Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

Kanumba ni msanii mkubwa hivyo lazima taifa lifike wakati kuenzi mazishi ya watu mbalimbali wenye vipaji ata ukiwa mchekeshaji nawe pia ni sehemu ya ukuaji wa taifa letu.....RIP kanumba

tofautisha wasanii waliotumia usanii wao kwa manufaa ya taifa zima na wanaotumia usanii wao kwa manufaa yao binafsi. Wengine wanatakiwa waenziwe na taifa na wengine na wasanii wenzao na mashabiki wao. Huwezi kunishawishi mimi leo uumie kodi yangu kusafirisha msiba wa kanumba wakati kuna wagonjwa kibao leo wamekosa dawa. Sikuwa shabiki wake hata muvi zake nilikuwa naziona accidentaly kwenye basi wakati nasafiri. Tofautisha wasanii kama l.dube,blenda fasie, bob, waliotumia usanii wao kwa manufaa ya taifa wakati wa kupigania uhuru,this is nationally kwani walipopata uhuru watu wote walinufaika. Mambo ya kanumba ni yake na mashabiki wake. Kufahamika nigeria hainiletei faida yoyote mie nisie shabiki wa huu upuuzi wanaoufanya. Huwa wanashindwa hata kufanya consultation ya sehemu zinazohusu profesion fulan!
 
Kama baba alimtelekeza Kanumba alikuwa na Haki kusema hisia zake,wewe unajua athari ambazo mtoto anaishi nazo kwa kutelekezwa na Baba yake? Si jambo jepesi,huyo baba yake Kanumba alitakiwa amwombe radhi mwanae kwa kumtelekeza kama ni mwenye Akili Timamu na Mwenye Hofu ya Mungu!!

Neno la Mungu linatutaka Watoto tuwaheshimu wazazi wetu ili tupate HERI na MIAKA mingi lakini ni Biblia hiyo hiyo inawaonya Wazazi KUTOKUWACHOKOZA watoto wao!!

Baba anapomtelekeza Mtoto,halafu mtoto akikuwa akisema kama ulimtelekeza unasemaje kwamba anakuvunjia Heshima? Utakuwa Mwehu na Tabia ya Wanaume Waovu ambao Ukimbia kulea watoto halafu akikuwa anajifanya kuwa karibu naye kuliko hata mama ambaye alimlea mwana kwa dhiki nyingi!!
Imeandikwa "Laana Isiyo na Sababu Haimpigi mtu",Kuhusu watu wanaotelekeza watoto wao Mungu anasema hivi "Yeye ni MBAYA asiyewahudumia Watu wa Nyumbani mwake kuliko asiye Amini"
Kwa maana hiyo basi,kama Kanumba amefariki ni kwa sababu zingine lakini siyo radhi ya huyo Mzee Hopeless and Irresponsible,kwa Mungu huyo ni MBAYA na atatoa Hesabu kwa nn alitelekeza Mwana!!

Kizee kama hicho hapo sasa kitakuwa kinawaza Mirathi tu maana hakina Uchungu,U cant Lose what u never had!!

so touching...but Mungu ameagiza KUSAMEHE ili nasi tuweze samehewa maana sisi tunamkosea Mungu mara nyingi kuliko watu wanavyotukosea still anatusamehe, ili kusamehe inahitaji upendo maana imeandikwa- upendo husitiri wingi wa dhambi hivyo kwanza inabidi umpende huyo unaetaka kumsamehe ndipo utakapoweza kusamehe. Si jambo jepesi ni gumu lakini ndivyo inavyopasa maana hatakama Mzazi alikukana/ kutelekeza bado Mungu alikutunza kwa jinsi alivyokutunza hata hapo unapofanikiwa ni yeye akufanikishae. Ni kweli wazazi wanajukumu la kulea na kutunza watoto but sometimes things are mixed up sasa hiyo kesi mwachie mzazi na Mungu wake, mtoto ASAMEHE tu it will do you so much good than holding grudges and hard feelings over your own parent.
 
Hata sijui niamini yupi Kanumba alisema hanywi, Lulu akasema hana boyfriend na alikuwa single, Polisi wanasema Kanumba kanywa pombe kali tena "uchunguzi" unaonyesha ni kinywaji gani.....kipi ni kipi??

nadhan report ya awal ya polis imetegemea mahojiano ya ndugu na mtuhumiwa
 
Msimuhukumu huyu mtoto; kinachotakiwa hapa ni autopsy report kuhusu sababu ya kifo cha Kanumba. Ninadhani kuwa tuna utaratibu wa kufanya post mortem examination kwenye mwili wa marehemu iwapo kifo chake kinahusisha na uvunjaji sheria.

Miezi michache iliyopita tuliona PDiddy akianguka ghafla na kufariki bila kuguswa na mtu yeyote, inawezekana kulikuwa na sababu nyingine kama vile stroke iliyotokea kwa Merehemu Kanumb wakati Lulu anamsukuma, ambayo bado ingechukua uhai wa marehemu hata bila kusukumwa na Lulu kama ambavyo ilivyotokea kwa Marehemu PDiddy. Kujua chanzo cha kifo ni jambo la muhimu kwanza kabla ya kujadili mazingira ya kifo hicho.

Ni vizuri pia tukumbuke kuwa mabadiliko ya lifestyles za mastaa wetu yanaendanana na mabadiliko ya kiafya kama vile kupanda au kupungua kwa sugar levels katika damu, kujengeka kwa plagues za cholesterol kwenye mishpa ya damu na na kupanda kwa blood pressure mwilini. Ni vizuri sana masataa wetu wajenge utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara kuhakikisha kuwa hawana matatizo ya kiafya yaliyojificha miilini mwao yanayoweza kuchukuwa uhai wao kwa muda mfupi tu.
Muongo mkubwa wewe mbona pdiddy yupo hai usitumie hili jukwaa kutuletea habari za uongo
 
Yametokea na mengineyo yanayojili ni maongezi yaweza kuwa ya kweli ama si kweli!!ila sometimes naamini familia bora ni matunda ya baraka njema na maombi na kuomba toba nayo ni tiba kwa yalea mabayo Mungu akushirikisha.Kanumba aka THE GREAT ni mtoto wa Mzee KANUMBA [Baba Msukuma] na Debora [MHAYA],ambao wamemzaa kanumba nje ya mahusianao kamilifu ya NDOA.

Malezi ya Kanumba kwa upande wa Baba yake yani kwa mama wa Kambo yalikuwa niyale malezi zilizo familia nyingi za kiaafrika na hasa za kitanzania kuwa mama wa kambo kidogo anakuwa na matendo yasiyo furahisha katika malezi mema ya watoto wasio kuwa damu yao.

Kanumba kasoma shule ya msingi Bugoyi yani Bugoyi Primary School [Shule aliyosoma Lady Jay D na pia ndio shule aliyosoma Johari].Shule ya Sekondari O'level kasoma Mwadui Primary School [Kishapu-Shinyanga] na hatimae kuhamia Dar es Salaam kwa elimu ya juu pia yani Advance Level.

Binafsi namjua kama kijana mpole ambae ujana wa primary school na sekondary school hakuwa karibu na watoto wa kike zaidi mwana mwadilifu zingatia watoto ambao wanapitia maisha ya malezi ya misukosuko ya mama wa Kambo na hasa pale Baba anapokuwa amebanwa na Mrs na hivyo kusahau kumtimizia mwanawe wa damu mapenzi asilimia mia bali kumtimizia kwa mujibu wa ushawishi wa kiwango cha mahitaji ya mama wa Kambo.

Ila sometimes Life Is Full Of Surprises ukweli Mungu ana mitihani,na mitihani hiyo inaitaji busara sana hasa kwa sisi waje wake.Mzee kwa uhalisia kibidamu tunamuhukumu kwa kutotimiza wajibu wake,lakini hatujui sometimes vitu vinatokea for a reason.Na uenda Mungu alipanga hivyo Kanumba kupitia maisha ya misukosuko lakini,waliopaswa kumlea Kanumba kama mtoto aliyestahiki malezi ya utoto pasipo misukosuko nao hawakutimiza wajibu wao nao ni Baba Mzazi na Mama wa Kambo,ambao kwa imani yangu ni kuwa walikuwa mbali na Mungu.Lakini kwa kuwa Mungu ni Mkuu amemlea Kanumba na kumuinua ili lile jiwe la pembeni leo ndio limekuwa jiwe ambalo waashi wameliona bora kama jiwe la kati.Mungu alitaka kuongea na Baba ya Kanumba na Mama wa Kambo na kweli aliongea nao kuziilisha ukuu wake.

Lakini pale pale pia Mungu aliongea na Mwana alieteswa pamoja na Mama yake Mzazi,baada ya kuinuliwa na Mungu kuwa maisha waliyopita wakishirikiana na mwanae Je waliwasamee watesaji wao??? Kwa sababu tunapaswa kutambua mambo yanatokea kwa sababu!!Mungu alitaka kuthibitisha ukuu wake kwa watesaji wa Kanumba kwa kumuinua ili imani ya mzazi wa Kanumba itambue kuwa Mungu yupo na ni Mwema.

Sote tuliona mahojiano ya Kanumba na kipindi cha Zamaladi [Take One] kuwa mahusiano ya Baba na mwana yalikuwa na hitilafu,na vyombo vya habari vingi vimekua vikionyesha maisha ya Baba mzazi kutokua na support ya mwanae huyo ambaye kiuwezo tayari alijimudu kumtunza Baba yake mzazi kama zilivyo familia nyingi za Kiafrika kuwa watoto wanawajibu wa kutunza wazazi wao pindi vijana wanapojimudu kimaisha.Kwa wakilstu wanajua amri ya kumi za Mungu amri namba nne inasema waheshimu baba na mama,upate miaka mingi na heri duniani.

Kwa waelevu na watu wenye imani wanajua maana ya sentensi hiyo juu [red].Kama wanadamu ukishindana na sentensi hiyo basi,utakuwa unapingana na Mungu.

YANAYOENDELEA KWA SASA KUHUSU MAZISHI YA KANUMBA:
Mama mzazi wa marehemu Kanumba amekwisha wasili Jijini toka jana [Jumamosi] lakini kumekuwa na mivutano kati ya familia mbili ya upande wa mama ikiongozwa na Mama mwenyewe na upande wa Baba yuko Baba yake mzazi wa Kanumba,lakini vile vile wasanii wenzie na wapenzi wake wengi nao wamekuwa na upande wao wa kutaka Kanumba azikwe wapi.

1: Upande wa Mama
Mama anasema kwa kuwa yeye ndiye bidii zake zimemfikisha Kanumba kufika hapo alipofika basi angependa mwanawe azikwe Dar es Salaam,lakini kwa ndani pia zilikuwepo kuwa apelekwe Bukoba kwa upande wa mama yake anakotoka.Lakini Kwa Jadi ya wahaya kwa style ya familia ya Kanumba iliyojitokeza basi Baba yake anapaswa kulipa mahari ya mama yake na kupewa mwanae akazikwe.Kitu ambacho ujombani imesikika wakisisitiza ilo lifanyike Baba apewe Mwanae.

2: Upande wa Baba:
Yeye anasema Mwanae azikwe Shinyanga

3: Upande wa Wasanii na Wapenzi wa Kanumba
Kundi hili limeonekana kuonyesha kuwa Kanumba azikwe Dar es salaam,kundi hili kwa sasa lina support ya mama.Na kwa asilimia kubwa linaonekana kupewa uzito.Vinginevyo ule msemo wa what goes around comes around [yani watu wazima wakiulizana who is Kanumba by the way?] Jibu itakuwa fupi Kanumba asilia yake wapi?Yani hilo jina kuwa kubwa na kupendwa hivyo na jamii ya Tanzania asili yake wapi?Hapo ndipo tunaludi nyuma nakusema YAKITOKEA YANATOKEA KWA SABABU [IT HAPPEN FOR A REASON].Kwa Watanzania walio wengi wetu tunafuata uhalisia wetu toka upande wa Baba, hivyo kwa picha hiyo Kanumba asili yake ni Shinyanga.

Vijana tukigombana na wazazi,na kama una bahati ya wazazi wote kuwa wapo hai basi waheshimu sana na shukuru Mungu kwa kuwapa wazazi wanaokuombea Mungu kukulinda mara zote kabla ya kulala na bahada ya kuamka.Usijione mzima nyuma yetu kuna watu wanajitolea kufanya maombezi juu yetu.Na kama wazazi walikukosea mwambie Mungu awafungue wajue makosa yao nawaone utukufu wake kupitia wewe!!Angalia tusilejee kwenye njia waliyopita wao hivyo yaliyotokea kwa sababu yatakuwa hayana maana kwa kuwa Mungu ameya sababisha kwa sababu.

Hivyo mpaka jana usiku muafaka wa azikwe wapi ulikuwa haujapatikana Jumamosi tarehe 7 april.
 
tunajifunza vitu viwili,ukiwa maarufu usiwe uongo,kipindi cha mkasi alisema hanywi pombe,sasa nini kimetokea,kale katoto kwenye kipindi hichohicho kalisema hakana boyfriend.unayofanya gizani mungu huyaweka mwangani.namsikitia kale kabinti kwani nikadogo sana.Kanumba mungu amempenda zaidi
 
Wewe ni nani tena unatutabiria bao la ushindi wakati mpira umeshaisha na ushindi unajulikana? Hata Yahya tapeli hakuwa kama wewe! alitabiri kimachale! alikuwa anasoma kwanza picha linakwendaje ndiyo aropoke
anatunyang'anya point
tatu hivi hivi............ tena mezani !
 
Nadhani hapa kikubwa ni kumuombea apumzike kwa amani,na kama kuna funzo tumelipata kupitia kifo chake sawa, Sidhani kama ni sahihi kuanza kumjadili marehemu hadi kufikia kumhukumu kwa kuwa alikuwa mzinzi,mlevi n.k,tumuombee na mambo ya hukumu tumuachie mungu mwenyewe.

Tujiweke tayari kwani hatujui lini,saa ngapi na wapi kifo kitatukuta.

R.I.P KANUMBA
 
Jamani mazishi ya Kanumba Serikali itakuwepo, namaanisha POLISI ndio maana ya Usalama huo umati sio mdogo mahali popote penye halaiki Serikali tunayoilipia kodi lazima iwepo
Kuhusu Baba Kanumba ana haki na mwanae (sikio halipiti kichwa) huenda Baba hakupenda tabia ya makundi yake kila siku magazetini tena Udaku na kubadili mabibi
Nimemwona Kanumba kwenye mkanda kwanza kabisa akiwa na kwaya ya DINI AIC Chang'ombe Dsm hapo naona Baba mzazi alipakubali
 
tofautisha wasanii waliotumia usanii wao kwa manufaa ya taifa zima na wanaotumia usanii wao kwa manufaa yao binafsi. Wengine wanatakiwa waenziwe na taifa na wengine na wasanii wenzao na mashabiki wao. Huwezi kunishawishi mimi leo uumie kodi yangu kusafirisha msiba wa kanumba wakati kuna wagonjwa kibao leo wamekosa dawa. Sikuwa shabiki wake hata muvi zake nilikuwa naziona accidentaly kwenye basi wakati nasafiri. Tofautisha wasanii kama l.dube,blenda fasie, bob, waliotumia usanii wao kwa manufaa ya taifa wakati wa kupigania uhuru,this is nationally kwani walipopata uhuru watu wote walinufaika. Mambo ya kanumba ni yake na mashabiki wake. Kufahamika nigeria hainiletei faida yoyote mie nisie shabiki wa huu upuuzi wanaoufanya. Huwa wanashindwa hata kufanya consultation ya sehemu zinazohusu profesion fulan!


hakika TANZANIA tumepoteza mt mhim sn sn kwan tulikuwa tumeanza kufahamika kimataifa kuwa kuna nchi Tz. R.I.P the great Kanumba hakika ww ulikuwa mtu mhm sn.
 
Kwang mm utabaki kuwa mfano kwangu, kwan bado nilikuwa na mengi ya kujifunza toka kwako. Kwan nilikuwa naona juhudi zako za kujarib kueleza ulimwengu kuwa hata ss tunaweza. Sioni msanii anayeweza kufanya hii kazi kwan nimekuwa nikiona fahari kuwa na mtu kama ww nchini mwangu. Kwa nn iwe kanumba. ss mpaka lini watanzania tutakuwa wanyonge nakuonekana hatuwezi kwa nchin nyingine? R.I.P. Stvn KANUMBA tutakukumbuka milele.
 
Muongo mkubwa wewe mbona pdiddy yupo hai usitumie hili jukwaa kutuletea habari za uongo

P Diddy wa bongo mkuu... Au Perfect Kagisa..

Yule wa Maimartha wa Jesse..

Inasikitisha vijana wanapokufa mapema... Kumbe si Ukimwi tu unaoweza kuondoa maisha ya vijana..
 
si wote wanaokuangalia wanakupenda

Hasa Lulu... Anachukiwa sana,na akina mama wenzake nadhani ndiyo wengi wanaomchukia!

Hata wale wanaompenda Kanumba,nawashangaa kwa kumchukia Lulu,wakati kipenzi chao Kanumba,alikuwa "kaoza" kwa huyo Lulu..

Yaani nashindwa kushangaa!
 
Kifo chako kimetuumiza na kututia simanzi Steven Kanumba.Paska imekuwa ya uchungu kwetu Ahh a a a h umetutangulia kwenye nchi ya walio hai. REST IN PEACE Kanumba.
 
Back
Top Bottom