Tanzania's Foreign Policy

ewe membe,kwanini unakubali kutumwa na JK kutetea ufisadi wa BOT?
Ewe membe ulikuwa wapi kuzungumza zamani haya mathalani yameanza zaidi ya mwaka,
ewe membe mbona hautaki kusoma alama za nyakati?
ole wana wa watazania mafisadi,msidhani watanzania ni mbumbumbu
 
hatunyamazishwi ng'o! nasikia warioba alitoa ripoti ya hao mafisadi mwaka 1996 lakini mkakaa kimya sasa tumechoka, kila siku idadi ya mafisadi inaongezeka eg mkapa mwaka 96 hakuwepo kwenye list laliki sasa hivi yupo inamaana miaka ijayo list itakuwa na watu 111 je tutafika kwa hali hiyo? kwanini tukae kimya? Membe angalia kwenye list haumo ila ukiwatetea tutakuona mtu wa ajabu. Hakuna haja ya uchunguzi fisadi ni fisadi tu. Ona sasa mpaka Kapuya anamiliki mgodi wake mwenyewe huku watu hata ardhi ya kulima wananyang'anywa eti kupisha uwekezaji ambao wanafaidika wao, loh aibu gani hii?
 
Well come Haki sawa.

Style yako ya kuingia humu nimeipenda. Lete maneno
 
Membe hawezi kuwajibu kwa nyodo watu ambao watusaidia 40% katika bajeti yetu, Yeye anafikiri wao wanafurahia uchafu wanaofanya na mawaziri wenzie?
Tushawachoka sasa akina Membe na wenzie.
 
Kwa sababu huyu mkuu rekodi yake kiuongozi ni safi, angetulia tu na kukaa kimya, hao mabalozi wakubwa wa dunia huwa hawahitaji kibali cha local government kuuliza yanayojiri,

Huyu hakuona waliyomfanyia Noriega na Saddam nini?
 

Hahaha sijui kama Mkandara unayakumbuka maandishi haya. They exist mzee. Keep it swinging mzee wangu
 
Jinsi habari hii ilivyo ripitiwa na HabariLEO:

Source link: HabariLEO.

SteveD.
 

Haya jamani, wengine wanatembea nchi nzima wakisema WAPINZANI NI WAONGO, huku Zitto kafungiwa kwa kusema uongo, sasa huyu Membe katumwa na JK anasema wanachunguza!!!!!!!!!!!!!!!!, NASIKIA KUZUNGUZUNGU
 
“Sisi Balozi wetu hawezi hata siku moja kufanya hivyo… balozi wetu wa nchi za nje akifanya hivyo watamrudisha mara moja kwa sababu siyo sahihi kutumia majukwaa kwa balozi,” alisema Membe.
Balozi wetu huko majuu, atasema nini wakati huko watu hufuata sheria? Wewe umesikia leo mkimbiaji maarufu Marion Jones, amefikishwa mahakamani kwa makosa aliyotuhumiwa toka mwaka 2000, leo ni 2007 ametinga kwenye mkono wa sheria na maekubali kuwa na makosa, pamoja na umaarufu wake wote, sasa balozi wetu huko atawasema kitu gani?

Hivi ni kitu gani anafikiri ana-accomplish kwa kuwadanganya hao mabalozi? Kwani wao wajinga hawaijui bongo? Hilo gazeti limeandikwa na nani? Hiyo kampeni wanayoitumia kupoteza hela zao kama sio zetu walipa kodi, kwa nini wasizitumie kuanzisha kesi mahakamani ili mzizi wa fitina ukatwe? Kesi ikienda mahakamani Membe hatakuwa na shida ya kumuelezea balozi yoyote, wala mawaziri kwenda mikoani, kwa nini wanapoteza muda wa watu bure na hadithi za Abunuwasi, wakati wananchi tunao mkataba wa Buzwagi tayari?

Je huu mkataba usinge-leak ingekuwaje, tungeyasikia haya? Wapunguze hadithi sasa ni wakati wa kazi na matendo, waache hadithi!
 
FROM WHAT HAS BECOME THE NORM OF RESPONSE FROM THE GOVERNMENT RECENTLY, I'M INCLINED TO SAY COLLECTIVE STUPITIDY IS AT WORK, AND THAT'S PRECISELY WHAT THEY ARE UNVEILING BY TRYING TO BE CRITICAL ABOUT BUZWAGI CRITICS!! FOR WE KNOW, THE WISDOM OF CROWDS AND THE ANTICIPATIVE COLLECTIVE INTELLIGENCE IS OUT OF THE DOOR ON THEIR PART!!

SteveD.
 
1. Hivi wewe membe si ndiye ulikiuka maadili ya UWT na kufichua uovu wa Bosi wako Kitine, kwani huko UWT hakuna taratibu za kutiana adabu mpaka ukamuumbua bosi wako?.........hivi unajua heshima uliyojijengea kwa lile jambo?

2. sawa Geneva Convetion inawabana, however FACT inabaki kuwa FACT irregardles of whichever convetion...........hata Convention ikitoka mwezini haiwezi kuondoa FACTS walizosema, atleast wameweza kuuliza kile ambacho KODI za wananchi wao zinatumika/zinatarajia kutumika directly or indirectly.........Trust me Membe hawa wote waliotoa matamko wanakuwa supported na nchi zao.........usifikiri wamekurupuka tu.

3.Membe wewe ni mwanadiplomasia mahiri na.............i mean heshima mbele, twende mbele turudi nyuma vile vile, hivi hawa mabalozi waliongelea hayo masuala wakiwa wapiiii?...............who were the audience.......na mada ilikuwa nini?.........
 
Mods jamani tunaomba mu merge threads zinazofanana fanana

kama mko sharo kuhamisha threads kwa nini mko slow kumerge threads mkiombwa?
 
TANZANIA HAS GOT 2 FOREIGN POLICIES......!
\ (TRADITIONAL FOREIGN POLICY president's circular no 2 of 1964 & NEW FOREIGN POLICY 2001)
 


Mkuu Kulikoni,

With all due respect hoja yako ya kwanza na hii I 'm sorry that I will have to disagree with you completely.

Katika hoja zako mbili unagusia economic diplomacy!, ni ipi hio.

Tanzania tokea ipate uhuru hadi leo inategemea pesa ya wafadhili kuendesha shughuli zake na hata bajeti hisimamiwa na wafadhili hao.

Nafikiri umesoma kitu kinaitwa interenational relations theory, ni conceptual model gani imebuniwa na wizara au mawaziri tokea uhuru kuiweka Tanzania katika duru la nchi zilizoendelea au basi kupiga hatua fulani?

Pia umetaja masuala ya watalii lakini hawa watalii huletwa Tanzania na mawakala ambao wapo nje kwa mfano UK ambao huwalipisha fedha nyingi hadi kufikia paundi 2000 kwa wiki mbili tu wakiwa Tanzania.

Mimi naona hujaeleza kwa ufasaha hasa foreign policy ya Tanzania imesimama vipi, vinginevyo naona unakuwa kama unatoa blanket statements tu.
 
my meseji to MOFA.......! wekeni mtandaoni TZ NEW FOREIGN POLICY(2001)
ili watu/wananchi wajue sera ya nje ya nchi yao....! hope nimeeleweka>>>>!
 
mtandaoni utakuta sera za mifugo, maji, viwanda n.k lakini sera ya mambo ya nje haimo...!
 
my meseji to MOFA.......! wekeni mtandaoni TZ NEW FOREIGN POLICY(2001)
ili watu/wananchi wajue sera ya nje ya nchi yao....! hope nimeeleweka>>>>!

Mkuu,

Lakini hii si naona itakuwa updated au ..!

Maana leo ni 2008
 
Hivi kuna mtu anajua kama ule ubalozi ulishafunguliwa Brazil?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…