kukubali udhalilishwaji katika mataifa mengine kwa wananchi wake kuja kufanya uhalifu nchi jirani wako wanafuatilia na watatoa tamko muda si mrefu.

  Ukisoma mithali 26 : 6 inasema " Apelekaye ujumbe kwa mkono wa upumbavu, hujikata miguu na kunywa hasara" hii ni ile ya bwana yule aliyempigia simu Ulimboka na kuwaita wale wauaji akidhani kuwa hawataonana tena kumbe mtu hajafa.

  Mithali hiyohiyo ya 26 : 12 inasuliza hivi " Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadahli kumtumaini mpumbavu kuliko yeye"

  Yaani kwa watu wenye kufuatilia ukifuatilia mistari hiyo ya 26 na 27 ambazo ni tarehe za mateso ya Ulimboka na Mistari na mistari ya 6 na 12 ambayo ni mwezi na mwaka utaona maajabu ya kinachoendelea. Mfano tukiangalia mithali 27 : 6 unasema " Jeraha utiwazo na rafiki ni amini; bali kubusu kwa adui ni kwingi sana" pia mstari wa 12 unasema " Mwenye busara huyaona mabaya na kujificha bali wajinga huendelea mbele wakaumia"

  Yaani maneno yote yanaonesha nani mjinga na ni kwanini wasinyamaze. Kubusu kwingi kwa adui ni hizo jitihada za akina Kova kujifanya wanafuatilia suala la Ulimboka wakati wahusika ni wao wenyewe. Serikali wajinga wanasonga mbele na wataumia.

  Huu ndio mtazamo wangu wa tarehe husika na matukio yaliyotokea.
   
 2. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  U made my day Ta Muganyizi
   
 3. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #3
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  kaka ndo hivo
   
 4. m

  mangifera Member

  #4
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haleluya! Hili neno halijatoka akilini mwako tu, bali ni Roho wa Mungu amekufunulia upate kuwaambia mataifa!
   
 5. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Nimelipokea na kulitafakari neno la bwana. Ubarikiwe. Jumapili njema!
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #7
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  asante mzazi
   
 8. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  mulemule
   
 9. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #9
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  kabisaaaaaaa
   
 10. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  baada ya kumaliza kusoma nimeshusha pumzi ndeeefu sana kuashiria shukrani zangu. Shukrani tena
   
 11. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,481
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Asante ndugu, nimekupata ingawa sipo upande huo kiimani ila andiko ni letu sote hata waliomfanyia unyama ule Dr. Uli wamelisoma.
   
 12. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Nilisikia kwa baadhi ya wanyakyusa kuwa jina ulimboka lina maana ya mtu ambaye hawezi kuachwa na Mungu. Wenye ufahamu zaidi naomba watujuze, hasa wanyakyusa!
   
 13. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Na iwe hivo
   
 14. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Thank you for good analysis, be blessed
   
 15. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  ulimboka=uniokoe/unisaidie (MUNGU) kwa kinyakyusa,uzi umenifumbua macho
   
 16. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  majina ya kinyumbani tunayopewa na wazazi wetu huwa yana maana sana.
   
 17. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #17
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  haponi mtu hapo neno limejidhihirisha...........serikali ijiandae kuumbuka. Kenya itawaita watuhumiwa iongee nao kwa kilugha chao waeleze ukweli woote kisha kenya watoe tamko.....kuwa wahusika wakuu ni serikali ya JK
   
 18. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Duh!! Kweli Roho Mtakatifu kayafunua yote!!!
  Ubarikiwe sana Ta Muganyizi
   
 19. M

  MtotoWaMandela Member

  #19
  Jul 15, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndio maana MUNGU hakumwacha masaa yote alipigwa na wale wauwaji tena sio mkenya ni watanzania wenzake km angekuwa mkenya Dr angejua matamshi yao maana kiswahili chao kinajulikana bana
   
 20. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #20
  Jul 15, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Na wewe pia mzazi
   
Loading...