TANZIA: Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Jacob Nkomola amefariki dunia

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,400
24,977
Arusha.

Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Jacob Nkomola amefariki dunia katika Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Nkomola ambaye aliteuliwa kuwa katibu wa chama hicho wilayani humo, Novemba Mosi mwaka jana akitokea Wilaya ya Musoma mkoani Mara, alifariki dunia jana saa moja asubuhi.

Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Omar Bilal na Katibu Mwenezi na Itikadi wa chama hicho mkoani hapa, Shaban Mdoe walithibitisha kutokea kifo hicho.

Bilal amesema Nkomola alifikwa na mauti hospitalini hapo alikopelekwa kwa matibabu baada ya kujisikia vibaya saa 10:00 alfajiri akiwa nyumbani kwake Dar es Salaam.

Chanzo: Mwananchi Online
 
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Musoma Mjini, mkoani Mara, Jacob Nkomola, anadaiwa kuhamasisha wafuasi wa chama hicho kufanya mauaji dhidi ya .. .
upload_2017-1-3_13-6-26.jpeg




ndo huyu? loh apumzike anapostahili
 
huyu alikuwa mmojawapo wa viongozi wa mwanzo wa CHADEMA akifanya kazi makao makuu ya CHADEMA miaka ya tisini baadaye wakaanzisha chama cha SAU na aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Dar es salaam Paul Kyara kabla ya njaa kuzidi na kutimkia CCM. RIP Jacob na pole kwa wanafamilia wote.
 
Back
Top Bottom