Tanzania's National Electoral Commission is toothless

Mambo yanavyokwenda hivi sasa kwa habari ya uchakachuaji wa kura za ubunge na uraisi, ningetegemea angalau wawepo wazee wenye hekima wenye "moral authority" ya kuikemea serikali na tume ya uchaguzi iamke na kuacha mchezo huu wa kijinga unaoweza kuitumbukiza nchi kwenye machafuko. Au kufa Nyerere ndio mwisho wa hekima nchini?
 
Kama wazee waliobaki ndo akina Kingunge!!, unategemea nini? Inchi inazama taratibu na hakuna anayesema na hatimaye watu watastuka watakapogundua kuwa kumbe nguvu ya umma ni kubwa kuliko nguvu ya mabomu!!!!!!! siku zote ukidhurumu watu haki yao usitarajie mema ujiandae kuilipa watakapoidai na watu wakichota wanatamani uwauwe kuliko kuendelea kuona madudu yanayotokea
 
Kama nchi inaongozwa na wazee wa mipasho. Hata ukiwa na hekima utatolea wapi? Ukisema ukweli wewe ni mpinzani. Wapo watu wenye hekima zao, lkn nani wa kuwasikiliza. Wapo kina warioba, ulimwengu, butiku, mtei. Tatizo kubwa viogozi wetu hawasikilizi hoja, wanaangalia nani kasema na ana nini,
 
Mambo yanavyokwenda hivi sasa kwa habari ya uchakachuaji wa kura za ubunge na uraisi, ningetegemea angalau wawepo wazee wenye hekima wenye "moral authority" ya kuikemea serikali na tume ya uchaguzi iamke na kuacha mchezo huu wa kijinga unaoweza kuitumbukiza nchi kwenye machafuko. Au kufa Nyerere ndio mwisho wa hekima nchini?

Kwani Nyerere alikuwa anajua demokrasia?
 
Kama wazee wenyewe ndio akina MKAPA na kauli zake za majuzi pale jangwani, hatuna wazee!
Mtu anasimama kwenye kipaza sauti kumwimbia mtetezi wa mafisadi, mchana kweupe!
 
Kwani Nyerere alikuwa anajua demokrasia?
Hatuwezi kujua perception yako juu yake (huenda in some ways uliathiriwa naye), but at most he had guts to talk and rebuke for the betterment of the society!...
 
Kutokana na malalamiko juu ya chaguzi zote tangu 1995, ni muda muafaka sasa kupata muundo mpya wa tume ya Uchaguzi, Tume ya uchaguzi inatumia mabilioni ya kodi za watanzania maskini ila ndo tume hiyo hiyo imejaa tuhuma lukuki kama watu kukutwa na shahada mitaani (Segerea), kutangaza matokeo kabla ya majumuisho na kero nyingine nyingi ukiachilia mbali mchakato mzima wa uchakachuaji....

wabunge wapya (wa Upinzani) wanajukumu kubwa la kusukuma hoja hii bungeni, ni muda wa mabadiliko sasa.....
 
Tatizo ni tume yenyewe kuundwa na watendaji wa serikali ya chama tawala.., unategemea nini hapo! Kwa mtazamo wangu inatakiwa tume ambayo watendaji wake ni wawakilishi wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi. Hapo hakutakuwa na mtu wa kupenyeza ma#^~%"" yake kwenye uchaguzi.

Hii tume haifai jamani, ni ya CCM ... tutaumia mpaka Masihi arudi kama hatutaikataa.
 
Back
Top Bottom