Taratibu naanza kuona dalili ya Uhusiano mbaya unakuja kati ya ' Wazito ' hawa Wawili ndani ya Chama cha CCM

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,734
Mara kwa mara Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu John Pombe Magufuli amekuwa akisikika akisema kuwa Tanzania ni nchi Tajiri na itakuja kuwa Tajiri sana. Wakati Mheshimiwa Rais akisema ( akitomboka ) hayo / hivyo leo tena Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Bashiru Ally Kakurwa amesikika nae akisema kuwa Tanzania si nchi Tajiri na pia si nchi ya Matajiri hivyo Mimi kama Mtanzania na Shabiki Mwandamizi wa CCM ( japo bado siyo Mwanachama Kamili ) nashinndwa sasa kujua niamini neno la nani kati ya hawa Waandamizi Wakuu Wawili ndani ya Chama.

Hata hivyo kwa mbali hivi ni kama vile naona Kauli za Siku hizi za Katibu Mkuu wa CCM zinakinzana mno na za Bosi wake Mwenyekiti kiasi kwamba naanza kuhisi kuwa huenda Katibu Mkuu ameanza Kukanyaga Waya hivyo pengine atasababisha aundiwe Zengwe bure na aondolewe hapo kwani ni kama vile anaenda Kinyume na ile Timu ya Kusifu na Kupamba iliyo na Wanafiki wengi ambao baadhi yao hivi punde tu mtaanza Kuwaona wakija Kujibu hapa kwa Jazba na wakimpamba mno Boss Mkuu na Kumdhihaki Naibu Boss Mkuu.

Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuwa makini sana na ukiweza pia unaweza taratibu ukaanza kujiandaa Kisaikolojia pia. Sishangai sana kwani ndiyo maana hata majuzi tu hapa ulisikika tena ukisema kuwa unatamani mno kurudi tena Kukufunzi Chuo Kikuu ambako ndiko ulikuwa ukihudumu kwa muda mrefu tu kwani huenda nawe pia ukawa tayari umeshaanza kuona dalili kuwa huendani na Boss Mkuu ( hasa Kimitizamo ) hivyo unataka umzingue tu kwa Makusudi ili akutoe na uendelee na Maisha yako mengine. Na kwa jinsi ninavyokujua hasa Kimisimamo na ni Mtu usiyependa Unafiki wala Upuuzi ( ambao wana CCM wengi japo siyo wote wa sasa wanao ) sidhani kama utaendana na Boss Mkuu na huenda akawa ameshakuchoka ila anakuvumilia tu.
 
nadhani Dr. aliwekwa pale makusudi kabisa ili ku 'neutralize' mapepo ya mwenyekiti. Mwenyekiti hana chembe ya busara wala hekima, tena hapimi uzito wa kauli zake, lakini Dr. yuko makini na anajaribu kuwakemea madogo wanaopandisha mapepo ili kuendana na mwenyekiti.
angalia jinsi alivyolizima suala la waraka wa wazee, kuna vijana wa 'praise team' walishaanza kupandisha mori.
 
Pia hii kauli ya marufuku kwa mwanaccm u mwanachadema kutoa maelekezo kwa watumishi wa umma ni ya msingi sana, ingawa naona kama inapishana na inaweza kuleta mgogoro, maana watumishi wa umma wanatupiwa kila kitu
 
Ukiwa CCM unatakiwa uwe mnafiki na mwongo.......

Ukiwa wewe ni mtu wa kumwogopa Mungu na msema ukweli na unapenda haki itamalaki bila kujali itikadi zetu za kisiasa, hakika utaitwa majina mabaya kuwa wewe si mzakendo na unatumika na mabeberu.

Ukiwa CCM ni condition mojawapo kuwa ni LAZIMA uambatane na shetani
 
Acha unafiki, wewe sio shabiki wa CCM, ht lugha iliyo ktk maandishi yako yanaonyesha sio shabkli mwandamizi km hnavyojitia, nikija kwenye mada yako ni kwamba siasa zina lugha nyingi, Magu anamaanisha kwa rasilimali zilizopo zikitumika vzr sisi no majiri na kwa Dr Bashiru yuko sahihi kwamba sisi no masikini, sasa wewe kaa ukitafsiri neno kwa neno utaishia hapo hapo
 
Ukiwa CCM unatakiwa uwe mnafiki na mwongo.......

Ukiwa wewe ni mtu wa kumwogopa Mungu na msema ukweli na unapenda haki itamalaki bila kujali itikadi zetu za kisiasa, hakika utaitwa majina mabaya kuwa wewe si mzakendo na unatumika na mabeberu.

Ukiwa CCM ni condition mojawapo kuwa ni LAZIMA uambatane na shetani
Haaa haaa we jamaa umenichekesha, hii condition ya kuambatana na shetani ni noma sn
 
Uchaguzi wa mwaka huu ni tofauti sana na miaka ya nyuma. Mpaka muda huu mitaani kupo kimya utadhani hakuna uchaguzi. Tunaotumia public transpot hatusikii malumbano ya abiria kushabikia wagombea kama 2015. Unasafiri toka Boko mpaka Kariakoo hakuna anayeongea uchaguzi. Baa za wenzetu wa kaskazini ni kimya, hakuna makundi ya uhamasishaji ya kutoa offer za bia na mbuzi. Kweli hii ni DALILI MBAYA kw wenzetu wa Kata ya Hananasifu😂😂
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom