TANZIA: Mwimbaji mkongwe wa taarab, Bi. Shakila Saidi afariki dunia

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
69ada31e-1adf-4a4e-8274-2e69ccb43e75.jpg

image.jpeg

Shakila Saidi enzi ya uhai wake akipeana mkono na aliyekuwa Rais wa JMT, Mh. Kikwete

Amefariki leo saa tatu usiku (19 Agosti) hospitali ya Temeke.

Marehemu alitoka safari juzi, na leo ameanguka huko nyumbani kwake, aliwahishwa hospitali ambapo umauti umemkuta.

Marehemu Shakila ameacha familia ya watoto 13.


============

Updates:

Shakila alilelewa na Bi Kidude na alianza kuimba nyimbo za kihindi huko Tanga baadae alitamba na Black Stars ya Tanga na JKT Modern Taarab.

Tutamkumbuka kwa vibao vyake kama Kifo cha Mahaba, Macho Yanacheka, Pazia, Kitanda Kuwekwa Kati Tatizo Nini? Mzingo, Bunduki Iso Risasi na nyingine nyingi.

Ameacha pengo katika tasnia lakini kwa mungu tunatoka na kwake tutarejea.

Hii niHistoria yake fupi aliyoitoa kwa Waandishi wa habari wakati wa Uhai wake MARCH 16, 2013...

Bi Shakila Mwasisi wa taarabu aliyesimama jukwaani kwa zaidi ya miaka 40

-Aliolewa mwaka 1960 akiwa na umri wa miaka 11

-Alifanya kazi kama mwimbaji Bendi ya JKT kwa miaka 40, alianza muziki mwaka 1961

-Amejaliwa kupata watoto 13, aliozaa na waume wanne

-Alistaafu muziki akiwa Bendi ya JKT mwaka 2009, sasa hulipwa ujira wa Sh 3000 kama nauri akifanya onyesho moja na JKT, anaishi kwa kuuza vitumbua,visheti

Dar es salaam.“'Macho yanacheka, moyo unaliaaa, macho yanacheka aeeh, moyo unalia, nikimkumbuka wangu my dear” Hayo ni baadhi ya maneno yaliyo katika wimbo aliouimba Bi Shakila alipokuwa na Bendi ya JKT miaka 1980 -1990, ambao ulijizolea umaarufu mkubwa ndani ya Tanzania na Afrika Mashariki.

Mkongwe huyo aliolewa mwaka 1960 alipokuwa na umri wa miaka 11 na mwanamume ambaye alizaa naye mtoto mmoja.

Shakila Said Khamis maarufu kwa jina la Bi Shakira ni mmoja wa waasisi wa muziki wa Taarabu nchini, ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Waimbaji wa Taarabu Tanzania.

Katika mahojiano na Starehe, Bi Shakila alieleza kuwa alianza kuimba taarabu sambamba na marehemu Saada Binti Saad, mwaka 1960 baada tu ya kuolewa na baadaye moja kwa moja alijiunga katika Bendi ya JKT aliyoitumikia kwa zaidi ya miaka 40.

"Nilianza muziki mwaka 1960 kabla ya Uhuru na nimekuwa huko kwa miaka mingi. Kabla ya kuanza muziki, nilimkuta marehemu Saada Binti Saad, Bi Kidude yeye nilimkuta akiwa tayari amejiunga na ngoma za Unyago, alikuwa bibi yangu na mtu wa karibu sana na mimi wakati huo nilikuwa na miaka sita.”

Hayo ni baadhi ya maelezo ya awali Bi Shakila katika mahojiano na Starehe nyumbani kwake Charambe, Dar es Salaam, kabla ya mfululizo ufuatao wa maswali na majibu na mwandishi wa makala haya.

Mwandishi: Hali yako kiuchumi kwa sasa ikoje?

Bi Shakila: Sina pesa, kiwango ninachokipata kama kiinua mgongo hakinitoshi kabisa. Nalipwa Sh80,000 kwa mwezi na NSSF, matumizi yangu kwa siku ni zaidi ya Sh15,000 kwa siku. Nilistaafu mwaka 2009, lakini mpaka sasa huwa naendelea na kazi yangu pale JKT mara chache na kama tukifanya shoo huwa napewa nauli Sh3000 inayonisaidia kunirudisha nyumbani. Kwa sasa hali yangu ni mbaya kiuchumi.

Mwandishi: Katika kipindi chote cha kazi yako hukuweza kujiwekea vitega uchumi, kama ndivyo sababu ni zipi?

Bi Shakila: Zamani muziki ulikuwa kama starehe, tulilipwa ujira mdogo na hata kukiwa na shoo tulipata ujira mdogo. Kwa sasa muziki ni ajira, tena kubwa kuliko ofisini, lakini umri umeshaenda sana na sisi wakongwe tunatamani haya yangekuwepo hapo nyuma, hii ndiyo sababu ya mimi kushindwa kuweka vitega uchumi.

Mwandishi: Unadhani Serikali inaweza kukusaidia?

Bi Shakila: Kabisa, sisi wakongwe hatuthaminiwi na tunatupwa jalalani, lakini watoto wadogo wavuta unga ndiyo wanasaidiwa, Msanii Ray C alienda mwenyewe kuvuta unga akijua kabisa ni kinyume cha sheria, lakini Serikali imemsaidia, kwa nini na sisi tusiangaliwe? Sisi ni dhahabu, wapo kina Mzee Gurumo, Small, Bi Kidude hivi sasa ni wagonjwa na wanahitaji msaada ila hawasaidiwi mpaka tufe ndiyo waje kutuzika?

Mwandishi: Pole! Wewe huamka saa ngapi na nini majukumu yako ya kutwa nzima?

Bi Shakila: Naamka saa 11 alfajiri kwa ajili ya kuanza kuandaa unga wangu wa vitumbua na maandazi, baada ya hapo naanza kupika. Alhamdulilahi, nina wateja kidogo wanaoniungisha. Saa4 asubuhi namaliza, napumzika kidogo na kuanza kuanza kutengeneza visheti hadi saa 12 jioni. Naoga, napumzika na wanangu tunazungumza mawili matatu kisha naenda kulala hadi kesho tena. Kama ninakwenda mazoezi JKT, basi siku hiyo ratiba yangu huvurugika kidogo. Biashara ya vitumbua nimeifanya kwa miongo minne sasa.

Mwandishi: Kwa kulinganisha na wakati wenu, unadhani taarabu ya sasa inakua?

Bi Shakila: Taarabu kwa sasa hakuna. Kwa sasa kuna rusha roho, mipasho, kiduku na khanga moja. Vitu hivi vimevamia na kuiharibu taarabu yetu. Zamani taarabu ilikuwa na ustaarabu na waimbaji tuliimba kwa staha na maneno yalikuwa ya kuburudisha na kusifia kitu fulani si sasa hivi. Hii wanaita Morden Taarabu mimi siikubali kabisa.

Mwandishi: Maisha yako ya ndoa yalikuwaje?

Bi Shakila: Niliozwa nilipokuwa na miaka 11. Mume aliyenioa kwa ndoa aliniacha mwaka mmoja baadaye kwa kuwa tulitofautiana kwa mengi. Aliniacha nikiwa na mtoto mmoja mchanga, hapo ndipo nilipoanza balaa hilo. Niliolewa tena na mume mwingine huyu niliishi naye miaka 18 na kuzaa naye watoto watano, mwaka 1975 alifariki, iliniuma sana nikakaa eda.

Baadaye niliolewa na mume mwingine, huyu nikazaa naye watoto watano na baadaye tuliachana. Nikaolewa tena kwa mara ya nne, nikazaa watoto wawili, nilipokuwa na mimba ya huyu mtoto wa mwisho mwaka 1993, mume akaniacha. Mwanangu wa mwisho Shani nilimzaa Ijumaa ya tarehe 27 Machi 1993. Tangu hapo niliwachukia wanaume na sijataka kuolewa tena mpaka leo.

Mwandishi: Waimbaji wa muziki wa taarabu waume kwa wanawake huoa sana au kuolewa na kuachika, tatizo ni nini?

Bi Shakila: Sijui, kwa kweli mimi siyo kwamba nilikuwa nikiacha wanaume, hapana ila walikuwa wakiniacha wao. Kwa upande wangu nahisi ilitokana na kuwa mwanamuziki na wakati huo muziki ulichukuliwa kama uhuni. Lakini huenda kuna sababu nyingine ambazo mimi sizijui.

Mwandishi: Tangu kustaafu umeshafikiria kufanya kazi ya muziki ukiwa mwenyewe?
Bi Shakila: Ndiyo, tangu nimestaafu nilianza kufanya kazi nikiwa na mwanangu na mpaka sasa nipo mwishoni kumalizia albamu yangu ya Mama na Mwana itakayokuwa na nyimbo nane. Kati ya hizo tano zimekamilika ikiwamo ya Mama na Mwana.
 
image.jpeg

Mwanamziki mkongwe wa Taarabu, Shakila Saidi amefariki usiku huu.

Mazishi yatakuwa kesho huko kwao Tanga.

Kwake Tumetoka, Na kwake tutarejea.

Msiba upo Mbagala Charambe nyumbani kwa marehemu. Hakuwa anaumwa, ameanguka na kufikishwa hospitali wakaambiwa amefariki.
 
Innalillah wainnah ilayh raajiuun,

Dah huwa sichoki kusikiliza nyimbo zake kama kifo cha mahaba,mapenzi yamepungua, kwa sauti tu tunasema mashallah,
Nilimsikia kwenye mkutano wa ccm akilalamika Maisha magumu kwa wasanii wakongwe,
Alale mahali pema
 
Haleyuya Tutaonana, Haleyuya Tutaonana, Tutaonana Mbinguni kwa Baba, Haleyuya tutaonana! X2
 
Back
Top Bottom