TANZIA: "PAKA MAPEPE" wa ToT amefariki DUNIA.

TUJITEGEMEE

Platinum Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
27,504
Reaction score
28,436
Msanii huyu amefariki leo asubuhi baada ya kujifungua. Mungu alilaze mahali pema peponi.

Source: M/kiti wa CCM taifa kupitia TBC/ITV
 
Pole nyingi kwa Baba wa mtoto aliyeachwa, kwa mtoto mwenyewe, wazazi, ndugu na marafiki wa "Paka Mapepe". Hakika inauma sana. Kweli hakuna kifo kizuri hata kimoja. Lakini kuna uchungu mwingine huzidiiiii! Hembu fikiria, mtoto hajanyonya, hatamjua mama yake maisha!!! Malengo ya dada huyu katika maisha yamesimama ghafla!!! Lakini sasa utashangaa kusikia "Kazi ya Mungu haina makosa", "Mungu amechukua kiumbe chake" ; "Mungu kachuma ua lake" ; "Kama uliandikiwa...." n.k. n.k. Jamani, hembu wana JF tutafakari kidogo. Huyu Mungu, ambaye tunajua ni Mungu wa Upendo na Rehema na Fadhili, amemchukua mama mara baada ya kujifungua!!!! Kichanga kiteseke? HAKIKA, SI MUNGU KACHUKUA KIUMBE CHAKE. Hii ni kazi ya IBILISI. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo wa wanadamu, na ameendelea kuua, halafu ni mwongo, na anaendeleza uongo wake.Yohana 8:44. Tumlaani Ibilisi na malaika zake. Mungu atakikomesha kabisa kifo kisiwepo milele. Ufunuo 21:3,4. Nawatakia siku njema.
 
"Hii ni kazi ya Ibilisi" - Kuamini hivi Ni ushirikina

"MUNGU atakikomesha kabisa kifo kisiwepo milele" - Ni nani???? Mungu au Ibilisi?,

Ki-text: unajichanganya, wewe hata hili neno Mungu hapa halikuzindui kwamba ni yule mwenye kuweza kukiumba tu ndie anaeweza kukikomesha?

Ki-context: Wewe hii aya yote umeichukulia very literally, na kwa hiyo umejichanganya kwa mara nyengine tena. Maana wewe mwenyewe unajua hakika kwamba kila nafsi ina siku yake na itakufa. Kama ni kumlaani ibilisi basi Mitume na Manabii wanacho au walikuwa na cheo cha juu zaidi ya yeyote katika kuwalaani ibilis, na wamekufa. Vile vile siyo wewe, siyo mimi, siyo mchungaji, siyo kadinali, siyo Papa, siyo imamau, siyo shehe, hata umlaani ibilisi namna gani, basi siku ipo utakufa tu. Je unapinga hili??? Wooooooote ni lazima tuonje mauti, hivyo inaonyesha ya kwamba wewe mwenyewe hukufahamu maana ya hii aya yako hata kidogo, unajipinga, unajichanganya.

Je unaweza kuitafutia tafsiri yake au watu wanaoijua wakusaidie??
 
Jamani, picha yake.
5417682.jpg

Source>>>TOT Kumtambulisha 'Paka Mapepe' Kwa Washabiki Wake
 
Eeeh,kifo cjake kinatangazwa na mwenyekiti wa ccm taifa?
Basi walau anajua wanawake wanakufa wakati wa kujifungua,yatosha. Huenda akaleta badiliko.

Poleni wafiwa na fans wote

Back
Top Bottom