TANZIA: Ajali yaua watu zaidi ya 15 baada ya Noah kugongana na lori huko Tinde

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
FB_IMG_1478464841879.jpg
FB_IMG_1478464835027.jpg
FB_IMG_1478464829229.jpg
FB_IMG_1478462825982.jpg

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba watu zaidi ya 10 wamepoteza maisha katika ajali iliyohusisha gari aina ya Noah iliyokuwa inatoka Nzega kuelekea Tinde na Lori aina ya Scania lililokuwa linatoka Kahama kuelekea Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea majira ya mbili kasorobo usiku leo Jumapili,November 06,2016 katika eneo la Nsalala kata ya Tinde mkoani Shinyanga.

"Waliopoteza maisha ni wengi sana,wapo zaidi ya 10,ajali inatisha",kimesema chanzo chetu cha habari .

Majeruhi wanakimbizwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Chanzo: Mitandao ya Kijamii

UPDATE:
- Waliofariki wamefikia 17; 15 walifariki papo hapo na wawili wamefariki wakipelekwa hospitali



=========

AFANDE RC TAARIFA YA (M) SHINYANGA KWA SAA 12 ZILIZOPITA

(1) AJALI YA GARI KUGONGANA NA KUSABABISHA VIFO SHY/TR/AR/185/16.

06/11/2017 MAJIRA KATI YA 1900 - 1930HRS KATIKA BARABARA YA NZEGA - TINDE, KATIKA KIJIJI CHA NSALALA KATA YA TINDE WILAYA NA MKOA WA SHINYANGA GARI NA T 232 BQR TOYOTA NOAH MALI YA MWINYI KHAMIS WA TINDE IKIENDESHWA NA SEIF S/O MOHAMED, 32YRS, SUKUMA NA MKAZI WA TINDE, IKITOKEA NZEGA KWENDA TINDE ILIGONGANA USO KWA USO NA SEMI TELLER T198 CBQ/T283 CBG ILIYOKUWA IKITOKEA TINDE UELEKEO WA NZEGA MALI YA ALOYCE S/O KAVISHE, MCHAGA, 46YRS MKAZI WA DSM NA AMBAYE PIA ALIKUWA DEREVA WA GARI HILO NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU 18.

KATI YAO WANAUME 7 , WANAWAKE 9 NA WATOTO 02 WAKIKE WENYE UMRI WA KATI YA MIAKA 3- 5, MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITAL YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA.

TUKIO HILI LIMEKAGULIWA NA ACP J. MULIRO KAMANDA MKOA WA SHINYANGA, SSP MWAKISAMBWE - RCO SHINYANGA NA SP ANTONY MASANZU - RTO SHY AKISAIDIWA NA DTO SHY ASP ANTONY GWANDU. MADEREVA WOTE MBARONI KWA MAHOJIANO YA TUKIO HILO NA HATUA ZA ZAIDI ZA KISHERIA.

CHANZO CHA AJALI HII KWA TAARIFA ZA AWALI NI UZEMBE WA DEREVA WA NOAH KUAMUA KUYAPITA MAGARI YALIYOKO MBELE YAKE BILA KUCHUKUA TAHADHARI NA HATIMAE KUGONGANA USO KWA USO NA LORI - SEMITELLAR. MAREHEMU WATATU WAMETAMBULIWA.

(2) MAKOSA YA USALAMA BARABARANI YAMEKAMTWA 167, YOTE YA MELIPWA, MADUHURI YALIYOKUSANYWA TSH 4,990,000/=,

3.AFYA ZA ASKARI NA WATUMISHI RAIA KWA UJUMLA NI NZURI.

RPC SHINYANGA

Habari hii imetumika kwenye Kipindi cha JamiiLeo kinachorushwa kila siku jioni katika Channel ya JamiiForums kwenye mtandao wa YouTube.

Kuona kipindi hicho angalia video ifuatayo, acha maoni yako na kisha Subscribe kwenye Channel ya JamiiForums.

 
Marehemu wote wapumzike kwa amani, Mungu pia awsaidie majeruhi wapone haraka na kuwapa faraja ndugu na jamaa ktk kipindi hiki kigumu.

Nasi tuliowazima tusipende sana hizi noah kwa safari ndefu maana ni majanga.
 
Sina hamu na naoh. Nilishawahi panda noah ya magazeti toka mtwara saa 11 kasoru na kuingia dar sa 3 na robo hivi usiku. Yaani njiani ilikuwa ni 130 kwa 150 ha ha
 
Ilikuwa inatoka nzega kwenda tinde, sehemu pekee noah zinabeba abiria ni hapo tinde tu sijui kuna mkono wa nani hapo?
 
Back
Top Bottom