Tarehe 18 Mei 1985: Shirika la kijasusi la KGB kulikuwa na idara iliyojulikana kama Directorate K

SEHEMU YA 3

Stalin alikufa mwaka 1953.Aliyemfuata baada ya yeye kufariki alikuwa ni Nikita khrushchev. Miaka mitatu tu toka afariki Stalin aliyemfuata alianza kuuponda utawala wake kwa kuwa ulikuwa wa kimabavu akiwa anahutubia mkutano mkuu wa 20 wa chama .Baba yake Oleg alipigwa na butwaa sana na akaamini huenda ndio itikadi za kijamaa zinaenda kufa kutokana na sera za Nikita. Kwani wafungwa wa kisiasa waliachiliwa,masharti ya censorship yakalegezwa n.k. Hiki ni kipindi ambacho mambo ya umagharibi na uhuru ulianza na raia wakaanza kuona hafueni . Kwa upande wa mzee Anton hakufurahishwa( mlinda legacy) lakini kwa mwanaye ilikuwa ni ahueni.
Akiwa na miaka 17 Oleg alijiunga na Moscow state institute of international relations. Huko alivutiwa na maisha ya chuo . Alijihusisha pia na deep discussion kuhusu sera za nchi yake za usosholisti
.kwa kifupi alianza kuamini katika mrengo wa kibepari(hakuonyesha waziwazi).lakini asijue kwamba mle chuoni kulikuwa na spies wa KGB. Akaonywa kiaina na wenzake. Na pia alikuja kugundua mambo hayajabadilika kabisa . Hii ni baada ya urusi kuivamia Czechoslovakia, raia wa huko wakiandamana kupinga kuwepo kwao ndani ya umoja wa Soviet. Lakini maadamano yalizimwa na ikapelekea umwagaji mkubwa wa damu.

Hiki chuo kilikuwa ni chuo Cha hadhi ya juu sana kwa wakati huo kiasi kwamba Henry Kissinger aliwahi kukiri mwenyewe na kusema ni "Russian Harvard". Chuo hiki kilikuwa chini ya wizara ya mambo ya nje ilikuwa ndio tunaweza kusema breeding ground ya wanadiplomasia, wanasayansi,wachumi,wanasiasa na zaidi training center ya majasusi wa KGB.
Akiwa hapo Oleg alijikita kwenye masomo ya historia, geography,uchumi pamoja na mahusiano ya kimataifa,yote ya haya masomo yakiwa yamejikita katika itikadi za kikomunisti. Taasisi hii pia ilikuwa inafundisha lugha 56 zaidi ya chuo chchote duniani kwa wakati huo. Kujifunza lugha chuoni hapo ilikuwa ni njia na sababu ya kupata ajira nje ya nchi kwa mwana KGB. Na pia ni kwa sababu kilikuwa special kwa ajili ya ujasusi.Oleg kwakuwa alijifunza kijerumani tokea akiwa mdogo aliamua kujifunza kingereza,lakini kaka yake akamlazimisha asomee kiswedish ambaye tayari ni mwajiriwa rasmi wa KGB . Kwani alimsisitizia kujifunza lugha hiyo kutampa mwanya wa kufanya kazi nchi za Scandinavia.
Chuoni hapo alikuwa anasoma magazeti ya nje hususan magharibi Japo yalikuwa machache lakini kulimpa mwanga Fulani wa duniani huko.
Akiwa na miaka 19 Oleg na rafiki yake wa chuo kwa wakati huo aliyeitwa stanislav kaplan walianza mazoezi ya kujijenga miili Yao . wakaaanza kufanya cross-country running kama sehemu ya kuweka mwili fiti.hii ilikuwa ni sehemu ya course hapo chuoni. Huyu rafiki yake alikuwa anasoma kozi fupi za kufanya tracking mwenye asili ya Czechoslovakia. Yeye tayari alikuwa na degree yake tayari aliyoipata kwenye chuo Cha Charles mjini Prague. Na kuja kwake hapo chuoni ni kwamba alichaguliwa kama wale the best and gifted students ndani ya muungano wa Soviet.
Kwa kuwa walikuwa ni marafiki walikuwa wanashare baadhi ya mambo na namna gani hawakuwa wanavutiwa na mfumo wa taifa lao kwa maana walihisi kama wamefungwa akili na propaganda za nchi Yao. kwa kuwa walikuwa ni vijana rijali na wenye muonekano wa kuvutia ,walikuwa ni Magnet kwa wanawake wengi hususan walipokuwa wakipata maakuli kwenye mkahawa mmoja kitingoji Cha Gorky park. kwa hiyo kukaa hapo waliweza kujirusha na bebezi.
kaka wa Oleg ,Vasili yeye tayari alikuwa ameajiriwa ndani ya KGB kama illegal ndani ya kundi kubwa la majasusi waliosambazwa duniani.
huyu Vasili alikuwa ni majasusi kwenye kundi la illegal au kwa kirusi ni Nelegal.
Iko hivi wanasema urusi kulikuwa na aina mbili za majasusi .legal na nelegal. Kuna wale wanatumwa kukusanya taarifa za Siri kwenye nchi Fulani wakijifanya wafanya biashara,wafanya kazi kwenye mashirika ya msaada, wahisani,walimu, waandishi wa habari n.k. . Na wanakuwa na majina feki, passport feki na utambulisho batili. Hawa ikitokea wamekamatwa ina kula kwao mazima na nchi inawakana kama raia wao endapo wamekamatwa . Kwa kifupi wanakuwa hawana formal cover na ni sleeper agents. Sasa Kuna wale ambao ni legal , Hawa wanakuwa na diplomatic cover. Hawa ni wale ambao ni wafanyakazi wa ubalozini (consular staff) akiwemo na balozi mwenyewe . Hawa ikitokea wanahusishwa na ujasusi/uhaini kwenye nchi Fulani mara nyingi hawawezi kushtakiwa wanakuwa declared persona non grata na kufukuzwa na nchi hiyo ndani ya masaa 24 au 72. Hawa Sasa wanakuwa na formal/diplomatic cover .
Kwa hiyo bwana Vasili yeye alikuwa ni illegal aliyeajiriwa mwaka 1960 na FCD (First chief directorate). ndio aliyemshauri bwana mdogo asomee lugha ya kiswedi. Na ndie aliemtambulisha mdogo wake kitengoni kwa mabosi wake wa kitengoni FCD. Hichi kitengo ndani ya KGB kilikuwa kinajihusisha na ujasusi wa nje ya urusi.
Mwaka 1961 bwana Oleg Gordievsky alipata mwaliko wa ghafla na akapewa maelekezo aende kwenye jumba Moja karibu na makao makuu ya KGB lililoko mitaa ya Dzerzhinsky.


View attachment 2591897
Bwana Oleg kwenye miaka yake akiwa chuoni.
View attachment 2591901
Oleg akiwa kwenye sare za KGB
Unajua CFR
 
33



Yote hayo yakiwa yanaendelea kwa upande wa Oleg , jijini London, makachero wa M16 bado walikuwa wanafikiria Nini kimemkuta bwana Oleg Kutokana kwamba mpaka muda huo hawakupata signal kutoka kwake. Hivyo plan ya kumtorosha ikawa ipo active Sasa. Ni kwamba makachero wa M16 kwa upande wa Moscow waliopaswa kupokea signal kutoka kwa Oleg walikuwa ni wafanyakazi wa ubalozi wa London hapo Moscow waliokuwa wanakaa kwenye maghorofa yaliopo kitongoji Cha Kutuzovsky prospekt karibu na mto wa Moscow. Upande wa pili kulikuwa na jengo kubwa lililoitwa hotel Ukraine. Hotel Ukraine lilikuwa mkabala na duka la mikate ..
Kwa mujibu wa plan ya kumtorosha Oleg ya PIMLICO, ilipaswa hawa maafisa kwa zamu wanafika kila mara kwenye duka Hilo la mkate kila jumanne majira ya saa Moja jioni Ili kupata signal kutoka kwa mtu aliyevaa suti ya grey na aliyebeba mfuko wa Safeway bag (Oleg) naye akizuga kama mnunuaji mkate,kama ishara ya kumaanisha operation ianze. Hivyo Mmoja wa afisa wa M16 alipaswa kufika duka Hilo akizuga kununua mkate . Hivyo ikiwa amemuona Oleg ,basi afisa huyu alipaswa kupita karibu na Oleg akiwa na mfuko ulioandikwa Harrod bags huku akila kipande Cha chocolate yenye logo ya mars bars au kit-kat. Baada ya hii signal kuwa received ilimaanisha Oleg baada ya siku tatu akate tiketi ya treni ya usiku inayoenda Hadi mji wa Leningrad Jiji la upili kwa ukubwa Russia, lililopo magharibi ya moscow. Akifika Leningrad hapo Oleg alipaswa kuchukua taxi Hadi kwenye kituo Cha treni zinazoenda Finland. Hapo ilimpasa kupanda treni Tena ya kwanza inayoelekea kwenye mji mwingine ulio karibu na bahari ya Baltic wa Zelenogorsk . Kisha akifika Tena hapo Oleg alipaswa kupanda basi linaloenda mpakani na Finland na kabla ya kufika mpakani ashukie njiani umbali kama wa maili 16 kabla ya kufika mji wa mpakani wa Vyborg. Hapo alipopaswa kushuka ndio rendezvous point au sehemu ya kukutana na makachero wa M16.
Kwa upande mwingine maafisa wa M16 wangepaswa kutoka Moscow kwa magari Yao yakiwa na diplomatic number plate ,Kisha walale Leningrad na waendelee na safari kesho yake . Na wangetegemea kufuatiliwa na makachero wa KGB kutokana na kuwa ni maafisa wa ubalozi . Hivyo wangepaswa kuwachanganya maafisa wa KGB wakiwa njiani kuelekea mpakani mwa Finland na wakikaribia rendezvous point wawakwepe maafisa wa KGB wanofanya patrol barabarani na Kisha wamchukue Oleg ambaye atakuwa amejificha kichakani sehemu Fulani hapo rendezvous point. Na hapo wangeanza safari ya kuelekea Finland.......... Hii plan ilipewa jina PIMLICO.


Sasa bwana Oleg akiwa nyumbani akitafakari na kuona sasa kama kifo kikimkaribia ,akaona Sasa afanye kitu aokoe maisha yake . Hii ni kutokana na plan ya kutuma signal kufeli. Hapo akakumbuka kichumba kidogo kama boksi kilichopo kwenye korido Moja ya nyumba yake Hiyo ilikuwa sio rahisi kujua kama kwenye ukuta huo wa korido Kuna kichumba kingine kidogo .. ilikuwa ni sehemu ya Siri sana kiasi kwamba hata kama kulikuwa na kamera zimewekwa ,sio rahisi kuonekana . Hapo alikuwa ameficha kikaratasi mfano wa cellophane chenye maelekezo yote kuhusiana na operation hii ya PIMLICO. Akakichukua hicho kikaratasi na kurudishia chumba hicho kama awali. Na hapo alianza kusoma maelekezo yote step by step. Na Kisha akalala nacho chini ya mto Ili ikitokea ghafla amevamiwa na maafisa wa KGB wanaomfuatilia aweze kukiharibu kwa haraka. Na kesho yake akayasoma maelekezo yote kwa umakini . Siku hii Oleg hakutaka kufanya mistake ,akajiandaa kwa ajili ya safari ya kwenda Hadi kwenye signal site . ambapo kulikuwa na duka la mkate Ili kuweza kutoa signal Tena kwa M16 . Majira ya jioni duka Hilo linakuwa limejaa watu wanofanya manunuzi ,wengine wakisoma magazeti huku wengine wakisoma ratiba za mabasi na treni .. ilikuwa ni sehemu iliyo bize sana . Hivyo akawa amesimama kwenye eneo ambalo angeweza kuona watu wengi kwa wepesi na muda huo yupo na mfuko wake wenye logo ya Safeway bags aliouweka baadhi ya vitu alivyonunua. Akiwa anavuta muda akaamua kuwasha sigara na kuendelea kuivuta Ili aweze kuona signal yoyote kutoka kwa Afisa wa M16 ambaye nae muda huo alipaswa awepo hapo kwa mujibu wa plan.
Kwa upande wa kikosi kazi Cha M16 hapo Moscow. Plan ilikuwa inaenda kama ilivyopangwa . Afisa Arthur gee naye alikuwa anaendesha gari kuelekea lilipo duka la mikate Kutuzovsky kwa ajili ya kununua mikate alipofika eneo Hilo akaangaza macho kutokana na eneo Hilo kuwa na watu wengi Ili aweze kumuona mtu aliyesimama akiwa amevalia suti ya grey na akiwa amebeba mfuko wa Safeway bag. Na kweli akamuona mtu amesimama akiwa na mfuko kwenye pavement za jengo hilo akiwa Hana uhakika kama ni yeye. Haraka akaamua kwenda kupaki gari kwenye maegesho. Kisha akashuka na kuelekea uelekeo alipomwona bwana yule aliyemwona akiwa amebeba mfuko wa ulioandikwa Harrod bags huku akiwa ameshika kipande Cha Chocolate kikiwa kwenye pakiti ya kampuni ya mars bars. Lakini kutokana na mwingiliano wa watu akiwa anaelekea duka la mikate aliendelea kuangaza macho na kweli akamuona jamaa Oleg akivuta sigara. Kutokana na maelezo ya plan hiyo hakuna sehemu ikielezea kama Oleg ni mvutaji sigara lakini kwa kugonganisha macho tu na akilinganisha na picha ya Siri aliyowahi kuiona aka confirm ni yeye. Naye Oleg akiwa Hana hili Wala Lile akamuona bwana gee akiwa anakula chocolate wakaangaliana . Na hapo signal ikawa acknowledged .Ni kwamba operation hii ikawa ipo active Sasa.
Baada ya hapo bwana Arthur gee akatuma ujumbe wa Siri kwa Roy Ascot ambao ni maafisa wenzake kuhusiana na signal iliyokwisha pita kati yake na Oleg Ili wajipange kwa ajili ya operation hii.

Kutokana na harakati hizi.. surveillance team ya KGB walimpoteza Oleg kama mara mbili hivi kwenye radar zao na haikujulikana ni kwanini na Sasa wakaazimia kuwa makini kuanzia Sasa Ili Oleg asiwapotee Tena machoni mwao. Lakini hii timu haikumjua Oleg ni nani vizuri , linapokuja swala la kuwakwepa ........
Hivyo ilipofika tarehe 17 July majira ya asubuhi Oleg alienda Hadi kwenye kituo Cha treni kilichopo maeneo ya komsomolskaya , na hapo akaenda benki iliyokuwa kituoni hapo kutoa kiasi Cha kama rubble 300 keshi. Kwenye kituo Cha treni hapo alikata tiketi kwa majina feki ya daraja la nne inayoanza safari Jioni ya saa 11 . Treni hii ilikuwa inaenda hadi Leningrad tarehe 19 July ijumaa. Kisha akarudi nyumbani.

Na maafisa wa Moscow wa M16 wakatuma ujumbe wa telegram tarehe 17 julai Hadi London kwamba Sasa operation PIMLICO ni active Sasa . Baada ya vikao kadhaa ndani ya M16 kuhusiana na operation hii ,ikaamuliwa kutumwa afisa martin shawford Hadi Copenhagen nchini Denmark kwa ajili ya kupata ushirikiano kutoka kwa shirika la kijasusi la nchi hiyo PET . Na Kisha aende Hadi mji wa Helsinki Finland kuandaa magari na ku survey eneo la rendezvous point karibu na mpaka wa nchi hiyo na Russia kwa ajili ya mtu wao mtarajiwa. Lakini kulikuwa na kipengele kimoja kwenye hii plan
Ni kwamba ikitokea Oleg amefanikiwa kuingia Finland haikumaanisha kwamba ndio atakuwa Salama . Kwa maana Finland ilikuwa na makubaliano ya kubadilishana wafungwa . Hivyo ikitokea Oleg akishtukiwa na mamlaka za Finland na kukamatwa ni dhahiri atarudishwa Tena Russia.
good plan
 
Ngoja tuone, jamaa kama alikuwa anatazamwa 24hrs sasa hiyo plan mbona kama ilikuwa uchi sana.

Maana ukianza kwenda uelekeo ambao haulewiki inakuwa vipi?

Je, hakuwa na katazo la kutembea umbali fulani? Naona kama alikuwa anatembea popote anapojisikia.

Tupia mzee hata episode 3
 
Ngoja tuone, jamaa kama alikuwa anatazamwa 24hrs sasa hiyo plan mbona kama ilikuwa uchi sana.

Maana ukianza kwenda uelekeo ambao haulewiki inakuwa vipi?

Je, hakuwa na katazo la kutembea umbali fulani? Naona kama alikuwa anatembea popote anapojisikia.

Tupia mzee hata episode 3
Ukifatilia ,kunasehemu aliandika kimemo alichotaka kuwapa M16 kama alarm kwamba anafatiliwa na anawaasa wawe makini na ajali na Kuna radioactive dust

Mwamba ,alishagundua kitu lakini KGB hawakujua kashawajua kilakitu...... Hebu tusubirie mbeleni huko ,aliachana na zile nguo na vile viatu kuvaa vilivyokua na vumbi Ili afanikishe kusepa ....... Ngoja tumsubirie

MC M16 tobby
 
Ngoja tuone, jamaa kama alikuwa anatazamwa 24hrs sasa hiyo plan mbona kama ilikuwa uchi sana.

Maana ukianza kwenda uelekeo ambao haulewiki inakuwa vipi?

Je, hakuwa na katazo la kutembea umbali fulani? Naona kama alikuwa anatembea popote anapojisikia.

Tupia mzee hata episode 3
KGB wanafanya mistakes sana kwa Oleg,huyu wangemuhifadhi chimbo
 
KGB wanafanya mistakes sana kwa Oleg,huyu wangemuhifadhi chimbo
Kumuhufadhi ni ngumu kutokana na cheo alichokuwa nacho.. Kwa cheo hicho lazima wawe na ushahidi wakutosha kumdhibiti Kumbuka hadi muda huo walikuwa wanamhisi tu na yeye anajua wanamhisi tu so anajihami sana.
Na inavyoonekana hao wanaomfuatilia hawana uwezo kamshinda yeye, anajua kuwakataa zaidi wajuavyo
 
Yan kile kitendo cha kuisafirisha familia yake tuu ilikua ni kigezo tosha cha kumtilia mashaka zaidi na kum tight nyavuni

Bado haikuwa sababu tosha ya kuizuia familia hasa ukizingatia wanapo kwenda huko ni kwa the former KGB.

Nadhani pia walichodhamiria ni kumfuatilia kupata ushahid zaidi kuliko kumhifadhi pamoja na familia yake.

Mpe uhuru, lkn bakini naye macho. Wakiamini kbs kuna sehemu tu atajaa kama kweli anawasaliti.
 
KGB wanafanya mistakes sana kwa Oleg,huyu wangemuhifadhi chimbo

Kumuhufadhi ni ngumu kutokana na cheo alichokuwa nacho.. Kwa cheo hicho lazima wawe na ushahidi wakutosha kumdhibiti Kumbuka hadi muda huo walikuwa wanamhisi tu na yeye anajua wanamhisi tu so anajihami sana.
Na inavyoonekana hao wanaomfuatilia hawana uwezo kamshinda yeye, anajua kuwakataa zaidi wajuavyo

Yan kile kitendo cha kuisafirisha familia yake tuu ilikua ni kigezo tosha cha kumtilia mashaka zaidi na kum tight nyavuni

Bado haikuwa sababu tosha ya kuizuia familia hasa ukizingatia wanapo kwenda huko ni kwa the former KGB.

Nadhani pia walichodhamiria ni kumfuatilia kupata ushahid zaidi kuliko kumhifadhi pamoja na familia yake.

Mpe uhuru, lkn bakini naye macho. Wakiamini kbs kuna sehemu tu atajaa kama kweli anawasaliti.
Ndugu zangu ni kwamba hapa tunababwaja tu lakini ukweli ni kwamba hawa KGB walionyesha udhaifu uliopindukia mipaka ama kwa lugha nyepesi udhaifu kiwango cha laMi😂😂
 
Ndugu zangu ni kwamba hapa tunababwaja tu lakini ukweli ni kwamba hawa KGB walionyesha udhaifu uliopindukia mipaka ama kwa lugha nyepesi udhaifu kiwango cha laMi
Muda mwingine mkiwa mnasoma taarifa kama hizi muwe na tafakuri. Mmeambiwa kuanzia cheo Cha Kanali kinahitaji ushahidi ndio atuhumiwe, unadhani ukilichukua swala kama hilo kichwa kichwa utaleta picha gani Kwa Waandamizi wengine kama yeye.
 
Nilichogundua nchi za wenzetu zilizo serious kwenye mambo yake huwekeza sana kwenye ujasusi.

Hapa kwetu na Afrika kwa ujumla ujasusi walio nao sirious ni wa siasa tu , tena siasa za ndani ambazo kimsingi ni siasa mbovu na zenye ubinafsi na kujikimbikizia madaraka.

Hatuna ujasusi wa uchumi, ujasusi wa teknolojia, ujasusi wa matibabu madawa , ujasusi wa elimu na mengi yenye muktadha wa namna hiyo.

Hii ni changamoto kubwa sana kwetu na natumaini tutaendelea kuwa kua daraja la chini mpaka tutakapo badili fikra na mitazamo yetu.
Nilishawahi kushauri kuhusu haya mambo. Lakini kwa sababu raia tupo branded kuwa HATUNA AKILI kama za mafisadi wanaowamiliki watu wa vitengo. Tutaendelea kuumia mioyoni huku nchi yetu ikiporomoka

Soma hapa Tanzania inacheza upatu kwenye ujasusi wa kouchumi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom