mkolaj
JF-Expert Member
- Mar 24, 2014
- 3,023
- 1,092
![]()
Kocha Sylvester Marsh (kushoto), enzi za uhai wake alipokuwa Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa. Pichani akiwa na Kim Poulsen, aliyekuwa Mwalimu wa timu hiyo.
Aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars na kocha mkuu wa Kagera suger mwalimu Silvestre Marshi hatunae tena duniani.
Kocha huyo alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kipindi kirefu .
Poleni sana ndugu na jamaa pamoja na familia nzima ya tasnia ya mpira.
Pumzika kwa Amani Marshi, sote tupo njia moja.
Chanzo; #Sportzclub
=============
Enzi za Uhai wake, Marsh alianza kuwa Kocha Msaidizi wa timu za vijana Tanzania mwaka 2003 chini ya Alhaj Abdallah Athumani Seif kabla ya mwaka 2006 kupandishwa timu ya wakubwa, akianza kumsaidia Mbrazil, Marcio Maximo na baadaye Wadenmark, Jan Poulsen na Kim Paulsen.
Katika kipindi cha uongozi wa Rais Jamal Malinzi kushinda Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) aliondolewa kwenye benchi hilo.
Tangu hapo Marsh amerudi kufanya kazi katika kituo chake cha Marsh Academy mjini Mwanza, lakini mwaka jana ndipo maradhi ya saratani koo yalipoibuka na akaletwa Muhimbili kwa matibabu.
Mbali na timu za taifa, Marsh pia amefundisha klabu za Toto Africans ya Mwanza, Kagera Sugar ya Bukoba na Azam FC ya Dar es Salaam.
Miongoni mwa mafanikio yake akiwa kocha, mwaka 2005 aliiwezesha Kagera Sugar kutwaa Kombe la Tusker, ikiifunga Simba SC katika fainali mabao 2-1 Dar es Salaam.
Mwaka 2004, akiwa Msaidizi wa Kibadeni katika U17, maarufu Serengeti Boys, waliiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya kucheza Fainali za Afrika nchini Gambia, baada ya kuzitoa Rwanda, Zambia na Zimbabwe.
Hata hivyo, timu hiyo iliyoibua vipaji vya wachezaji waliogeuka nyota wa taifa kwa miaka 10 iliyopita kama Nizar Khalfan, Athumani Iddi , Amir Maftah na wengine, ilienguliwa fainali za Gambia kwa kashfa ya kumtumia Nurdin Bakari aliyekuwa amezidi umri.
Mwaka 2009, Marsh akiwa Msaidizi wa Maximo Taifa Stars, waliiwezesha timu hiyo kukata tiketi ya kucheza fainali za kwanza za CHAN nchini Ivory Coast.
Inaelezwa kwa muda wote wa Marsh kufanya kazi na timu za taifa hakuwahi kuwa na Mkataba.