TANZIA: Timotheo Paul kiongozi wa BAVICHA kata ya Kimwani Muleba, afariki dunia

Nonsense...rest in hell..vifo vyote ni vya kizembe.mtu utajiuaje kisa mpinzani wako kashinda?
Afu thread imekaa kichochezi hii.
 
Tishu paper nyingine zilizotumika kumfanya bwana mkubwa awe msafi hizo zimetupwa kwenye jalala, sehemu ya laana. Aliyejifuta maisha yanaendelea, machoni mwa watu yu msafi, yu mtanashati. Masikini tishu, hakuna anayeziulizia, kuzijali wala kuzithamini. Jalalani ni sehemu wanakoishi wendawazimu, hakuna mwenye akili timamu aendaye huko, labda tu mtumwa mtupa taka. Masikini tishu!
 
Poleni wafiwa,
Huyo alojinyonga kisa mama yake kushangilia ushindi wa ccm nae alikuwa punguani! Siasa za majitaka!
 
Inasikitisha sana Mungu awalaze pema ndugu zetu marehemu,hasa huyo dogo aliyejinyonga anaona maisha yanavyomchapa chini ya serikali kandamizi ajira hakuna,pesa imekuwa ngumu sometimes alitaka kuendelea na masomo ya juu kakosa mkopo halafu bimkubwa anashangilia upumbavu kisa yeye analetewa na baba au ana alternative way ya kupata ridhki..last election nilimsikia bimkubwa ananitambia kwamba vyama vya vijana haviwezi kushindana na baba yao,nilimwangaliaa ni vile tu sina uwezo wa kumwadhibu ila angenikoma.na nilichogundua hawa watu wazima kuna wakati unafika IQ zao zinatetereka maana wakikuomba kitu ukiwaambia kwa sasa huna mambo magumu kazi hazendi pesa imekuwa ngumu wanakulaumu wanasahau kuwa wao ndo walioweka mzimu mbele yako.
 
Makamanda, tunasikitika kuwatangazia chama kimepoteza kamanda mwenzetu Timotheo Paul (28) ambaye alifariki jana hospitalini Bugando kutokana na majeraha aliyopata akiwa kwenye kampeni Kata ya Kimwani, Muleba Kagera.

Alikuwa kiongozi wa Bavicha katika kata hiyo. Kutokana na mazingira ya kifo chake, chama ngazi ya kanda ya ziwa Viktoria kimesafirisha mwili wa marehemu kwa kutumia gari la kanda leo alasiri.

Hivi ninavyoandika, msafara ndio unakaribia Kimwani. Waliosindikiza mwili huo wakiambatana na ndugu wa marehemu, ni Meshack Micus, Katibu wa Kanda, na Khalid Selemani, ofisa katika ofisi ya kanda.

Kamanda Timotheo amefia kazini. Amekufa kwa heshima. Tumwombee huko aendako alikotangulia. Mungu amweke mahali pema!

Taarifa nyingine zitafuata kadiri zitakavyotufikia.

Hapo hapo, huko huko Kimwani, kijana mwingine amezikwa leo. Huyo alifariki kwa ajali siku ya uchaguzi.

Kutoka Nkome, Geita, kuna kijana aliyejiua Jumapili siku ya uchaguzi baada ya matokeo, alipomwona mama yake mzazi anashangilia ushindi wa CCM. Kijana (jina lake halijapatikana bado ). Alijinyonga .

Mungu awape faraja wafiwa!. Na aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. AMEEN

............................................
ANSBERT NGURUMO
Makamu Mwenyekiti CHADEMA

Kanda ya Victoria
Hawa wa ajali kwa kweli ni wapiganaji. Unajinyonga kisa matokeo. Huu ni umbururah!!!
 
Duh Naona mama huyo hiyo incidence haitakaa imtoke.
Hapo ukute jamaa ndio anahangaika kulisha famili na jinsi hali ya uchumi ilivyo MBAYA unakuta mtegemezi wako anashangilia serikali hii. Ndio maana kila siku nasema tuache kutukana tufungwe jela, tujiandikishe na kupiga kura ndio silaha pekee tuliyonayo. Kaondoka Jammeh itakuwa kile chama cha ajabu ajabu.
 
Makamanda, tunasikitika kuwatangazia chama kimepoteza kamanda mwenzetu Timotheo Paul (28) ambaye alifariki jana hospitalini Bugando kutokana na majeraha aliyopata akiwa kwenye kampeni Kata ya Kimwani, Muleba Kagera.

Alikuwa kiongozi wa Bavicha katika kata hiyo. Kutokana na mazingira ya kifo chake, chama ngazi ya kanda ya ziwa Viktoria kimesafirisha mwili wa marehemu kwa kutumia gari la kanda leo alasiri.

Hivi ninavyoandika, msafara ndio unakaribia Kimwani. Waliosindikiza mwili huo wakiambatana na ndugu wa marehemu, ni Meshack Micus, Katibu wa Kanda, na Khalid Selemani, ofisa katika ofisi ya kanda.

Kamanda Timotheo amefia kazini. Amekufa kwa heshima. Tumwombee huko aendako alikotangulia. Mungu amweke mahali pema!

Taarifa nyingine zitafuata kadiri zitakavyotufikia.

Hapo hapo, huko huko Kimwani, kijana mwingine amezikwa leo. Huyo alifariki kwa ajali siku ya uchaguzi.

Kutoka Nkome, Geita, kuna kijana aliyejiua Jumapili siku ya uchaguzi baada ya matokeo, alipomwona mama yake mzazi anashangilia ushindi wa CCM. Kijana (jina lake halijapatikana bado ). Alijinyonga .

Mungu awape faraja wafiwa!. Na aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. AMEEN

............................................
ANSBERT NGURUMO
Makamu Mwenyekiti CHADEMA

Kanda ya Victoria
R.I.P kamanda,nadhani itakuwa alishindwa kukubali kama ccm ilishinda sasa kuna mawili presha au sukari ilishuka ndio sababu.
 
Kifo cha kijinga sana.nife kisa siasa? Yaani unakufa kwa kumtafutia mwenzako ajira?
Mkuu ukiweka ubinafsi mbele hutawahi leta ukombozi au kwenye mageuzi yoyote hapa duniani au kwenye jambo lolote unalojihusisha nalo. Huyo alikuwa anatekeleza wajibu wake na yakamkuta yaliyomkuta sasa unafkiri alitaka kufa tu out of nowhere??? Mkuu jifunze kuwa sacrifice ndio number one priority kwa wanamageuzi kote duniani odinga mpaka walimuhasi hawezi kuzaa, steven biko aliuawa, lumumba aliuawa hawa wote walitoa kafara maisha yao kupigania haki za wanyonge na kutetea walichokiamini. Ila miaka mingi damu za hawa wanaukombozi zilikuja kuleta mabadiliko kwenye maeneo yao na ndio maana ya mageuzi na uanamabadiliko ''NI KUJENGA MTI AMBAO KIVULI CHAKE HUTAWAHI KUKAA'' kwa hyo we should consider ths BAVICHA guy as a hero haina haja ya kumkejeli maana kifo kilimkuta hakukifata....so mind ur words
 
Back
Top Bottom