Tanzanian diaspora mnatuangusha


Kama mfano wako ni huo basi huyo unayemuita mchaga kama akihama kwao na akauza shamba lake pia hawezi kurudi baada ya miaka kadhaa na kudai arudishiwe lile shamba kwa maana ni la ke tangu vizazi, kama akirirudi na akiwa bado hajauza shamba lake basi ruksa kulitumia kama ameliuza basi imekula kwake na inabidi aanze moja kutafuta shamba lingine!

 
Yawezekana lile linalosemwa la kazi yao kubwa ni kubeba mabox lina ukweli hivyo wanapata pesa ya kula tu huwawezi kutuma bongo.
 

Sio arudi arudishiwe shamba bali arudi kama anarudi nyumbani bila kuitwa mpogolo bali mchagga kwani mtanzania aliyeondoka anarudi kudai alichouza? Anarudi nyumbani kwao kama mtanzania sio mmarekani au mjerumani awe na haki zote kama mtanzania aliyeondoka. Huyo mchagga akirudi atambulike kama mchagga aliyerudi kwao bila masharti yeyote iwapo aliuza shamba hawezi lidai maana si lake lakini utambulisho unabaki palepale kuwa ni mchagga na si mpogolo na ana haki zote kama aliowaacha za kuwa mchagga
 

wanigeria waliopo UK tu wanakadiriwa kuwa zaidi ya million 2
 
Yawezekana lile linalosemwa la kazi yao kubwa ni kubeba mabox lina ukweli hivyo wanapata pesa ya kula tu huwawezi kutuma bongo.

Watanzania wa ajabu kweli mtu akifanya kazi yake bila kuiba anadharauliwa lakini wezi watawala wanashangiliwa unataka kusema Tanzania kila mmoja kazi yake ni boss? Unachekesha ni heri kubeba box ulaya kuliko kufanya kazi ya kawaida Tanzania labda uwe na access na rushwa ndo maana Tanzania kila mmoja anataka kuwa mwanasiasa, mkurugenzi wa kampuni mfanyakazi TRA, Bandari, Benki Kuu, Hazina au mkurugenzi wa wilaya au mkoa ili awe fisadi maana kazi Tanzania unajua kabisa wapi penye kuiba kirahisi utoke kwa wenzetu si lazima uibe maana daktari tu wa kawaida na si bingwa analipwa dollar 150,000 kodi hapo dollar 20,000 anapeleka nyumbani 130,000 milioni 220 hata kwa maisha ya Marekani ni pesa nyingi sana huyo mmbeba box analipwa 32,000 kwa mwaka takribani milioni 50 yuko safi kuliko afisa wa serikali hapa Tanzania anayelipwa milioni 15 kwa mwaka labda na za kuiba na kuiba ni dhambi si uhodari na hizo milioni 15 kwa mwaka bado kulipia wanafunzi gharama hata chekechea ya maana milioni kwa mwaka fanya kazi yeyote ili mradi huibi na hujalazimishwa

Mbeba box akiona kazi moja haitoshi anapiga mbili Tanzania hakuna pa kupiga mbili bali kwenda kuiba, rushwa na wanawake kuwa mahawala wa mabosi au kujiuza ndo madeal na watu wanajisifu kuanzia ikulu deal mpaka kwa katibu kata
 

Huyo hata hakuelewi uandikacho mbishi mbishiii ,umemuelimisha inatosha achana naee
 

TZ diaspora mmo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…