MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,011
- 16,748
Mara kwa mara Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu John Pombe Magufuli amekuwa akisikika akisema kuwa Tanzania ni nchi Tajiri na itakuja kuwa Tajiri sana. Wakati Mheshimiwa Rais akisema ( akitomboka ) hayo / hivyo leo tena Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Bashiru Ally Kakurwa amesikika nae akisema kuwa Tanzania si nchi Tajiri na pia si nchi ya Matajiri hivyo Mimi kama Mtanzania na Shabiki Mwandamizi wa CCM ( japo bado siyo Mwanachama Kamili ) nashinndwa sasa kujua niamini neno la nani kati ya hawa Waandamizi Wakuu Wawili ndani ya Chama.
Hata hivyo kwa mbali hivi ni kama vile naona Kauli za Siku hizi za Katibu Mkuu wa CCM zinakinzana mno na za Bosi wake Mwenyekiti kiasi kwamba naanza kuhisi kuwa huenda Katibu Mkuu ameanza Kukanyaga Waya hivyo pengine atasababisha aundiwe Zengwe bure na aondolewe hapo kwani ni kama vile anaenda Kinyume na ile Timu ya Kusifu na Kupamba iliyo na Wanafiki wengi ambao baadhi yao hivi punde tu mtaanza Kuwaona wakija Kujibu hapa kwa Jazba na wakimpamba mno Boss Mkuu na Kumdhihaki Naibu Boss Mkuu.
Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa makini sana na ukiweza pia unaweza taratibu ukaanza kujiandaa Kisaikolojia pia. Sishangai sana kwani ndiyo maana hata majuzi tu hapa ulisikika tena ukisema kuwa unatamani mno kurudi tena Kukufunzi Chuo Kikuu ambako ndiko ulikuwa ukihudumu kwa muda mrefu tu kwani huenda nawe pia ukawa tayari umeshaanza kuona dalili kuwa huendani na Boss Mkuu ( hasa Kimitizamo ) hivyo unataka umzingue tu kwa Makusudi ili akutoe na uendelee na Maisha yako mengine. Na kwa jinsi ninavyokujua hasa Kimisimamo na ni Mtu usiyependa Unafiki wala Upuuzi ( ambao wana CCM wengi japo siyo wote wa sasa wanao ) sidhani kama utaendana na Boss Mkuu na huenda akawa ameshakuchoka ila anakuvumilia tu.