Tanzania's Lotus disqualified from Big Brother

Habari zenu wanajanvi na wanaofuatilia kinachoendelea ndani ya Big Brother House.

Mmoja wa wawakilishi wa BBA toka nyumbani kwetu Tanzania, ametakiwa kupaki mizigo yake,

Nakuondoka baada ya kubishana na Luclay toka South Africa, na kupelekea Lotus kushindwa kujizuia na kumpiga vibao Luclay.

Kwa mujibu na sheria za BBA unapopigana na mwenzio huna nafasi tena ya kuendelea na

mashindano.

Ni hayo tu yaliyotokea. Thanks.
 
BIGBROTHER is Bighouse wc Gorgerous n Boys Riding Ovals(maws) Tremendous Higher wc Exposure to Republic. MAMBO HADHARANI.
 
Kibali wamempa WASHENZI wooote wanaokaa na kupiga CHABO kwenye TV.

Halafu leo wanakuja na kuanza kulaani yanatokea huko ndani, kwani ulifikiri ni TV ya Dini?

Mmeyataka wenyewe na kuangalia TV za namna hii. Mvumilie tu.

Nawapa HONGERA hao vijana kwa kuonyesha Dunia ya kweli ya sasa ilivyo na si UNAFIKI.

Kama watu wasingeangalia na hata kuja kuweka vilawama vyao hapa au pongezi, BBA ingelikufa.

Hamna haja ya viboko wala nini. Wote wanao-NGONOA huko, ndiyo wanaofaa kwenye BBA na si hawa wanakwenda na kujifanya watu wa dini. Dunia sasa inataka SKENDO na si watu wenye nidhamu. Hao kawatafute kwenye majumba ya dini, ingawa hata huko nako kumeshaingiliwa.

Mie napenda Mabinti wanaoonyesha kila kitu kwenye TV. Hao ndiyo wanafaa maana macho yanafaidi huku ukisubiri Jumapili na Ijumaa zifike ili tukafute/kutubu dhambi zetu, AMEN.

(Akili za Mbayuwayu utumie unaposoma maneno yangu...........)


mkuu ni kweli

makampuni makubwa yanawekeza hela nyingi sana kwenye hiyo michezo. Na ili kuvutia watazamaji wengi ni muhimu washiriki wafanye waandaaji wanavyotaka. Kwa hiyo hizo ngono, ulevi, na anasa ndo vitu watu wanataka waone..Ili hela za investors zirudi...

Na bado, tutasikia mengi: Ni sawa sawa na movies za siku hizi, haiwezi kuuza sana kama haina mambo ya sex; huo ndo ukweli..
 
mh atakuwa hawezi kuvumilia hasira, either alie au apige ndo zinapungua. masikini pole yake
 
ana lolote huyo,atoke tu kwanza alikuwa anabore! Ujuaji mwingi!
 
hapo kwenye red sisi tuondoe

katika maswala haya hakuna utaifa
sijui wamepelekwa na nani? wazara ya michezo na utamaduni ina habari?
Mkuu bora useme wewe, manake mi nashindwa kuelewa inakuwakuwaje tunalazimishwa kuwa tunawakilishwa katika huu upumbavu wa BBA. Hao wajinga wanajiwakilisha wenyewe tu period.
 
yani BBA Tz tukipeleka wanawake tu shida..halafu hata hawajifunzi ni kubweteka tu na kufanya mambo ya ajabu!
 
Sa kama ishu ni kuishi maisha halisi,,iwaje wakipigana wanafukuzwa??

Kwani kwenye maisha halisi watu hawagombani??

Kumbe sio reality show wala nini.


Ni bora wafanye malavidavi kuliko kupigana..(kupigana mjengoni ni dhambi kubwa sana) lol..
 
Wacha atoke tu mana alikuwa anatutia aibu tu afu alitaka awepekee tu kwenye nyumba ya kaka mkubwa na mwenzie atoke..Atakuwa amesaidia kupunguza washiriki kabla ya muda uliopangwa..hata huyo Luclay nae anaweza kutoka mana ni radical kweli
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom