Nimepata mtoto wa kiume. Mama na mtoto wanaendelea vizuri
hapa natetemeka kwa furaha, nimeweka muziki wa rose mhando uitwao MUNGU NITAKUSHUKURU. nimejawa na furaha, lakini niko mbali sana nje ya Tanzania, ningependa kuwepo lakini nimesafiri masafa marefu kutafuta maisha lakini mwenzangu kwa ujasiri mwingi kajifungua salama mtoto wa kiume! Glori to God.
nimetafuta kila upande ndugu yangu wa kumshirikisha furaha yangu nimekosa isipokuwa JF members. jamani Mungu ashukuriwe kwa jinsi anavyotujalia waja wake mapaji kwa ukarimu. libarikiwe jina la Bwana wa Mabwana. amen.
nachakarika nirudi mapema nyumbani kumpakata mwanangu... ooo, nimejawa na furaha wapendwa siwezi kusema kwa usahihi
Daaaaaah!!Nimeishiwa maneno ndugu yangu,ninachosema ni pole japokua nahisi kama haitoshi vile!Mungu awe nawe kipindi hiki kigumu!Daaah!
asante sana mpendwa, sisi sote ni wa kwake na hatimaye kwake tutarejeaPole sana kwa kweli
Pole sana Mtu mmoja....Kazi yake Mola haina makosa. Mungu akujaalie wepesi na akujaze imani katika kipindi hiki kugumu.Pole sana.
Pole sana jamani.Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu
Mpendwa! Pole sana tena narudia pole sana! Najua unavyoumia sana kwa namna ujuavyo ila nakuhakikishia ya kwmb MUNGU atakujaza nguvu na utampata mwingine tu,ni vigumu sana kusema niliyonayo lakini kuwa jasiri kwa kipindi hiki chenye majonzi Mpendwa. Pole sana na Mungu amlaze mahala pema peponi! Amen!
Pole sana mpendwa; hakuna maneno nitakuyooandika yatakayoleta faraja, kwani naujua uchungu wa kuondokewa na mpendwa wako. Mungu akupe nguvu ya kuendelea kuishi na kumshukuru kwa kukupa hiyo miezi michache ya uhai wa mwanao mpenzi.
Mungu ailaze roho ya malaika wake mahali pema peponi. Kwa sisi tunasema umepata muombezi huko mbinguni.
pole sana mkuu hii inasikitisha sana umempata mwanzo wa mwaka na umempoteza kwenye mwisho wa mwaka kifo chake kitakuwa na utata, narudia tena pole sana mkuu
Mtu MMoja... pole sana, yani nimesoma hii thread na nimepatwa na depression kabisa, this is tough to take and i pray that you maintain your strength and composure ili umsaidie mama mtoto naye
Kids are little flowers, they always brighten our lives and broaden our smiles... But we always owe it to the higher one
Shukuru Mungu umewahi kumuona mwanao, kuna watu wanakesha kwa waganga, kwenye ibada na mahospitali wakitafula mtoto japo wa kumuona kwa sekunde moja
MSHUKURU MUNGU
RIP Mtu mmoja jr..
asanteni sana wapendwa. yaani nimechimbika moyoni kwa kweli
Duh! Hadi machozi yamenilenga lenga. Pole mkuu, jikaze maana kila jambo linalotokea hutokea kwa sababu.
Pole sana sana mkuu
Mungu akujalie lililo jema katika kipindi hiki kigumu. Pole sana sana mkuu. Inauma sana na ni kipindi kigumu sana ila muombe Mungu sana akupitishe katika kipindi hiki kigumu. Pole sana mkuu.
Pole sana. Mungu akujalie nguvu katika kipindi hiki cha majonzi.
Magumu yatupatayo ni ya kitambo, Mungu yupo na sisi daima! Usibondeke moyo mpendwa, Mungu wetu ajua sababu ya yale yote tuyapitiao na yeye ndie mwenye kutupa faraja na amani!! Pole saaana mpendwa wetu, pole pia kwa mwanamke mwenzangu i.e mama wa mtoto! Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani malaika wake mpendwa......AMEN!!!