kmp
Member
- Jun 18, 2009
- 39
- 0
Habari nilizozipata zinasema Prof. Mwaikusa Mwalimu wa Sheria na Mwanasheria aliyebobea wa Chuo Kikuu cha DSM amefariki dunia baada ya kuvamiwa na watu wanaosemekana kuwa ni majambazi alipokuwa akirejea nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo.
Prof. Mwaikusa pia alikuwa rafiki wa mahakama ambaye alitetea vizuri hoja alizowakilisha kuhusu mgombea binafsi. mwenye data zaidi atujuze. rip prof.mwaikusa.
---
Wakili mwandamizi wa utetezi nchini Tanzania wa mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa inayoshughulikia kesi za washukiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda amepigwa risasi na kufa nje ya nyumba yake mjini Dar es Salaam.
Profesa Jwani Mwaikusa, ambaye pia alikuwa mkufunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, aliuawa wakati akitaka kuingia nyumbani kwake nje kidogo ya mji huo.
Polisi wanasema mpwa wake pamoja na jirani yake waliuawa pia.
Imearifiwa kuwa wahalifu hao walilipekua gari la marehemu na kuondoka na mkoba wake wa kazi pamoja na hati kadhaa.
Bw Mwaikusa alikuwa wakili mtetezi wa mfanyabiashara wa Rwanda Yussuf Munyakazi anayekabiliwa na tuhuma za kuhusika katika mauaji ya kimbari kwenye mahakama ya kimataifa mjini Arusha.
Wakati akimtetea, alifanikiwa kuzuia Munyakazi asirejeshwe nchini Rwanda, kwa hoja kuwa asingeweza kutendewa haki na mahakama za huko.
Gazeti la Citizen nchini Tanzania limesema kumekuwepo na ongezeko la matukio ya uhalifu mjini Dar es Salaam katika siku za hivi karibuni.
Watu watano wameuawa kwa risasi na wahalifu wenye silaha katika kipindi cha miezi mwili iliyopita.
---
Viongozi na Wanasiasa wengine waliowahi kupigwa riasasi
- Utata kifo cha hayati Abeid Karume
- DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali
- Simulizi: Kisa na Mkasa wa Mauaji ya Jenerali Imran Kombe (Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa-TISS)
- TANZIA - John Mwankenja auawa kwa risasi
- Dr. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake
- TANZIA - Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!
- Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA
- Maandamano ya CHADEMA: Aqulina Akwilini Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza NIT apigwa risasi na kufariki; Polisi wakiri kuhusika
- Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana
- Askari polisi aliyepigwa risasi na majambazi Tanga afariki
Last edited by a moderator: