Tanzia: Sheikh Omary Alhad wa msikiti wa Kichangani Magomeni, afariki dunia

Uungwana Vitendo

JF-Expert Member
Nov 20, 2013
1,322
507
INNALILLAHI WA INNA ILAIHI RAJIUN!

Sheikh Omari Alhadi, Imamu wa msikiti wa KICHANGANI Magomeni mapipa amefariki leo. Mazishi tutataarifiana inshaalah!


========

SHEIKH OMAR ALHAD AFARIKI DUNIA

Taarifa zilizotufikia punde zinasema Mhadhiri maarufu na mtoa khutba wa msikiti wa Kichangani wa jijini Dar es salaam sheikh Omar Alhad omar amefariki leo muda wa mchana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

attachment.php


Sheikh Omar alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya figo kwa muda mrefu.Sheikh omar ni mdogo wa Imamu wa Msikiti wa kichangani na ni mtoto wa Sheikh Alhad omar.

Sheikh Omar aliyezaliwa miaka 44 iliyopita elimu yake ya dini alianza kuipata kwa mama yake, Bi kijakazi maarufu kama bi 'Mwalimu'.

Sheikh Omar aliyekuwa kipenzi cha watu ameacha mjane na mtoto mmoja wa kike. Mwenyezi Mungu amuweke mahala pema peponi.

Taarifa zaidi za taratibu za mazishi endelea kufuatilia blogu yako ya Ahbaabur Rasuul.


Chanzo: Ahbaabur blog

updates
kwa wasiojua ni kuwa omary Alhad anatokea ktk familia ya wanawazuoni yeye na kaka zake na dada yao wote mungu amewajaalia .ni kama unavyoona familia zingize za wanamichezo,siasa ila kwa familia hii baba ,mama na watoto wote ni walimu wa dini.Omary ndiyo khatibu wa msikiti wa kichangani na kaka yake ndiyo.wapo wanne kaka yao alishafariki anakuja Shekh Walid Alhad ambaye ni Imamu mkuu Kichangani, Omary ni watatu na wa nne ni dada yao .Ni msiba mkubwa kwa waislamu tumwombe mungu aipe subra familia na waislamu wote.
ataswaliwa kesho msikiti wa Kichangani na kuzikwa katika makaburi ya Mwinyimkuu saa kumi al asir inshaallah.kama kutakuwa na mabadiliko yoyote tutajuzana.
 

Attachments

  • omar alhad.jpg
    omar alhad.jpg
    16.7 KB · Views: 3,783
Mungu wa upendo awajalie wafiwa moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Atukumbushe na sisi pia kuhesabu siku zetu maana tu mavumbi na mavumbini tutarejea kusubiri mapambazuko ya asubuhi njema
 
Al hamdullilah....mchango wake ni mkubwa saana na khotuba zake siku za Ijumaa zikikuwa nzuri saana.ALLAH amsamehe makosa yako
 
Back
Top Bottom