TANZIA Ruge Mutahaba afariki Dunia! Azikwa kishujaa kwao Kabale, Bukoba

Ndugu yangu Mkuu The Invincible, hakuna haja ya kutukanana "kenge wewe" na kuwahukumu marehemu wa watu, waachwe wapumzike, anayetoa huku ni Mungu mwenyewe, na hivi vitu ninavyowaambia hapa nyinyi wafia dini, usiviite vya kijinga, kwa sababu haya ninayoyazungumza humu ni mafundisho yake YEYE mwenyewe, ametufunza, "Tutaokolewa kwa neema na sio kwa matendo", hivyo hata mtu awe aliishi kihuni vipi na kanisa kugoma kumzika kwa heshima zote, wakovu haitokani na matendo yake bali ni neema tuu. Na wote wanaozikwa kwa sala na misa Takatifu, sio kigezo kuwa wao ndio wataenda mbinguni.
Mwacheni Ruge apumzike, tusinyooshe vidole na kumhukumu kwa maisha yake, yale ni maisha yake, ajuaye ya mbele ni Mungu pekee.
P
Haya baba nimekusikia.
 
Kwa heshima zote za kiserikali na kibinadamu na mapokezi aliyopata Marehemu Ruge, Je, alisitahili kuzikwa kwa ibada kuendeshwa na KATEKISTA?

Ukitilia maanani ukaribu wa familia ya marehemu na Askofu M. Kilaini

Ujirani uliopo kijijini kati ya Askofu na Prof. Mutahaba

Mazingira ya mwamko wa kidini ya RC uliopo hapo kijijini

Ujirani na Parokia yake ya Itahwa

Ushiriki wa viongozi hao wa dini katika kuaga mwili wa Marehemu hapo Bukoba Club/Gymkhana

Mwisho wa Mwisho ibada ya mazishi ikaishia kuendeshwa na KATEKISTA ikishuhudiwa viongozi hao wa kanisa kushindwa kushiriki ibada hiyo.

Kwanza Sio utamaduni wa eneo hilo kwa mtu kama wa aina ya Mutahaba.

Mwisho wa RUGE imekuwa simanzi kubwa kwani mbwembwe za mitaani zimezimwa na KANISA lake.

The very last RESPECT imeua yote.
Matendo ya Mungu si ya mwanadamu amestahili alichopata kulingana na ushiriki wake katika mambo ya kiroho... Alichopata kinaitwa minimum service

Jr
 
Pole nyingi sana kwa Zama na watoto wake, mapito anayopitia kwakweli ni Mungu tu ndio anajua.
Iliwahi kunitokea aisee nikaachiwa mtoto wa miaka miwili yaan sijawahi kusahau mpk leo. Nilikuwa naona kila kitu kibaya, nilitamani ht niache kazi ili niwe najifungia tu ndani.
Nikiona picha ya Zama na watoto wake nakumbuka kbs jinsi ilivyokuwa kwangu na mtoto wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Oooh pole mkuu...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msianze...
Kinachomuingiza binaadamu mbinguni au motoni, sio misa yako ya wafu imeendeshwa na nani, au watu wamekulilia vipi, bali tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo.

Kwa mujibu wa the law of the karma, Ruge as of now, ameingia peponi straight kwa mengi mengi aliowatendea watu hapa duniani.

Siku ukifika mbinguni, unaweza kushangaa kuwaona hao maaskofu motoni, halafu yule Katekista ndio ukamkuta peponi.

Hata kimataifa, unaweza kumkuta Bush, Blair na Obama, upande wa chini wakiogelea kwenye lile ziwa la jehanum ya moto was milele, halafu ukashangaa kuwakuta Osama, Saadam na Ghadafi wakiwa peponi wakienjoy.
P
-1.Usiingize karma wakati issue ni christianity
-2.Afadhali yaliyomkuta Ruge amepata katekista kuliko yalimkuta tajiri wa ngurudoto(waligoma kumzika kisa ushiriki wake kanisani)
 
Wabongo wanyime chakula, si majungu. Azikwe na askofu, padri, mchungaji, shehe ama katekista, roho yake imeenda mahali alipostahili, kilichozikwa ni mwili tu ambao utaoza na kuliwa na udongo
 
Msianze...
Kinachomuingiza binaadamu mbinguni au motoni, sio misa yako ya wafu imeendeshwa na nani, au watu wamekulilia vipi, bali tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo.

Kwa mujibu wa the law of the karma, Ruge as of now, ameingia peponi straight kwa mengi mengi aliowatendea watu hapa duniani.

Siku ukifika mbinguni, unaweza kushangaa kuwaona hao maaskofu motoni, halafu yule Katekista ndio ukamkuta peponi.

Hata kimataifa, unaweza kumkuta Bush, Blair na Obama, upande wa chini wakiogelea kwenye lile ziwa la jehanum ya moto was milele, halafu ukashangaa kuwakuta Osama, Saadam na Ghadafi wakiwa peponi wakienjoy.
P
Heri kukaa kimya kuliko kuandika vitu usivyokuwa na uelewa navyo wa kutosha.

Mambo ya Mungu sio siasa mzee.
 
You are surely a poor and bad teacher.
Kuna nilicho ongopa hapo? Au wabakaji ni makadinali na mapadri wa Ulaya, Marekani, Australia, na Amerika ya kusini tu? Hawa wa Afrika na Asia i watakatifu? Ni mila na tamaduni zetu kandamizi ndo zinafanya waliobakwa hawajitokezi. Na naimani huu ubakaji unaendelea mpaka sasa.

Sishangai juzijuzi tu tumejuzwa ubakaji na unyanyasaji kijinsia unaendelea kushamiri Tanzania na wazazi kwa upumbavu wao wanamalizana kimyakimya na wabakaji.

Jana wanafunzi wa chuo kikuu cha mtakatifu Agustino Mwanza wametoka kumlilia Ole Nasha wananyanyaswa kijinsia kutakwa ngono na mtu waliyemtaja hadi kwa jina, kwa miaka 3 wanalalamika uongozi wa chuo hauchukui hatua.

Tukubali tusikubali, tuna mila potofu na kandamizi na kuna taasisi kubwa kama kanisa katoliki zinazitumia kuendeleza maovu...
 
Tena kuna wafia dini wa ajabu sana, Biblia zipo, maandiko yapo, mafundisho yapo, mfano mzuri ni kuhusu ibada za masanamu, watu wanawaaminia sana binaadamu, wanamtumikia shetani wakiaminishwa ni Mungu, bila wenyewe kujijua, sisi Wakatoliki tuliojitambua, tunamwelewa sana mtu kama Ruge kukataa ujinga ujinga fulani in the name of Catholic Church, zimewekwa sheria kibao ati usipofanya hivi, siku ukifa hatukuziki!.
Tena kitu cha ajabu ni wanafanya Cherry picking, kwa kuangalia status.
Angalieni msiba huu wa kigogo huyu walifanya nini na sikilizeni rais Magufuli alisema nini juu ya mtu huyu na bado alizikwa kwa heshima zote za kanisa, tena kwenye Hilo mimi meshauri
"Pongezi Rais Magufuli Kuwa Mkweli Daima. Tuanzishe Church of Africa, Tuoe Wake Wengi, Tuzae Watoto Wengi?" - JamiiForums
P
Mtume Pasco,

Mimi ni mumini wa kanisa katoliki, kanisa kuna Sanam za bikria Maria naYesu kadhalika sala ya mama Maria utuombee sisi wanao! na kuna swala la kumuungamia Padri hili limekaaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msianze...
Kinachomuingiza binaadamu mbinguni au motoni, sio misa yako ya wafu imeendeshwa na nani, au watu wamekulilia vipi, bali tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo.

Kwa mujibu wa the law of the karma, Ruge as of now, ameingia peponi straight kwa mengi mengi aliowatendea watu hapa duniani.

Siku ukifika mbinguni, unaweza kushangaa kuwaona hao maaskofu motoni, halafu yule Katekista ndio ukamkuta peponi.

Hata kimataifa, unaweza kumkuta Bush, Blair na Obama, upande wa chini wakiogelea kwenye lile ziwa la jehanum ya moto was milele, halafu ukashangaa kuwakuta Osama, Saadam na Ghadafi wakiwa peponi wakienjoy.
P
Kwa taratibu za kanisa katoliki Ruge hakuwa na sifa ya kuzikwa na ibada ya ekaristi au misa. Ibada hiyo ndiyo nguzo kuu ya kanisa na ndiyo inayoliweka imara, licha ya misukosuko, kwa miaka zaidi ya elfu mbili. Ruge hakuwa mtiifu kwa kanisa au kwa kifupi alikuwa mkanamungu katika maisha yake hivyo ingekuwa ni kutomtendea haki kumshirikisha katika ibada ambayo hakuishiriki kikamilifu au kuiamini wakati uhai wake
 
Huko instagram wananzengo wanasema ruge kapewa sumu ya muda mrefu.

Ata alivyokwenda india walimuambia labda ajaribu SA matibabu.

Haikuwa tatizo la kubadili organ tu,
Wanasema alichukulia poa sana tatizo lake muda alioanza kuhangaika nje ilikuwa late

SIO MANENO YANGU , NMEONA INSTAGRAM kwa theoriginaleast

Sent using Jamii Forums mobile app

Udaku tu wa mitandaoni
 
Ruge na Kingunge wote sawa. Hawakulijua kanisa wala kuishi imani yao. Maziko waliyoyapata ndiyo heshima waliyostahili. Hakuna Misa Takatifu ya mazishi. Ni Sala tu ya kuongozwa na Katekista. Ndilo Kanisa Takatifu, Katoliki la Mitume. Halibagui wala kupepesa macho. Safi sana. Fanya fiesta lakini kumbuka kusali na kuhudhuria Misa Takatifu.
Kwahiyo ukifanyiwa misa takatifu ya mazishi hata ukiwa na dhambi unaenda mbinguni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Neema is The Lord's Grace, tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo

Karma ni hukumu ya haki kwa mawazo yako, maneno yako na matendo yako.
Kuokolewa kwa neema maana yake Mungu anatuona hadi ndani ya mioyo yetu na dhamira zetu. Hivyo kuna watu wanafanya mema ili tuu watu waone, lakini moioyoni mwao ni mashetani wakubwa. Hawa hata wafanye wema mkubwa kiasi gani, haijalishi.

Kuna watu with nothing, kama mimi nilivyo, ni masikini wa kutupa and yet I'm a rugged trousers philanthropist, Mungu anaona moyo wangu wa kusaidia. Hivi ndivyo alivyokuwa Ruge,
Ni peponi straight, by now tayari yuko mkono wa kuume wa Mungu Baba Mwenyezi, Muumba wa vitu vyote vinavyoonekana na visivyo onekana.
P
Wacha kusemea maisha ya watu, huna tofauti na yule mfarisayo aliejipiga kifuani akisema mumi sio kama hao wengine wacha kujikweza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1. Sala ya Toba anaongozwa mtu???
2. Huyo anaeongoza Una uhakika yeye hana Dhambi??
3. Yule mnyang'anyi aliesulubiwa na Yesu msalabani lakini akatubu na kusamehewa dhambi alitubu moyoni au alisubiri mtu aje amuongoze kwa sala??
4. Wewe mwenyewe unapaswa kufanya Toba na Mola wako. Askofu, Mchungaji,Sheikh hana Mamlaka ya Kumuombea mtu msamaha
5.mtu akishakufa Kumbukumbu yake imesahaulika hata aje Paroko kumuombea hakuna kitu.
6. Hizo misa za kuwaombea Marehemu mnajisumbua tu. Nipe fungu la Biblia linalotaja Marehemu waombewe
Je, hatuwezi kupunguza mateso ya roho za marehemu waliokwenda toharani?
Ndiyo: twaweza kupunguza hata kuyamaliza kwa kuwasalia na kuwapatia rehema na hasa kwa kuadhimisha Misa kwa ajili yao. (2Mik 12:38-46)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom