Tanzia: Capt. Chekingo wa ATCL afariki dunia

Tanzia: Capt. Chekingo wa ATCL afariki dunia

Pole kwa wafiwa, Mama Stella Fulgence Lubuva, Abdillai, Daudi. Ni habari ya mstuko hii, leo asubuhi nilikuwa napitia faili la kesi yake fulani hivi nikataka nimpigie tujadiliane.

R.I.P Captain
 
Huyu mzee namkumbuka sana alikuwa hakosi pale Octar's Pub pembeni ya French Embassy. RIP Mzee Chekingo
 
Chek in go huyo ndio kapteni CHEKINGO Pumzika kwa amani kapteni bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana libarikiwe
 
Pole sana kwa Brenda ,Cindy and Kanon!!!!
R.I.P dady ulikuwa mzee muelewa sana!!!!!!
 
Ndugu wapendwa,

Wale wafanyakazi wote waliokuwa ATC na waliofanya kwenye ndege za serikali, asubuh ya leo tumeondokewa na mpendwa wetu capt. Chekingo.

Amefariki akiwa anafanya kazi ATCL.Ni wakati wetu kuombea wale ndugu na marafiki waliofikwa na huzuni hii kwa kushirikiana nao katika hali na mali kuweza kuulaza mwili wa marehemu kwenye nyumba yake ya milele.

Bwana ametoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Nilikuona siku moja tu pale Nyuma ya French Embassy nilipokuja kumuona Rafiki yangu Abdi kuhusu issue za Insurance.

Mlikua wewe, Abdi , Mhindi mmoja Engineer , na Mzee mwingine .

Baadae nikamuomba Abdi anipeleke kwenye gari nikampe document, lengo ni kumsema mbona anakaa na Wazee tupu? Abdi akanijibu anajua anachopata from them.

Kurudi ukaanza kunipa issues za kumiliki mashamba Mlandizi na business zingine kibao, nikaamini Abdi asemacho.

Mwisho wa siku kumbe Capt ulilala bweni moja na Mzee wangu O-Leve, Songea, ukanipa salaam zake nimfikishie, pamoja na kunifahamisha Nickname ya Mzee ya wakati huo.

RIP Capt Chekingo!
 
R.IP. Capt Chekingo.Pole zangu kwa wanafamilia wote,Cindy na Ronald

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Bwana huyo Mwenyezi Mungu aiweke roho yake pema peponi marehemu namkumbuka enzi za Mgulani TMA mwaka 1974 tulipokuwa recruit kwa mara ya mwisho tulikutana naye Dodoma wakati huo alikuwa akiendesha na kurusha kariboo madege ya jeshi
 
Pole kwa wafiwa, Mama Stella Fulgence Lubuva, Abdillai, Daudi. Ni habari ya mstuko hii, leo asubuhi nilikuwa napitia faili la kesi yake fulani hivi nikataka nimpigie tujadiliane.

R.I.P Captain

Sasa Masuala tena Ya Kesi Sisi hapa Ya Nini? Tunamlilia Marehemu Wewe Unaleta Habari Ya Kesi! Haya Mpigie basi Hiyo Simu................................ RIP Captain Chekingo.
 
Tupo msibani na hanspope na l
awrence masha

Mpenda Misiba Je Nae Hayupo au Hajafika Hapo? Nyie Vijana Wa Hapo Morogoro Stores hadi Kilima N....ge Kurudi huku Mitaa Ya Mkadini hadi Shule Ya Oysterbay Hebu Nendeni Msibani Kwani Captain alikuwa Mtu Wetu Sana Mitaa Hiyo na Hata Kwa Wakazi Waishio ktk Iliyokuwa Nyumba Ya Marubani wa ATCL Nyuma Ya Karibu Hotel Nendeni Msibani Mkatuwakilishe. Poleni Sana Wafiwa!!!!!!!!!!!!
 
Sasa Masuala tena Ya Kesi Sisi hapa Ya Nini? Tunamlilia Marehemu Wewe Unaleta Habari Ya Kesi! Haya Mpigie basi Hiyo Simu................................ RIP Captain Chekingo.

Mkuu GENTAMYCINE,

hata kwenye msiba wa mzee Madiba Rais Kikwete alikumbushia jinsi mzee alivyosahau boot zake tz na ambapo alipotoka jela akaomba apelekewe, na jinsi alivyomtania Mbeki arudishe passport yake ya tz aliyokuwa akitumia enzi hizo wakati wakipigana vita ya ukombozi. Kulikuwa na umuhimu kwa Kikwete kuzungumza haya?? Jibu ni rahisi, kwamba inapotokea taarifa ya msiba wa fulani, kila mtu aliyemfahamu marehemu au kufanya nae kazi humkumbuka kwa mambo tofauti tofauti waliyofanya nae.

Shark nae kaandika tukio lake analomkumbuka marehemu sijui nae utamwambiaje.
 
Back
Top Bottom