Tapeli awaingiza mjini Chief Mareale na Mrisho Mpoto

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Binti mmoja wa kilokole hapa jijini Arusha amezua heka heka na gumzo baada ya kuwaingiza mjini aka kuwatapeli watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na watu maarufu kama vile Chief Mareale kutoka uchagani na msanii wa kughani ndugu Mrisho Mpoto.

Inasemekana nusura tego hili la kitaplo limkute mheshimiwa rais alipokuwa ziarani jijini Arusha wiki kama moja na ushee iliyopita.

Binti huyu aliyetumia mwamvuli wa 'bwana yesu asifiwe' aliandaa tamasha feki la kutangaza utamaduni ambalo lilitakiwa kuwajumusha machifu,watemi,maleigwanani,mamwinyi na wakuu mbalimbali wa makabila ya Tanzania.Idea ilikuwa superb hata watu wa TANAPA walitaka kuidhamini na hata mheshimiwa rais angeombwa kufungua tamasha hili!

Hatimaye tamasha lilianza kwa maandamano tena yakishirikisha kina chief Mareale akiwa kapanda ngamia kama matajiri ya dubai yanavyobeba falcon!

Tamasha likaendelea na ilipofika siku ya kilele yaani jumamosi ndipo tafrani likaanza.

Binti wa kilokole ambaye ni director wa NGO feki akatokomea kusikofahamika na kuwaacha solemba wateja wa tamasha,waandaaji kwa maana ya wafanyakazi wake na wote waliokodishwa,kina Mrisho Mpoto na Mareale waliolala hoteli bila kulipiwa wala kulipwa.

Hatimaye jamaa zetu wa Fanya Fujo Uone wakavamia tamasha hapo uwanja wa shekh amri abedi ili kuepusha maafa yatokanayo na hasira za wote walioingizwa cha kike!

Kwa sasa binti huyu yuko nje kwa dhamana na inasemekana anadaiwa karibu shilingi milioni 80.

UPDATES
Kuna maswali yanaulizwa hapa mjini,iweje binti huyu aweze kupiga mchongo mkubwa namna hii bila ya kuwa na mtu au mtandao nyuma yake?

Kuna hisia tofauti ya kwamba hata Mangi mareale anaweza kuwa ni sehemu ya mchongo ambao lengo lake ni kuchota mafedha kutoka ughaibuni.







































 
huyu siyo binti mlokole bali ni tapeli lililokubuhu!!
 
huyu siyo binti mlokole bali ni tapeli lililokubuhu!!

Sema hakuamua kifungua kanisa lake....Laiti angeamua kufungua kanisa ungemuita Mtumishi....Yeye kaamua kufanya utapeli kwa stail yake na si utapeli kwa staili ya kanisa
 
Jina kake nani? Ajira kwa vijana wapi? maisha bora kwa kila mtanzania wapi? ahadi hewa kisiasa haya ndiyo matokeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…