Tanzania yaweza kukosa Mkopo wa Dola Milioni 500 kutoka Benki ya Dunia

Gambino

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
3,449
2,000
Bank ya Dunia wiki hii mwishoni itakutana kujadiliana na kuamua kama wataikopesha Tanzania au kuipa mkopo nafuu wa kuboresha elimu wa Dollar Millioni Mia Tano ($500M) ambayo ni sawa na Shilingi za Kitanzania Trillioni 1.3.

Mwaka 2018 bank ya Dunia ilisitisha mkopo nafuu kwa Tanzania wa Dollar Millioni 300 au Billioni 660 za Kitanzania baada ya serikali kutangaza kua hakuna ruhusa kwa wanafunzi waliopata mimba kusoma katika shule za umma.

Tokea mwaka huo kumekua na majadiliano kati ya bank na serikali ya Tanzania na serikali kuahidi kua itatengeneza njia mbadala kwa watoto wanaopata ujauzito kuendelea na masomo..

Wanaharakati kadhaa pamoja na wanasiasa wamepinga mkopo huo kwa Tanzania kua utaendelea kuminya haki za watoto wanaopata ujauzito shuleni. Bank ya Dunia wanadai wamepewa uhakika na Magufuli kua watoto waliopata ujauzito watapatiwa njia mbadala kuendelea na elimu.

Soma hapa👇
https://edition.cnn.com/2020/01/24/...irls-world-bank-loan-asequals-intl/index.html
 
Nkanini

JF-Expert Member
Jun 6, 2017
1,878
2,000
Hii ni moja ya sheria dume na kandamizi ,nikipewa Urais kwa siku moja ikifika saa 9am sheria hii nitakuwa nimeifutilia mbali,mtoto wa kike na kiume wote wana haki sawa,why anaadhibiwa motto wa kike tu kwa kufukuzwa shule?wakati wa kiume anaendelea na masomo?,mwanafunzi mwenye ujauzito ataendelea na masomo hadi siku ya mwisho atakayoenda kujifungua,na akishajifungua anarudi shule na kuendelea na masomo na kama kichanga chake kipo jirani watapewa muda maalum(lunch time)kwa ajili ya kuwanyonyesha.social workers watapewa maarifa zaidi ya kuifanya kazi yao,elimu ya uzazi itatolewa mashuleni ili wanafunzi wajitambue,condoms na njia zingine za kuzuia STDs na mimba zitasogezwa zaidi kwa wanafunzi.
 
Lord eyes

JF-Expert Member
Aug 2, 2018
7,379
1,995
Shame Tanzania hata hili wanashindwa kulichambua mpaka wasubiri bodi ya mkopo wa bank ya dunia ndio iwape masharti na sera za mkopo huo
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
18,634
2,000
..usd 191 billion tunazowadai accacia ziko wapi?

..badala ya kukopa WB kwanini tusiwabinye accacia mpaka watulipe?

..tunaogopa nini kuwashtaki accacia MIGA?
 
GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,251
2,000
Bank ya Dunia wiki hii mwishoni itakutana kujadiliana na kuamua kama wataikopesha Tanzania au kuipa mkopo nafuu wa kuboresha elimu wa Dollar Millioni Mia Tano ($500M) ambayo ni sawa na Shilingi za Kitanzania Trillioni 1.3.

Mwaka 2018 bank ya Dunia ilisitisha mkopo nafuu kwa Tanzania wa Dollar Millioni 300 au Billioni 660 za Kitanzania baada ya serikali kutangaza kua hakuna ruhusa kwa wanafunzi waliopata mimba kusoma katika shule za umma.

Tokea mwaka huo kumekua na majadiliano kati ya bank na serikali ya Tanzania na serikali kuahidi kua itatengeneza njia mbadala kwa watoto wanaopata ujauzito kuendelea na masomo..

Wanaharakati kadhaa pamoja na wanasiasa wamepinga mkopo huo kwa Tanzania kua utaendelea kuminya haki za watoto wanaopata ujauzito shuleni. Bank ya Dunia wanadai wamepewa uhakika na Magufuli kua watoto waliopata ujauzito watapatiwa njia mbadala kuendelea na elimu.

Soma hapa
https://edition.cnn.com/2020/01/24/...irls-world-bank-loan-asequals-intl/index.html
Kwa nini mkope wakati nchi tajiri hii , ndege kwa cash , elimu kwa mkopo?
 
la magica

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
976
1,000
Wasitutishe na vijisenti vyao, na sisi ni dona kantri tunaweza wakopesha hata wao.
 
Forbes1990

JF-Expert Member
Apr 14, 2018
496
1,000
Hii ni moja ya sheria dume na kandamizi ,nikipewa Urais kwa siku moja ikifika saa 9am sheria hii nitakuwa nimeifutilia mbali,mtoto wa kike na kiume wote wana haki sawa,why anaadhibiwa motto wa kike tu kwa kufukuzwa shule?wakati wa kiume anaendelea na masomo?,mwanafunzi mwenye ujauzito ataendelea na masomo hadi siku ya mwisho atakayoenda kujifungua,na akishajifungua anarudi shule na kuendelea na masomo na kama kichanga chake kipo jirani watapewa muda maalum(lunch time)kwa ajili ya kuwanyonyesha.social workers watapewa maarifa zaidi ya kuifanya kazi yao,elimu ya uzazi itatolewa mashuleni ili wanafunzi wajitambue,condoms na njia zingine za kuzuia STDs na mimba zitasogezwa zaidi kwa wanafunzi.
Umesahau huyo aliempa mimba kuwa anaishia gerezani miaka 30

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom