Tanzia: Ben Kiko afariki dunia

Tanzia: Ben Kiko afariki dunia

kayogo

Member
Joined
Sep 15, 2010
Posts
75
Reaction score
42
Tanzia
Aliekuwa Mtangazaji maarufu wa radio Tanzania (TBC) mzee BEN KIKO amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo 31/10/2014 kwenye hospital ya jeshi mirambo Tabora.

benKiko.jpg

R.I.P BEN



Rais JAKAYA KIKWETE amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dokta FENELA MUKANGARA kuomboleza kifo cha aliyekuwa Mtangazaji na Mwandishi Mkongwe na Mahiri hapa nchini wa iliyokuwa Radio Tanzania - RTD ambayo kwa sasa ni TBC Taifa, BEN HAMIS KIKOROMO maarufu kama BEN KIKO.

Katika salamu zake Rais KIKWETE amesema amehuzunishwa na kusikitishwa na taarifa za kifo cha BEN KIKO ambaye ametoa mchango mkubwa wa kihabari kwa Taifa.

Wakati wa vita dhidi ya Nduli IDI AMIN wa UGANDA mwaka 1978, BEN KIKO alifanya kazi kubwa kwa Taifa kwani aliweza kuripoti matukio mbalimbali kutoka katika uwanja wenyewe wa vita, na hivyo kuliwezesha Taifa na wananchi kwa ujumla kuhabarika vilivyo na matukio yaliyokuwa yakiendelea.

BEN KIKO amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya figo baada ya kuhamishiwa hapo akitokea Hospitali ya Jeshi ya MILAMBO Mkoani TABORA.
Katika hatua nyingine Rais JAKAYA KIKWETE amesaini kitabu cha Maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa ZAMBIA, MICHAEL SATA.

CHANZO: TBC
 
May eternal peace of God be upon you marehemu Ben Kiko, ulale kwa amani.
 
weka picha basiii,wengine dot com jamaani
mie nimezaliwa wakati wa TBC hiyo RTD sikuwepo
RIP kiko
 
Mtoa mada edit hiyo heading watu watapita tu ila wakiona ni Ben kiko lazima waifungue!!
 
Jina lake halisi alikuwa no BENJAMIN KIKOTI. Umaarufu wake ulikuwa mkubwa Wakati wa vita yetu na Uganda. Huyo jamaa alikuwa anaripoti akiwa mstari wa mbele. RIP Kikoti
 
Aisee nakumbuka alivyokuwa anarupoti matukio ya Tabora....mara nyingi yalikuwa ya kusisimua na kustaajabisha....R.I.P jembe
 
Oooh... Poleni TBC. Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe!
 
Tanzia
Aliekuwa Mtangazaji maarufu wa radio Tanzania (TBC) mzee BEN KIKO amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo 31/10/2014 kwenye hospital ya jeshi mirambo Tabora.

R.I.P BEN

May his soul rest in eternal peace
 
Back
Top Bottom