Ndugu wapendwa,
Wale wafanyakazi wote waliokuwa ATC na waliofanya kwenye ndege za serikali, asubuh ya leo tumeondokewa na mpendwa wetu capt. Chekingo.
Amefariki akiwa anafanya kazi ATCL.Ni wakati wetu kuombea wale ndugu na marafiki waliofikwa na huzuni hii kwa kushirikiana nao katika hali na mali kuweza kuulaza mwili wa marehemu kwenye nyumba yake ya milele.
Bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Mkuu GENTAMYCINE,
hata kwenye msiba wa mzee Madiba Rais Kikwete alikumbushia jinsi mzee alivyosahau boot zake tz na ambapo alipotoka jela akaomba apelekewe, na jinsi alivyomtania Mbeki arudishe passport yake ya tz aliyokuwa akitumia enzi hizo wakati wakipigana vita ya ukombozi. Kulikuwa na umuhimu kwa Kikwete kuzungumza haya?? Jibu ni rahisi, kwamba inapotokea taarifa ya msiba wa fulani, kila mtu aliyemfahamu marehemu au kufanya nae kazi humkumbuka kwa mambo tofauti tofauti waliyofanya nae.
Shark nae kaandika tukio lake analomkumbuka marehemu sijui nae utamwambiaje.
Jamanii eeh mwenyezi mungu ipumzishe roho ya marehemu Sam Chekingo pahala pema peponi amen. Wanazika wapi na lini au watasafirisha? Tujuzeni mliokwenda huko.
Mods hii futa futa ya post vipi tena siku hizi? Nimeweka picha watu wamtambue mumeitoa namna gani siku hizi? Huyu ni mtu mashuhuri sana jamani. Huyu hapa akipiga tumba
![]()