Tanzania yetu nchi ya kuvutia

Tanzania yetu nchi ya kuvutia

GH014J2F8.4-1.jpg
Inawavutia wazungu tu

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli ni nchi nzuri ila chama chakavu kinaiharibu.,ajabu hatupati hata nyama pori madukani.
Inashangaza sana kaka, wadau walioko Australia wanadai nyama za Mamba na Kangaroo ziko madukani, hata kwenye migahawa, hata hapo kwa Bw. Zuma tu, nyama zote pori zapatakana buchani na kwenye migahawa!
Ila kwa sasa naona waTz wamecharuka, wanatembelea mbuga aise, beach zetu na hata hoteli pembezoni ya bahari na maziwa...Tunachangamka ila kwa kasi ndogo sana, hatujajuwa ni kubana kupanga na kudunduliza mapeni tu, likizo wewe na familia hao mnapiga trip...
 
Tumenufaika vipi na huo uzuri?maisha magumu wazawa hawamudu utalii wa ndani.Yote haya yamesababishwa na ccm na genge lake
Yani ulitaka simba na swala wakusaidie maisha yako yawe rahisi..

Nikupe taarifa ndogo tu.. ukikaa kulaumu watu kutokana na maisha yako kuwa magumu, hutofikia mahali popote. Zaidi sana ujue kuwa hakuna nchi yoyote duniani ambayo haina watu kama wewe wanaolalamika kila siku maisha yao magumu.

Halafu kuna wale kama sisi ambao maisha yetu siyo magumu..
 
Ni kweli usemacho ndugu ni vigumu kwa nchi masikini yenye watu wachache wa daraja la kati kuwa na mass local tourism lakini hii ni moja tu ya sababu.

Sababu nyingine ni kwamba hatuna tamaduni ya kutembelea vivutio vyetu hata kwa hao middle class wachache wawezao kumudu gharama.

Na ndio maana wakati mwingine huwa naona labda tuweke vivutio vingine artificial kwenye mbuga zetu na hifadhi za misitu ya asili kama hotel yenye architectural design ya kipekee(but affordable), treetop walkways, cable cars, zip line, roller coasters. Hivi vyote viambatane na visitors centers za kisasa kwa ajili ya kupokea wageni zenye screen kubwa kwa ajili ya kuonyesha matukio ya moja kwa moja toka mbugani na matangazo kwenye media mbali mbali za ndani yasikauke kama ambavyo coca cola wafanyavyo. Africa kusini mwa jangwa la sahara kuna cable car moja tu, table mountain cable car iliyoko SA na niliona mahali Rwanda wanataka kujenga.

Na amini kwa kufanya hivyo soko la ndani la utalii litakua sana na tutavutia hata nchi nyingine za Africa ukiacha USA na Europe sababu waafrica wengi wanaona kama hakuna umuhimu kwenda kuangalia tu wanyama.
Mkuu Universe UPI correct kabisa,sasa tuje kwenye point,nani wa kuhamasisha hayo mazuri yote uloandika?hamna,maana hata waziri si mbunifu
 
Yani ulitaka simba na swala wakusaidie maisha yako yawe rahisi..

Nikupe taarifa ndogo tu.. ukikaa kulaumu watu kutokana na maisha yako kuwa magumu, hutofikia mahali popote. Zaidi sana ujue kuwa hakuna nchi yoyote duniani ambayo haina watu kama wewe wanaolalamika kila siku maisha yao magumu.

Halafu kuna wale kama sisi ambao maisha yetu siyo magumu..
Nyinyi ndo wale wapumbavu,yaani kikundi kidogo kiharibu rasilimali zetu alafu tuwanyamazie?
 
Mkuu Universe UPI correct kabisa,sasa tuje kwenye point,nani wa kuhamasisha hayo mazuri yote uloandika?hamna,maana hata waziri si mbunifu
Waziri Prof Maghembe ni dinosaur, haiwezi ile wizara, ni wale wazee wa kuendeshwa kwenye SU, wakifika ofisi ni chai na mandazi ya inflated prices, gazeti, mkutano apate posho siku imeisha, zaidi sana atafanya bidii ya kufa mtu na kutoa jasho kishenzi apate trips za nje! Hatuna waziri pale
 
Upo sawa,wizara inahitaji Vijana wazalendo walete mapinduzi ktk wizara,tupo wengi ila je nani wakutuona?
 
Mkuu Universe UPI correct kabisa,sasa tuje kwenye point,nani wa kuhamasisha hayo mazuri yote uloandika?hamna,maana hata waziri si mbunifu
Kuna pande mbili zinazoweza kuhamasisha na kuyafanya haya.

Serikali ifanye kazi yake vyema hasa kuandaa sheria na sera rafiki kwa wawekezaji na watalii lakini hata serikali kupitia Tanapa inaweza tenga budget kutoka katika mapato yake ya shughuli za utalii na ikafanya hayo niliyoainisha hapo juu. Kuboresha na kusimamia huduma zote zitolewazo kwa watalii ili ziwe katika viwango vya ubora vinavyokidhi vigezo vya kimataifa. Matangazo ya vivutio vyetu pia bado hayajafanywa kwa kiasi kinachohitajika na hapa ni kwa masoko yote local na international tourism.

Upande wa pili unahusisha wawekezaji binafsi. Hawa bado hawajawa wabunifu kuweza kufanya miradi itakayovuta watu zaidi. Wakati mwingine wanaweza fanya promotion ya ofa maalum ili kuvuta watu wengi zaidi kwenye makampuni yao ya utalii, na hili litafanya wafahamike na watu wengi, ni watanzania wachache sana wanafahamu angalau kampuni moja tu ya utalii nchini. Pia, matajiri wengi wakubwa nchini wamekua sijui niseme waoga wa kuwekeza kwenye sekta ya utalii nchini na hata wakiwekeza ni kwenye hoteli tu tena za "kawaida" ukilinganisha na "iconic" hotels zinazopatikana katika nchi na miji inayoingiza mamilioni ya watalii kama UAE(Dubai), paris, singapore, cape town tena hawa wanategemea urban tourism pekee.
 
Ni kweli ni nchi nzuri ila chama chakavu kinaiharibu.,ajabu hatupati hata nyama pori madukani.
Wazungu wanajivunia 'Hunting in Africa' wanajivuni nyama ya pori.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Kwa upande wa sekta binafsi kuna urasimu mwingi sana wanapotaka kuwekeza mitaji mikubwa kunakuwa na mlolongo mrefu sana na milango mingi ya rushwa.niliwahi Fanya Nazi sekta ya utalii
 
Huo ndio ubaya wa nchi zetu za "kiafrika", na nimeeleza hapo juu wahusika wa kusimamia utalii hawaweki mazingira wezeshi kwa wawekezaji ila nimeona mahali bakhresa anajenga hoteli nzuri kwa kufanya land reclamation pamoja na satellite town nzuri inaitwa fumba town huko Zanzibar.

Nafikiri ni kitu kizuri na kitavuta watalii wengi. Na mimi pia nafikiria siku moja kama nikiwa na uwezo nije kutekeleza kwa kuwekeza katika hayo niliyoainisha hapo juu.
 
Wazungu wanajivunia 'Hunting in Africa' wanajivuni nyama ya pori.
Inasikitisha kwa kweli,winda wewe uone kama askari wa nyama pori hawajakuua kinyama.,hatustahil kukosa nyama ya nyumbu,nyati,dikdik nk,iliyokaushwa ni nzuri sana uwapo safarini inakuondolea brake brake za kutafuta misosi.
 
Jaribu kuwatizama wanaoburudika hapo,kuna mzawa?hii nchi imebarikiwa ila nadhani watu wake wamelaaniwa
kaka usiwe mwoga wa maisha hapo mbona unaingia tu hata kama una kipato cha kawaida
 
Back
Top Bottom