Mukulu wa Bakulu
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 4,052
- 12,906
jipe moyoNaamini watatukopesha ili kusaidia watoto ambao ndio taifa la kesho.
Sent using Jamii Forums mobile app
Bure kwako wewe unae soma lakini waalimu hawafundishi bure, serikali inakulipia hiyo pesa ya ada uliyo futiwa.
Bure kwako wewe unae soma lakini waalimu hawafundishi bure, serikali inakulipia hiyo pesa ya ada uliyo futiwa.
Hapana mkuu, utakuwa umenitafsiri vibaya.
Hapana mkuu, utakuwa umenitafsiri vibaya.
Bank ya Dunia wiki hii mwishoni itakutana kujadiliana na kuamua kama wataikopesha Tanzania au kuipa mkopo nafuu wa kuboresha elimu wa Dollar Millioni Mia Tano ($500M) ambayo ni sawa na Shilingi za Kitanzania Trillioni 1.3.
Mwaka 2018 bank ya Dunia ilisitisha mkopo nafuu kwa Tanzania wa Dollar Millioni 300 au Billioni 660 za Kitanzania baada ya serikali kutangaza kua hakuna ruhusa kwa wanafunzi waliopata mimba kusoma katika shule za umma.
Tokea mwaka huo kumekua na majadiliano kati ya bank na serikali ya Tanzania na serikali kuahidi kua itatengeneza njia mbadala kwa watoto wanaopata ujauzito kuendelea na masomo..
Wanaharakati kadhaa pamoja na wanasiasa wamepinga mkopo huo kwa Tanzania kua utaendelea kuminya haki za watoto wanaopata ujauzito shuleni. Bank ya Dunia wanadai wamepewa uhakika na Magufuli kua watoto waliopata ujauzito watapatiwa njia mbadala kuendelea na elimu.
Soma hapa
World Bank to consider giving Tanzania $500 million education loan despite ban on pregnant schoolgirls | CNN
A multi-million dollar World Bank education loan to Tanzania is back on the table for possible approval next week after it was pulled over a year ago amid concerns about the country's policy of banning pregnant girls and young mothers from attending state school.edition.cnn.com
Waafrika akili zetu zina shida.Tukikopeshwa tutanunua mandege elimu si bure
Sent using Jamii Forums mobile app
Umesahau huyo aliempa mimba kuwa anaishia gerezani miaka 30Hii ni moja ya sheria dume na kandamizi ,nikipewa Urais kwa siku moja ikifika saa 9am sheria hii nitakuwa nimeifutilia mbali,mtoto wa kike na kiume wote wana haki sawa,why anaadhibiwa motto wa kike tu kwa kufukuzwa shule?wakati wa kiume anaendelea na masomo?,mwanafunzi mwenye ujauzito ataendelea na masomo hadi siku ya mwisho atakayoenda kujifungua,na akishajifungua anarudi shule na kuendelea na masomo na kama kichanga chake kipo jirani watapewa muda maalum(lunch time)kwa ajili ya kuwanyonyesha.social workers watapewa maarifa zaidi ya kuifanya kazi yao,elimu ya uzazi itatolewa mashuleni ili wanafunzi wajitambue,condoms na njia zingine za kuzuia STDs na mimba zitasogezwa zaidi kwa wanafunzi.