The Genius
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 820
- 2,070
Picha hizi mbili zimepigwa jana tarehe 23 Julai 2021 wakati wa tukio la ufunguzi wa michezo ya Olimpiki jijini Tokyo, Japan.
Ki-utaratibu, kila nchi iliyopeleka wawakilishi inatajwa halafu wawakilishi wanapita mbele ya umati wakiwa na bendera ya taifa lao. Kutakuwa na jumla ya matukio 339, kwa aina za michezo 33, kwa namna 46
Picha ya juu ni tukio baada ya Tanzania kutajwa. Wawakilishi wa Tanzania ni watatu tu, lakini hawakuwepo. Hapa alionekana mtu mmoja mwenye asili ya Asia akipeperusha bendera ya Tanzania kama mwakilishi wa nchi yetu.
Picha ya chini ni tukio baada ya Kenya kutajwa.
Jumla ya wanamichezo 11,091 kutoka nchi 206 duniani watashindana kupata medali za dhahabu, fedha au shaba. Zipo nchi zimepeleka wanamichezo 100+, 200+, 400+ hadi 600+
Tanzania, nchi yenye watu takribani milioni 60, na asilimia zaidi ya 90 wapo chini ya miaka 35, umri wa michezo, imepeleka wawakilishi watatiu, ambao hawajaonekana wakati nchi yao ikitajwa.
Vijana wamebaki ndani ya nchi yao wanacheza ndondo, kubeti, singeri na kuuza karanga. Viongozi wao hawajali! Maneno mengi ya kutia matumaini yanasemwa majukwaani, vijana wanakubali bila kufikiri, na akili ya kudai hawana. Wamefungwa akili, wanaamini Mungu ndiye aliyewapangia kuwa kama walivyo, siku yao itakuja... miaka mia ijayo.
Ni nani mwenye akili ya kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kuboresha sekta ya michezo na kuiunganisha nchi na jumuia za michezo za kimataifa? Hakuna. Kuna wizara ya michezo? Ipoipo tu.
Tuendelee na masiasa yetu ya kuumizana, ndicho tunachoweza.