TANZIA: Timotheo Paul kiongozi wa BAVICHA kata ya Kimwani Muleba, afariki dunia

Mhere Mwita

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
235
1,275
Makamanda, tunasikitika kuwatangazia chama kimepoteza kamanda mwenzetu Timotheo Paul (28) ambaye alifariki jana hospitalini Bugando kutokana na majeraha aliyopata akiwa kwenye kampeni Kata ya Kimwani, Muleba Kagera.

Alikuwa kiongozi wa Bavicha katika kata hiyo. Kutokana na mazingira ya kifo chake, chama ngazi ya kanda ya ziwa Viktoria kimesafirisha mwili wa marehemu kwa kutumia gari la kanda leo alasiri.

Hivi ninavyoandika, msafara ndio unakaribia Kimwani. Waliosindikiza mwili huo wakiambatana na ndugu wa marehemu, ni Meshack Micus, Katibu wa Kanda, na Khalid Selemani, ofisa katika ofisi ya kanda.

Kamanda Timotheo amefia kazini. Amekufa kwa heshima. Tumwombee huko aendako alikotangulia. Mungu amweke mahali pema!

Taarifa nyingine zitafuata kadiri zitakavyotufikia.

Hapo hapo, huko huko Kimwani, kijana mwingine amezikwa leo. Huyo alifariki kwa ajali siku ya uchaguzi.

Kutoka Nkome, Geita, kuna kijana aliyejiua Jumapili siku ya uchaguzi baada ya matokeo, alipomwona mama yake mzazi anashangilia ushindi wa CCM. Kijana (jina lake halijapatikana bado ). Alijinyonga .

Mungu awape faraja wafiwa!. Na aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. AMEEN

............................................
ANSBERT NGURUMO
Makamu Mwenyekiti CHADEMA

Kanda ya Victoria
 
Poleni wafiwa,,

Huyo kamanda aliyejinyonga kwakweli ni fundisho kubwa kwa Chadema,

Ukitaka kujenga anzia nyumbani haiwezekani mpaka ufikie hatua ya kujinyonga kisa mama yako ameshangilia ushindi wa mpinzani wako. Pengine hakumshawishi vizuri au alimshawishi ila Sera akaziona hazina mantiki.

Nashauri Chadema itafakari ni wapi inakosea.
 
Makamanda, tunasikitika kuwatangazia chama kimepoteza kamanda mwenzetu Timotheo Paul (28) ambaye alifariki jana hospitalini Bugando kutokana na majeraha aliyopata akiwa kwenye kampeni Kata ya Kimwani, Muleba Kagera.

Alikuwa kiongozi wa Bavicha katika kata hiyo. Kutokana na mazingira ya kifo chake, chama ngazi ya kanda ya ziwa Viktoria kimesafirisha mwili wa marehemu kwa kutumia gari la kanda leo alasiri.

Hivi ninavyoandika, msafara ndio unakaribia Kimwani. Waliosindikiza mwili huo wakiambatana na ndugu wa marehemu, ni Meshack Micus, Katibu wa Kanda, na Khalid Selemani, ofisa katika ofisi ya kanda.

Kamanda Timotheo amefia kazini. Amekufa kwa heshima. Tumwombee huko aendako alikotangulia. Mungu amweke mahali pema!

Taarifa nyingine zitafuata kadiri zitakavyotufikia.

Hapo hapo, huko huko Kimwani, kijana mwingine amezikwa leo. Huyo alifariki kwa ajali siku ya uchaguzi.

Kutoka Nkome, Geita, kuna kijana aliyejiua Jumapili siku ya uchaguzi baada ya matokeo, alipomwona mama yake mzazi anashangilia ushindi wa CCM. Kijana (jina lake halijapatikana bado ). Alijinyonga .

Mungu awape faraja wafiwa!. Na aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. AMEEN

............................................
ANSBERT NGURUMO
Makamu Mwenyekiti CHADEMA

Kanda ya Victoria
Poleni wafiwa. Ila Gurumo acha kuanzisha threet ya kichochezi tufanye siasa Zenye tija na siyo siasa za majungu ila sishangai kwa kuwa Wewe Mla senene kawaida yenu
 
Huyo aliyejinyonga Kwa sababu ya mama yake mzazi kushangilia ccm khaa I can't imagine that is very ridiculous
 
Back
Top Bottom