Tanzania's National Electoral Commission is toothless

Tanzania's National Electoral Commission is toothless

Hivi kweli ndugu zangu kwenye nchi ambayo haki ya mtu bado ni ndoto, tunategemea nini kwa mwenyeketi wa tume ya uchaguzi ambaye anateuliwa na rais ambaye huyo rais naye anakuja kuwa mgombea na huyu mteule wake ndo mwenye maamuzi? Lazima liwepo shinikizo la kuunda tume huru inayojumusha wajumbe toka vyama vyote vikuu (kama si vyote) ili haki iwe inatendeka. Vinginevyo kura zetu zitaendelea kutokuwa na maana yoyote. Na hii itaendelea kuwafanya watu wengine wasiende kupiga kura kabisa.
 
jana jioni nilikuwa nasikiliza BBC ambapo Jenarali Ulimwengu alikuwa akihojiwa kuhusu namna tume ya uchaguzi ilivyosimamia na suala la kuchelewesha matokeo. alisema kuwa kuchelewesha matokeo kwa tume kunasababisha hofu ya matokeo kupikwa(kuchakachuliwa) na hiyo ni kasoro kubwa sana. alisema anawahaheshi sana wazee( wakubwa wa tume) lakini ni wakati sasa wakastaafu na kuwaachia vijana na kuwa tume hiyo kwa sasa haifai hata kidogo. labda alichosahau kidogo ni kuwa hata aje nani kama tume bado itaendelea kulinda matakwa ya/kuwa chini ya ccm ni kazi bure, lazima tume iwe huru kabisa na uhuru ambao utalindwa na katiba.
 
Ukweli ni kwamba wakiingia mjengoni wabunge waanze nalo la kuunda tume huru ya uchaguzi kwani huu wizi wa kupora kura za wengine na kujiwekea unatia aibu na umekidhiri
 
I always like Jenerali, najua ulishakua mheshimiwa wakakufanyia fitna, wengine wakahoji hata uraia wako,tunashukuru kwa kua hujarudi nyuma na hawajaweza kukufunga mdomo unasema iliyo kweli, mungu akubariki mzee.
 
Ukweli ni kwamba wakiingia mjengoni wabunge waanze nalo la kuunda tume huru ya uchaguzi kwani huu wizi wa kupora kura za wengine na kujiwekea unatia aibu na umekidhiri

Hapo kwenye kuunda Tume huru ndio CCM wasipopataka maana wanajua once tume ikiwa huru watashindwa kuchakachua
 
Yaani I wish Jeneral ndio angekuwa mwenyekitu wa NEC yaani ingekuw apowa sana huyu Mzee haogopi mtu ni mtu muwazi na mweli na daima huwa anasimamia haki. Bravo Jenerali :A S crown-1:
 
Huyu Ulimwengu ni nani mpaka aseme Tume ya Uchaguzi haifai. Anaweza kuchakachuliwa uraia wake sasa hivi. Aende huko RWANDA na kumwambia KAGAME kuwa Tume ya huko haifai.

Siyo kila kitu anachosema Ulimwengu ni sahihi. Mimi nashangaa namna baadhi ya taasisi zinavyompapatikia Ulimwengu. Who is this Ulimwengu?
 
Mimi nadhani kuunda tume huru inawezekana kabisa hata kama CCM hawataki. kinachitakiwa ni kwa vichwa makini vilivyoingia mjengoni mwaka huu kuanzisha move ya kuwa na tume huru na pia kufanya marekebisho ya katiba. Utaratibu uwekwe ili mwenyekiti na wakurugenzi wa tume wasichaguliwe na raisi bali watokane na wawekwe kwa mujibu wa sheria. Hiyo ni kazi ya kwanza kwa waheshimiwa wetu hasa kutoka upinzani maana CCM hawataki hata kusikia. "Hakuna kulala mpaka kieleweke".
:A S angry:
 
Halafu kuna mtu mwingine ambaye hunishangaza pia huyu si mwingine bali ni ANANILEA NKYA. Yeye anaongoza TAMWA, Chama cha Waandishi wa habari Wanawake, lakini utamwona anuza sura yake kwenye TV kushutumu kila kitu katikaTanzania hii kwa kuwa tu TAMWA inafadhiliwa na foreign countries. Yaani anasahau jukumu la msingi la TAMWA na kuanza kujiingiza kwenye siasa. Ajabu yeye kama ULimwengu hawagombei ubunge au udiwani. Kazi yao kubwabwaja tu kwenye vyombo vya habari ili waonekanane wana akili sana. Watu hawa tumewachoka.
 
Ni faraja kubwa sana kwamba watu kama Generali Umlimwengu bado wapo Tanzania. Ni mtu aliye tayari kutetea kile anacho amini kuwa ni sahihi hata walitaka kumtisha na mambo ya uraia. Ana uzalendo na nchi hii kuliko huyo mtu aliye fanya uharamia wa kumnyima uraia.
 
Zanzibar, Seif ameomba tume irekebishwe, sijui kwa nini Bara hili halisemwi?
 
Jamani si kwamba tu tunahitaji muundo mpya wa Tume huru, bali hata katika hiyo tume tunahitaji vijana kama tulivyo pata wengi katika ubunge. Akina mzee Lewis Makame muda wao umepita. Ni jamii ya ya akina Kivuitu hao! Wanalinda maslahi ya waliowaweka hapo!
Fikiria tu mtu kama Halima Mdee ni mkurugenzi wa tume huru. Masaa kadhaa baada ya uchaguzi mambo yote yatakuwa hadharani na kwa ufanisi bila kuchakachua!!
 
Mimi nadhani kuunda tume huru inawezekana kabisa hata kama CCM hawataki. kinachitakiwa ni kwa vichwa makini vilivyoingia mjengoni mwaka huu kuanzisha move ya kuwa na tume huru na pia kufanya marekebisho ya katiba. Utaratibu uwekwe ili mwenyekiti na wakurugenzi wa tume wasichaguliwe na raisi bali watokane na wawekwe kwa mujibu wa sheria. Hiyo ni kazi ya kwanza kwa waheshimiwa wetu hasa kutoka upinzani maana CCM hawataki hata kusikia. "Hakuna kulala mpaka kieleweke".
:A S angry:

Mi nadhani ili tume iwe huru ni iwe chini ya bunge!! Bunge iunde sheria mupya ya namna ya kuiteua tume huru ikiwa chini yao!!! Lakini si kuteuliwa raisi, lazima watalinda mabosi wao kama wanavyofanya sasa!!!!!!!!!!
 
Wadau, tumshukuru Mungu uchaguzi umeisha kwa 'amani' ingawa hatua ya NEC kushindwa kutoa matokeo kwa muda unaotakiwa ni aibu na dosari kubwa. Wananchi sasa wamefikia hatua ya kuona kuwa chaguo lao haliwezi kuthibitishwa na Tume hadi walazimishe. Sote tu mashahidi kuwa pale ambapo CCM inapokuwa imeshinda Ubunge, Msimamizi wa Uchaguzi (kw aniaba ya NEC) anatangaza matokeo haraka, lakini pale ambapo wapinzani wa CCM wameshinda inachukua muda sana kuthibitisha matokeo hadi amani inakuwa inatishiwa.

Arusha, maduka yote yalifungwa mjini kwa sababu Msimamizi wa Uchaguzi alichelewa kutangaza matokeo hali iliyofanya mji uwe tete na maduka yote mjini kufungwa kwa ajili ya umma uliokusanyika Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi tangu aalfajiri! Umma unajua mshindi mapema maana matokeo yote ya Uunge na Udiwani hubandikwa kwenye kuta za vituo vya kupigia kura. Sehemu zote ambazo Wapinzani wameshinda, matokeo yameshinikizwa na Umma na kushuhudia uvunjifu wa amani (kama ilivyodaiwa na CCM wakati wa Kampeni, je, kuna kitu gani nyuma yake kama sio NEC na CCM/ Serikali kuwa kinyume na maamuzi ya umma? Uliona wapi na lini pale ambapo wananchi waliridhika na matokeo kukawa na vurugu? Zanzibar mwaka huu kulikuwa na fujo gani? Kwa nini hali ya fujo itokee Bara ambapo kuna vyama vikuu zaidi ya viwili vinanvyopingana? NEC, CCM na Dola wanasababisha hali hii, NDIYO!

Idadi ya Wapiga kura waliosajiliwa kwenye daftari ni tata na kuna uwezekano mkubwa kuwa na mahoka wengi sana na watu waliojiandikisha zaidi ya mara moja. Tuchunguze trend ya Wapiga kura tangu kuanzishwa kwa daftri, kwa nini idadi ya wanaojitokeza inakuwa ndogo? Hivi ni kweli wananchi hawajahamasika kupiga kura?

Mwaka 2005 (wakati daftari lilipotumika kwa mara ya kwanza) idadi ya waliojitokeza ilikuwa kubwa kulinganisha na chaguzi zilizofuatia, hii inawezekana kabisa kuwa idadai iliandaliwa maalumu kwa ajili ya matokea ya kishindo kwa CCM!

Tujiulize, kwa nini wakati idadi ya wanaojiandikisha inaongezeka kila daftri linapofunguliwa inaongezeka sana lakini ukifika uchaguzi idadi ya wapiga kura inapungua kuliko ya awamu ya uchaguzi ulopita? Hapo kuna jambo!

SHUKRANI KWA POLISI
Kama mwaka huu Polisi wetu wangekuwa wanongozwa na IGP Mstaafu Mahita, naamini kabisa Bara ingekumbwa na umwagaji mkubwa wa damu. Shukrani za pekee kwa IGP mwema ambaye amejitahidi kuachana na fikra za ukandamizaji.

LAkini pia inawezekana hata jeshi letu la Polisi limechoshwa na uvurugaji wa matokeo ya uchaguzi na kutumiwa na Wanasiasa (hasa CCM) kwa gharama ya maisha ya umma na kwa kupakwa matope kwa kutumia maguvu bila sbabu za msingi huku wao wakishutumiwa kwa rushwa wakati Wanasiasa wakishiriki kwenye rushwa kubwa zaidi.
 
Halafu kuna mtu mwingine ambaye hunishangaza pia huyu si mwingine bali ni ANANILEA NKYA. Yeye anaongoza TAMWA, Chama cha Waandishi wa habari Wanawake, lakini utamwona anuza sura yake kwenye TV kushutumu kila kitu katikaTanzania hii kwa kuwa tu TAMWA inafadhiliwa na foreign countries. Yaani anasahau jukumu la msingi la TAMWA na kuanza kujiingiza kwenye siasa. Ajabu yeye kama ULimwengu hawagombei ubunge au udiwani. Kazi yao kubwabwaja tu kwenye vyombo vya habari ili waonekanane wana akili sana. Watu hawa tumewachoka.

What a disgust and sickening article.Honestly what you have written proves how naive and illiterate you are.Ulimwengu and Nkya are entitled to give out their own opnions like any other citizen.What did you expect them to do?.You sounded so ignorant, i wonder whether you do understand the roles of TAMWA.If the media doesnt speak who else would do?. What you wrote was really annoying,disgusting and above else you sounded quite naive.I wonder whether you have even attended secondary school education.You sounded really naive!!!!
 
Huyu Ulimwengu ni nani mpaka aseme Tume ya Uchaguzi haifai. Anaweza kuchakachuliwa uraia wake sasa hivi. Aende huko RWANDA na kumwambia KAGAME kuwa Tume ya huko haifai.

Siyo kila kitu anachosema Ulimwengu ni sahihi. Mimi nashangaa namna baadhi ya taasisi zinavyompapatikia Ulimwengu. Who is this Ulimwengu?

Hebu acha upuuzi.Stop that foolishnes.You better do a constructive and productive thing than writing nonsenses.Hebu uwe mkweli Is the electoral commission doing it 's job properly?.How many incidents have been spotted za wizi wa kura tena watu hao hao walioteuliwa na tume been involved in the rubbishes.Nakuuliza wewe has the election been fair? Why have they been delaying to declare the winners?What was the secret behind?Even the observers have noted that.Ila kasoro wewe mwenyewe na tume yako ambayo unasema ni fair.The bottom line is bila kuwa na tume huru CCM will rig all the coming elections.Lakini ipo siku tu!!!!. Mungu anaona yote yanayotendeka.
 
Napendekeza bunge la 10 ajenda yao kuu iwe MAdiliko ya KATIBA itakayo saidia kuondoa mambo mengi yanayo dumisha demokrasia nchini. ikiwa ni pamoja na kuwapo kwa tume huru ya uchaguzi.
 
Napendekeza bunge la 10 ajenda yao kuu iwe MAdiliko ya KATIBA itakayo saidia kuondoa mambo mengi yanayo dumisha demokrasia nchini. ikiwa ni pamoja na kuwapo kwa tume huru ya uchaguzi.

Pia wahisani/Donors wasiipe serikali yetu hata senti tano wa msaada mpaka pale katiba itakapobomolewa na kujengwa upya
 
Back
Top Bottom