Tanzia UDSM rafiki kipenzi ametutoka

Tanzia UDSM rafiki kipenzi ametutoka

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2013
Posts
2,149
Reaction score
1,721
SOTE FAMILIA MOJA
Yakaribia jioni, 'desa' limenitibua
Mbiombio darasani, 'pepa' bandika bandua
Muhula upo mwishoni, mambo nayo yamejaa
Sote familia moja, wewe mbele sisi nyuma

Nakatiza ‘holu-wani’* naona watu kundini
Sura zao za huzuni, hawakuwa furahani
Najisogeza jirani, ndipo napata undani
Sote familia moja, wewe mbele sisi nyuma

Sekibenga metutoka*, ghafula tena meenda
Kabla mauti jafika, darasani ulienda
Mchana ulipofika, ukalalia kitanda
Sote familia moja, wewe mbele sisi nyuma

Safari ulosafiri, sote tutaipitia
Siku yetu ikijiri, kwa Manani tarejea
Masikini matajiri, hii yetu wote njia
Sote familia moja, wewe mbele sisi nyuma

Wamekwenda manabii, wajumbe walotukuka
Wakafwata mawalii, kwa wema walosifika
Kwamba yetu njia hii, ni hakika iso shaka
Sote familia moja, wewe mbele sisi nyuma

Nduguzo wa Mlimani, tumeingiwa fadhaa
Kila mmoja chuoni, jua anakuombea
Aloleta duniani, ndiye YEYE ametwaa
Sote familia moja, wewe mbele sisi nyuma

Ndimi wa Shaibu mwana, la kuongezea sina
Jambo lilo la maana, tumuombe Maulana
Kunako pepo mwanana, akujaalie Bwana
Sote familia moja, wewe mbele sisi nyuma

*Holu-wani=Hall One, Main Campus, UDSM.
*Sekabenga=Sekabenga Mwakimenya, mwanafunzi aliyekutwa amefariki bwenini ( Hall One) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana (30/5/2014). Chanzo cha kifo chake hakijaelezwa bado na wataalam wa Afya. Bwana ametoa, Bwana ametwaa.

10428491_769844323066592_2994590543965687360_n.jpg
 
Dah, kabinti kazuri kweli maskini. Mungu atusaidie.
R.I.P
 
Jamani inasikitisha sana

RIP Marehemu

Poleni familia kwa kumpoteza binti yenu

MUNGU ndie mfariji wenu
 
Rip sekabenga mwakimenya ,tulikupensa ila mungu amekupenda zaidi jina la bwana lihimidiwe,
 
Daaah na imagine wazazi wake wanavyojisikia, ukute hata siku alivyofariki aliongea na wazazi wake na akasema ni mzima kabisa. Baadaye mnapigiwa simu mtoto wenu amefariki daaah Mungu simama na familia hii. Pumzika kwa amani Sakay

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
RIP mwanafunzi,Mungu akulaze mahali pema peponi,amen
 
RIP jaman mdada mzuri mweeeeee ndoto zake zimeishia hewani
 
Rest in peace bi dada....mungu ni mpangaji wa kila kitu.


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
shairi la kuuzunisha sana umenikumbusha enzi ya gazeti la majira na akina andanenga BTW APEPE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom