Tanzia: Mwanajamvi afariki Dunia.

Wana JF poleni sana. Nafurahishwa na jinsi tunavyokuwa pamoja kwa mambo ya msingi na mazito kama haya.

MUNGU AILAZE MAHALI PEMA ROHO YA MAREHEMU
 
Pakajimmy mm niko Arusha naomba unipe ramani ya kwenye msiba! au unipm namba yako nikupigie unielekeze mkuu, kiukweli roho imeniuma sana! maana leo yeye kesho sisi!
 
kaka hayo hapo juu ndio maneno yako ya mwisho kwangu! Akilini kwangu yatakaa! Na moyoni kwangu nitayaweka ,,nitajitahidi kwa nguvu zangu zote na kwa akili zangu zote na kwa moyo wangu wote nihudhurie mazishi yako! Japo nikuone kwa mara ya kwanza na ya mwisho ndugu yangu! Ulale salama wasaimon!
 
Nitawafahamisha mipango ya mazishi in case kama atazikwa Arusha. Kuna uwezekano mkubwa akasafirishwa kwenda kwao Mbeya.
 
R.I.P Mwanajamvi.
Mungu awafiriji nyote na kuwafanyia wepesi katika wakati huu mgumu
 
Kweli jamani dunia sio fair yaani ndio nimetika kumzika rafiki yangu kipenzi kafia labour alikuwa anafanya kazi Ardhi na amekufa na mtoto tumboni,nakuja jamvini nijiliwaze nakutana tena na Tanzia sijui niende wapi mimi jamani jamani Mungu wangu may their soul rest in peace jamani,mungu tusaidie
 

Pole sana. Tunapaswa tukumbuke kuwa kifo ni lazima kwa kila nafsi na hakuna anayejua saa ngapi kitamkuta. R. I. P wapendwa.
 
Ninawapa pole sana wanafamilia woote wa karibu waliofikwa na msiba huu Mungu watie nguvu na kuwafariji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…