Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,163
- 37,801
TANZIA: AHMED KATHRADA HATUNAYE
Mpinga ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini ya enzi hizo, AHMED KATHRADA amefariki dunia leo, akiwa hospitali jijini Johannesburg. AHMED Mohamed KATHRADA, rafiki mkubwa wa hayati Mandela, alikaa jela kwa miaka 26, 18 ikiwa katika gereza la Kisiwa cha Roben, jela nyingine aliowahi kutumikia kifungo kitambo hiyo ni Pollsmoor (Pozamoyo) Jijini Cape Town.
AHMED KATHRADA alihukumiwa jela sambamba na Nelson Mandela katika kesi ya kupindua nchi enzi za Utawala wa Makaburu, katika kesi hiyo walikuwa Jumla ya watu 8, baadhi ni Elias Motsoaledi , Walter Sisulu, Mhlaba, Mlangeni, Govan Mbeki (Baba wa Thabo Mbeki) na Denis Goldberg. Kathrada alitoka jela mwaka 1990, akiwa jela alikuwa anatumia namba ya Mfungwa Na. 468/64.
AHMED KATHRADA alizaliwa mwaka 1929, alipozaliwa panajulikana kama Schweizer Reneke, Transvaal, wazazi wake wote wawili walikuwa na asili ya India. Ni mwana-ANC, mpambanaji na aliwahi kuwa Mbunge. Nchini Afrika Kusina, AHMED KATHRADA ni maarufu sana kama Uncle Kathy.
Akiwa jela, jamaa alisoma university degrees zipatazo 4, BA (in History and Criminology), B Bibliography (in African Politics and Library Science), BA Honours (History) na BA Honours (African Politics). Mwaka 1994 Kathrada alichaguliwa kuwa Mbunge na pia akateuliwa kuwa Mandela's Parliamentary Counsellor. Aliwahi kutunukiwa tuzo kubwa kuliko zote katika ANC ijulikanayo kama “Isithwalandwe”.
Kwa walioangalia Tv wakati ule wa Msiba wa Mandela, hususani siku ya Mazishi, AHMED KATHRADA alitoa speech moja iliokuwa na hisia kali sana na ndiye yeye katika kuuelezea msiba wa Mandela alisema: “I have lost a brother!”
RIP AHMED KATHRADA.