Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,944
- 69,530
BAADA YA TUZO YA WACHEKESHAJI. SERIKALI NA WADAU IANDAE TUZO ZA WAANDAJI BORA WA MAUDHUI MITANDAONI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Niwapongeze waandaji wa Tuzo za Wachekeshaji 2025, serikali na Wachekeshaji wote walioshinda Tuzo hizo.
Mimi ni mdau wa vichekesho hasahasa Standup Comedy kuanzia Watubaki na Cheka Tu. Wapo Wachekeshaji baadhi kutoka Standup Comedy ya Watubaki na Cheka Tu ambao mara kwa mara huniomba niwasaidie kuwaandikia contents za vichekesho au baadhi hao wakiona nimeandika makala yenye. Kuchekasha huwasiliana na Mimi wakiomba walitumie andiko langu kwa Kazi Zao hizo.
Niwapongeze Wachekeshaji wote ambao walikuwa ma moyo wa uungwana, kwa kuona sio Busara kuchukua andiko la mtu mtandaoni na kulitumia jukwaani pasipo kumshirikisha Mwandishi wa andiko Hilo.
Ninafahamu wapo waandaji wengi wa maudhui mtandaoni ambao Mawazo au maandiko Yao huchukuliwa sio tuu na Wachekeshaji Bali watu mbalimbali kwenye sekta mbalimbali. Sekta ambazo zipo connected na Mitandao ya kijamii ni kama vile Sekta za utangazaji wa vipindi vya Luninga na Redio. Kuna wakati baadhi ya waandaji wa maudhui haya humu JF walikuwa wakilalamika kuchukuliwa maudhui Yao na baadhi ya watu pasipo uungwana. Hili sio lengo langu kwa siku hii ya Leo.
Dunia ya Leo imebadilika Sana. Mambo Mengi Sana yanafanyika mitandaoni. Mapinduzi ya kifikra, kielimu, kisanaa, Kibiashara ,kisayansi, miongoni mwao mambo mengine yanatokea mtandaoni.
Waandaji wa maudhui mtandaoni wamekuwa chachu kubwa katika kuijenga, kuiboresha na kuiburudisha jamii.
Nilishasema karibu Sekta zote hapa Tanzania na Duniani kwa ujumla zinachukua Mawazo kutoka mtandaoni.
Siku hizi mtu akitaka Jambo lolote ni anaingia mtandaoni ana - search tuu. Vitu vinakuja. Vitu hivi tunajua havikujiweka VYENYEWE. Wapo watu waliotumia Muda, vipaji, ubunifu na wakati mwingine gharama kuviweka mtandaoni kwaajili ya Jamii na Dunia.
Kupitia uaandaji wa maudhui mtandaoni mambo yafuatayo yametokea;
1. Vijana wengi wamepata Elimu na mafunzo.
Waandishi wa Makala, Stori, Historia, wawekaji wa picha, Memes, video za mafunzo na burudani wameisaidia jamii Kupata Elimu na mafunzo mbalimbali.
2. Ajira na Ubunifu katika Ajira
Ninakuhakikishia kuwa asilimia kubwa ya mambo mengi yanayoendelea kwenye mini Mikubwa yametokea mtandaoni.
Vijana wamejiajiri mtandaoni na wapo ambao wametumia Mawazo ya mtandaoni kujiajiri au kubuni na kuboresha biashara au miradi Yao.
3. Chanzo cha Ideas Mbalimbali;
Tunajua kwa sasa ajira zimekuwa changamoto. Vijana wengi kwa sasa kimbilio Lao ni mtandaoni kuangalia ni idea gani wanaweza kufanya.
Vijana wengi kupitia mtandaoni wamepata Idea za nini wafanye katika maisha yao. Na kwa kufanya huko wamebadilisha maisha yao na serikali imejipungizia Mzigo wa vijana wasio na Kazi na inajipatia kipato.
4. Utoaji na Upataji wa taarifa.
Ni kupitia mtandaoni vijana na jamii kwa ujumla inashare taarifa mbalimbali. Serikali nayo inatoa na Kupata taarifa kutoka kwenye mitandao ya kijamii.
5. Burudani
Mitandaoni siku hizi ni chanzo namna Moja. Narudia chanzo namba Moja cha burudani. Yapo maudhui mbalimbali yanayowekwa mtandaoni yanayoburudisha. Hili hakuna mbishi.
Waandaji wa Memes, vichekesho, maudhui ya maandishi yanayoburudisha kama tamthilia, riwaya, ushauri.
Michezo, Uimbaji, na aina zote za kazi za ubunifu zinazoburudisha zinalisaidia Sana taifa letu Kwa namna nyingi Sana zenye Tija.
Na mambo mengine kama hayo;
OMBI LANGU KWA WADAU NA SERIKALI KULIONA JAMBO HILI NA KULIFANYIA KAZI;
Wadau na serikali ilitazame Jambo hili na kuanza mchakato mara Moja angalau kwa Mwaka Mara Moja, kuandaa Tuzo za Waandaji wa maudhui Bora Mitandaoni ambayo yanatija kwenye jamii na taifa letu.
Sio kwamba Taikon Master nataka kujipakulia Minyama kwa Sababu nami Niko huku Lakini ni katika kuzingatia ule ukweli usiojificha ya kuwa waandaji wa maudhui mtandaoni mchango wao ndani ya Jamii yetu upo wazi kabisa kwa matabaka yote na watu wa hadhi zote ndani ya Jamii yetu.
Ni ukweli usiopingika kuwa kuna watu wanaathiri maisha ya watu positive na kuyabadilisha kupitia maudhui Yao mitandaoni.
Maelfu ya watu wamebadili mitazamo Yao hasi na kuwa Chanya kupitia maudhui ya mitandaoni.
Baadhi ya Mahusiano ya watu ndani ya familia yameimarika kupitia maudhui ya mitandaoni.
Baadhi ya watu wameboresha afya Zao kwa kufuata maudhui ya mitandaoni.
Baadhi ya maelfu ya watu wamekuza fikra Zao kupitia maudhui ya mitandaoni.
Wanasiasa na watawala wengi wamejifunza mambo mengi ya uongozi na utawala kupitia maudhui ya mitandaoni.
Sasa kipi kinatufanya wadau na serikali kutoandaa Tuzo kwa Watu hao ambao wanalisaidia taifa?
NAPENDEKEZA TUZO HIZO ZIWE KATIKA MGAWANYO UFUATAO;
1. Muandaaji Bora wa maudhui ya Uchumi na biashara mtandaoni
2. Muandaji Bora wa maudhui ya Masuala ya Jinsia mtandaoni.
3. Muandaji Bora wa Maudhui ya Ujenzi Mtandaoni
4. Muundaaji Bora wa Maudhui ya Masuala ya siasa na utawala Bora mtandaoni
5. Muandaji Bora wa maudhui ya kijamii mtandaoni
6. Muandaji Bora wa maudhui ya Masuala ya Magari Mtandaoni
7. Muundaaji Bora wa Maudhui ya Mahusiano na Familia mtandaoni
8. Muandaaji Bora wa Maudhui ya Sayansi na Teknolojia mitandaoni
9. Muandaji Bora wa mitindo na Ubunifu katika Mavazi mitandaoni
10. Muandaji Bora wa maudhui ya Kilimo na ufugaji mtandaoni
11. Muandaji Bora wa maudhui ya uchambuzi wa Michezo na burudani mtandaoni
12. Muandaji Bora wa maudhui ya Memes mtandaoni
13. Muandaji Bora wa maudhui ya Katuni na Memes mtandaoni
14. Muandaji Bora wa maudhui ya Fasihi mtandaoni
15. Muandaji Bora wa maudhui ya taarifa za kiunguzi na muibua mambo kwenye jamii mitandaoni.
Na Tuzo zingine kadiri itakavyowezekana. Zinaweza kuongezewa au kupunguzwa kulingana na umuhimu na Hali.
Ninakiri, wapo watu mitandaoni hasa humu JF wamekuwa Baraka Sana kwenye jamii yetu. Binafsi wamenijenga Sana. Kuanzia kiuchumi, kijamii, kisiasa, kihistoria n.k.
Sio ajabu mara kwa mara kila mwisho wa mwaka huwa naamua kuchukua nafasi ya angalau kuwataja top ten ingawaje wapo wengi katika namna ya kuwatambua na ku- appreciate Kazi Njema wanazozifanya.
Ninajua Mawazo Mengi yaliyopo mitandao mengine yenye asili ya Watanzania Mengi Kati ya hayo huanzia hapa Jamiiforum kisha wengine huyachukua na kuyapost katika mitandao mingine.
Kufikia hapo Sina la Ziada. Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam