Nimepigiwa simu jioni hii, dakika kadha zilizopita kuwa Mwanajamvi mwenzetu anayekwenda kwa ID ya wasaimon amefariki dunia muda kama dakika 45 zilizopita, katika hospitali ya Selian hapa Arusha, na sasa hivi ndiyo anaingizwa chumba cha ubaridi.
:A S cry::A S cry:
Taarifa hizo zinasema kuwa amenguka akiwa katika harakati za kuonana na Daktari, akiwa amesindikizwa na baba yake mzazi. Wasaimon alijiunga na jamvi 6.10.2010.
Binafsi nilikuwa nafahamiana sana na wasaimon, alikuwa ni mtu wa kutoa ushauri wa hekima sana kuhusiana na maisha ya miaka hii, na alikuwa mpiganaji asiyechoka, akitumikia kampuni mojawapo ya Tours mjini Arusha. Naelekea msibani, nitawajuza kinachojiri. wasaimon alivinjari hapa majukwaani hadi juzi 14.01.2013,na naambiwa kuwa hadi jana alikuwa mzima wa afya. Ameacha Mke na watoto 3.
Mungu Ilaze Roho ya Marehemu wasaimon Mahala Pema Peponi. Baadhi ya comment za wanajamvi:
1.
Janjaweed he was positive, God fearing, blessed na wa kupeana moyo. Its a loss, hasa kwa wakati huu ambao JF imejawa zaidi na watu type yangu
kaka hayo hapo juu ndio maneno yako ya mwisho kwangu! Akilini kwangu yatakaa! Na moyoni kwangu nitayaweka ,,nitajitahidi kwa nguvu zangu zote na kwa akili zangu zote na kwa moyo wangu wote nihudhurie mazishi yako! Japo nikuone kwa mara ya kwanza na ya mwisho ndugu yangu! Ulale salama wasaimon! [/quote]
UPDATE1. Mpaka sasa hivi (0940am)wanasubiriwa Baba zake wakubwa na wadogo ili wafanye kikao cha maamuzi ya mahala pa kuzika(kuna option mbili, kuzika Arusha au Kusafirisha kwenda kwao Mbeya).
Pia aliyekuwa Mwajiri wake yuko njiani tokea Nairobi, anakuja kusaidiana na familia kupanga hatima ya marehemu.
UPDATE 2.
MAZISHI NI JUMAMOSI (19/01/2013) HAPAHAPA ARUSHA, NADHANI KWENYE PUBLIC CEMETRY NJIRO. MTAKAOWEZA TAFADHALI TUWE PAMOJA SIKU HIYO.
UPDATE NO 3 (jumamosi/ D-Day ya Mazishi).
Ibada ya Mazishi itaanza mnano saa 6.00 katika kanisa la KKKT Usharika wa Kijenge(Kanisa lipo njiani tu, UKIACHA bARABARA KUU YA moshono, unapopanda Kijenge.
UPDATE NO 4.
Nina wanaJF kadha toka Mkoa wa Kilimanjaro wamewasiliana na mimi na tumebadilishana namba wakiniahidi kuwa watafika msibani...Karibuni sana ndugu zetu toka MOSHI.
UPDATE 5.
So Far tuna michango(ya fedha) ya WanaJF toka Arusha, Tanga, na Dar.
Tunawashukuru sana wote waliojitolea chochote kwa Mwitikio wao chanya!...
Hii inaashiria umoja na kwamba JF ni zaidi ya kuzikodolea macho screens zetu.
Michango yenu itafika kwa Mjane wa SAIMON kama mlivyoitoa.
UPDATE 6.
Mazishi ya mwenzetu yaliisha salama kabisa.
Umati uliofika kumzika Wasaimon ulikuwa mkubwa mno.
Hata hivyo tulishindwa kumfikishia salamu ama mjane kutokana na udhaifu na machungu aliyokuwa nayo siku hiyo. Muda wote alikuwa amebebwa, hajiwezi kwa namna yoyote.
Tumepanga kuwa tutasoma maingira na kwenda kwake siku nyingine ili kuwakilisha salamu zetu za rambirambi.
UPDATE 7
Natumia nafasi hii pia kumshukuru member mchakamchaka ambaye alihakikisha tunaonana eneo la tukio, na akaungana na sisi kuchangia senti za rambirambi kwaajili ya mjane.
Mungu akuongezee pale ulipopunguza.
8.FINAL UPDATE
Shukrani zangu nyingi sana kwa Filipo, LIVEPOOLFC, IGWE na anonymous mmoja(mwanajf ambaye alikuwa anawasiliana na mimi muda wote lakini hakutaka kuja usoni kwangu tufahamiane), kwa kuwakilisha tokea Mwanzo, kati hadi Mwisho wa matukio ya kumuaga mpendwa wetu Wasaimon.
Mungu atawabariki kwa muda na majitoleo yenu.
Nawasilisha,
Aksanteni. View attachment 80206
So Sad... Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi... Pole saana kwa familia yake yoote; Mwenyezi Mungu awape 'amani' na 'imani' katika wakati huu mgumu...
Ni pigo kubwa kwetu, hasa kwa watu wa Arusha ambao walikuwa karibu na member mwenzetu. Kilichobaki ni kuiombea roho ya marehemu ipewe mapumziko memo na kuomba pia furaja na moyo wa subira kwa ndugu na jamaa wa marehemu, Amina
This just comes to say that, what has happened cannot be changed,
But the grief and pain can be lessened by keeping the faith and hope
that life will be fair and just and the days ahead brighter.