RIP kamanda.
Kwa wale tuliokuwa makutupora JKT - 1993 OP vyama vingi - mtakumbuka kamanda wetu alivyokuja kujiunga nasi wiki moja kabla ya kucheza parade (kwata) ya kuhitimu kwa niaba ya kambi zote; pia mtamkumbuka jinsi alivyofanya vikao vyetu (Yeye mwenyewe na sisi makukruta) kupeleleza kama kulikuwa na unyanyasaji ndani ya jeshi la JKT. Ikumbukwe that time wazazi walikuwa wana wasiwasi kwamba jeshi lina unyanyasaji wa kijinsia; hili tuli-prove kwa kamanda kwamba hatujaona kitu kama hicho.
Kwenye PASS OUT parade - Platoon A - Section A - Mstari wa mbele Kulia kulikuwa na mwanaye Kwame! Poleni wafiwa. kwa niaba ya wahitimu wa Makutupola JKT nawakilisha, maana kamanda huyu alikuwa ni mzazi, akitutembelea tu tulisema kila kitu pamoja na adhabu zisizo na mantiki, kichele kidogo (monthly allowance), nk
Mgeni rasmi kwenye kwata letu la kuhitimu alikuwa mzee wetu Mh. Malecela - wakati huo akiwa Waziri Mkuu wa JMT.