Magoiga SN
Member
- Oct 15, 2016
- 15
- 61
Magoiga SN
Sina mengi ya kusema kuhusu Peter Kalihose, kijana aliyeweka mbele maslahi ya taifa katika kupigania kile alichokiamini tena kwa kujitolea. Wengi waliotofautiana nae walimuona kama 'Conservative' lakini Peter aliamini Tanzania yenye Amani ni muhimu ktk maendeleo ya nchi kuliko kuiacha nchi kutumbukia ktk migogoro.
TAR 31 Desemba, Peter aliandika maneno yafuatayo Facebook "Maisha....Baada ya KUISHI (maisha) nini hufuata? (Kuna aliekwishafikiria kwamba maisha aliyoishi yanatosha)?" Kwa ufupi Peter alijua muda wake ulikuwa umefika, na alituaga kwa lugha nyepesi na ya kutufanya na kutukumbusha kuyatafakari maisha.
Peter alikuwa ni moja ya kiungo muhimu katika mchakato wa uanzishwaji wa CCM-Tawi La Mitandaoni. Alishauri kwa ukaribu na hata kupendekeza namna bora ya kujenga Tawi lenye watu wanaotambua maslahi ya taifa. Peter mara zote alisema, CCM ikitekeleza ahadi zote ni heshima kwangu kama mwanachama, na inanipa kiburi cha kutembea kwa madaha na kujiamini. Hivyo ni wajibu wetu kukisaidia chama na serikali yake kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.
Siku zote aliwashauri vijana kuhusu kuanza kubadili mitazamo ya matumizi ya mitandao ya kijamii na kuanza kuitumia kuanzisha biashara kama Chachu ya kujiingizia kipato na kupambana na umaskini. Aliwahimiza vijana kwa kusema ni vyema ukae Online masaa 10 kwa siku ukiwa unaitangaza biashara yako au unauza bidhaa zako, au unawasiliana na wateja wako na kujibu maswali yao kuliko kutumia masaa 10 Online kwa siku bila mitandao ya kijamii kukusaidia kuingiza kipato.
Ndiyo, leo hayupo nasi tena. Amefikwa na mauti akiwa nchini Uganda ambako ilikuwa moja ya sehemu alizokuwa akifanyia kazi zake.
CCM Tawi la Mitandaoni Itaukumbuka Mchango wako Daima,
R. I. P Pater Kalihose