Tanzania yatengwa EAC community

Tanzania yatengwa EAC community

isqo omy

Member
Joined
May 30, 2013
Posts
99
Reaction score
6
*Rwanda, Kenya, Uganda na Burundi zaungana kuunda Shirikisho la Kisiasa
*Waziri Sitta asema zina ajenda ya siri, ashangaa marais kuwaburuza wananchi wao.

HATIMAYE Tanzania imewekwa kando rasmi na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), katika kuunda Shirikisho la Kisiasa litakaloziongoza nchi hizo.

Tayari marais wa nchi hizo, Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Pierre Nkurunzinza wa Burundi wamekwishafikia makubaliano ya kuanzisha mchakato wa kuandikwa kwa Rasimu ya Katiba ya Shirikisho la Kisiasa la nchi wanachama waEAC, bila kuishirikisha Tanzania.

Waziri wa Serikali za Mitaa wa Rwanda, James Musoni,amekaririwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo akieleza kuwa makubaliano ya kuanzishwa kwa mchakato wa kuandikwa kwa Rasimu ya Katiba ya Shirikisho la Afrika Mashariki, yalifikiwa Septemba 12 mwaka huu, mjiniKampala na marais wa Rwanda,Kenya na Uganda na hivi karibuni Rais wa Burundi ambaye alialikwa katika mkutano huo na kushindwa kuhudhuria, naye sasa amethibitisha ushirika wake katika shirikisho hilo jipya.

Gazeti la The Sunday Times la Rwanda, limemnukuu Waziri Musoni kuwa marais wa nchi hizo wamekubaliana kukamilisha rasimu hiyo ndani ya muda mfupi.

Musoni ambaye alikiri kushiriki katika mkutano wa marais hao ulioshirikisha pia maofisa waandamizi wa nchi hizo isipokuwa Tanzania, alisema uamuzi uliofikiwa katika mkutano huo ambao ni wa pili kufanyika, ni moja ya maagizo ya uamuzi uliofikiwa kwenye mkutano wa kwanza uliofanyika piamjini Kampala.

"Tumekubaliana juu ya kanuni za kisheria na mpango mzima utakaotuongoza ili kupata Rasimu ya Katiba itakayoliongoza shirikisho hilo la kisiasa," alikaririwa Musoni.

Alieleza kuundwa kwa kikosi kazi maalumu kitakachojulikana kwa jina la High Level Task Force (HLTF), ambacho kitajumuisha wataalamu wa nyanja mbalimbali watakaoandika Rasimu hiyo kwa namna ile ile ya ulivyoandaliwa mpango wa Itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya AfrikaMashariki.

Musoni alisema mawaziri wa nchi wanachama waliopangiwa kushughulikia shirikisho hilo,wanatarajiwa kuelezea mwelekeo wa mafanikio ya mpango huo katika mkutano mwingine uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba huko Kigali Rwanda.

Kwa mara ya kwanza, marais Kagame, Museveni na Kenyatta walikutana kufikia makubaliano ya kuharakisha uundwaji wa shirikisho la kisiasa kwa nchi zao kwa kuondoa vikwazo vya kiuchumi na kuweka hati ya vitambulisho vya pamoja na ushirikiano wa kibiashara sambamba na kuzindua mradi wa ujenzi wa gati ya Bandariya Mombasa.
 
Kwanza yalikuwa ni makosa makubwa ya serekali kuzikubali nchi za Rwanda na Burundi kuingia katika shirikisho nakumbuka wananchi tulipiga kelele lakini wanasiasa wanafikiri wao wana akili kuliko wananchi hawakutaka kutusikiliza.
 
Kama wana haraka ya kuungana waache waungane, mwisho wa siku bomu likilupuka ni wao watakao umia. Kama wanaona maswala ya kuungana ni ya mzaha mzaha na Tanzania ina wachelewwsha basi haiko waendelee na mikakati yao.

Ukweli unabaki kwamba Tanzania ina uzoefu ya mambo haya kutokana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndio maana tuna sita. Pili nchi zote za Afrika Mashariki zina matatizo ya ndani ambayo mkiungana nchi zote shiriki mtarithi. Kenya kuna ukabila, Uganda kuna ukabila na Museveni yeye anataka kuwa raisi wa nchi itakayo kuwa East Africa, Rwanda nao ukabila nk. Kweli shirikisho lita fanikiwa kwa hali hiyo?
 
............Waache waungane hao wafu hatuna haja ya kurithi matatizo ya ukabila na vita, haya ya kwetu yanatutosha.
 
Kwanza yalikuwa ni makosa makubwa ya serekali kuzikubali nchi za Rwanda na Burundi kuingia katika shirikisho nakumbuka wananchi tulipiga kelele lakini wanasiasa wanafikiri wao wana akili kuliko wananchi hawakutaka kutusikiliza.

nakumbuka wananchi walikataa na walisema ni mapema mno lakin mchakato wa kuwaweka ukaenda fasta fasta wakajiunga
 
Kama wana haraka ya kuungana waache waungane, mwisho wa siku bomu likilupuka ni wao watakao umia. Kama wanaona maswala ya kuungana ni ya mzaha mzaha na Tanzania ina wachelewwsha basi haiko waendelee na mikakati yao.

Ukweli unabaki kwamba Tanzania ina uzoefu ya mambo haya kutokana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndio maana tuna sita. Pili nchi zote za Afrika Mashariki zina matatizo ya ndani ambayo mkiungana nchi zote shiriki mtarithi. Kenya kuna ukabila, Uganda kuna ukabila na Museveni yeye anataka kuwa raisi wa nchi itakayo kuwa East Africa, Rwanda nao ukabila nk. Kweli shirikisho lita fanikiwa kwa hali hiyo?

Sawa lakini mkumbuke wanatumia fedha za EAC kufanya vikao bila kuishirikisha Tz wakati nayo inachangia jumuiya. Hii si halali kabisa.
 
nakumbuka wananchi walikataa na walisema ni mapema mno lakin mchakato wa kuwaweka ukaenda fasta fasta wakajiunga

Yah umesema kweli kabisa. Saizi wanataka kurudia kosa lilelile kwenye huu mchakato wa katiba mpya.

Kuna watu watamsukuma rais aweke sahihi kwenye sheria ya katiba bila kutafakari.

Baadaye watarudi kupiga kelele kuna watu wanafanya nchi isitawalike kumbe chanzo ni wao.

Mwisho wa siku watakuta kama ilivyo mtwara nchi yote itahitaji kutawaliwa kwa marshal law.

Ukiangalia na hii pressure inayoletwa na hawa walio jitenga na eac yao ya kichina, utakuta Mh rais atakuwa mtu aliye maliza kipindi chake cha utawala akiwa katika hali ngumu sana.
 
Jamani Rwanda na Uganda zinaongozwa kijeshi tofauti na Kenya na Tanzania ambako kuna japo kaharufu ka demokrasia. Huwezi kuunganisha nchi kama hizi. hata EU ilizitaka nchi wanachama na zile zinazotaka kujiunga na umoja wao wa ulaya watimize masharti fulani fulani kabla ya kujiunga, sasa EAC ilitoa masharti gani kwa Rwanda na Burudi na huenda Sudani ya kusini?, EAC ilifanya nini Museven ilivyobadilisha katiba yake ili aongeze ukomo wa rais madarakani? hapa hakuna muungani bali kunyemelea utajiri wetu na kututapikia baadhi ya matatizo yao yanayohusu ardhi na waasi wanaosumbua nchi zao kwasababu ya kukosekana demokrasia ndani ya nchi zao
 
Let them go... Ila watajikuta wamesahau hazina moja kubwa sana...nayo ni Tanzania! Tanzania ni kubwa kwa eneo kuliko nchi hizo zote zikiungana kwa pamoja. Ukubwa wetu ni hazina tosha. Toka lini samaki akameza mamba, hata kama huyo mamba amelala?
 
Kwanza yalikuwa ni makosa makubwa ya serekali kuzikubali nchi za Rwanda na Burundi kuingia katika shirikisho nakumbuka wananchi tulipiga kelele lakini wanasiasa wanafikiri wao wana akili kuliko wananchi hawakutaka kutusikiliza.

unataka kuniambia kenya na uganda vinaendeshwa na rwanda na burundi? la kuvunda halina ubani tuachane na hili shirikisho kuilindia heshima tz.
 
Wanaungana afu sisi tunawamwaga wazenji.funny. Niliwahi kusoma a page ya bible inasema "kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe"go tz
 
Kama wana haraka ya kuungana waache waungane, mwisho wa siku bomu likilupuka ni wao watakao umia. Kama wanaona maswala ya kuungana ni ya mzaha mzaha na Tanzania ina wachelewwsha basi haiko waendelee na mikakati yao.

Ukweli unabaki kwamba Tanzania ina uzoefu ya mambo haya kutokana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndio maana tuna sita. Pili nchi zote za Afrika Mashariki zina matatizo ya ndani ambayo mkiungana nchi zote shiriki mtarithi. Kenya kuna ukabila, Uganda kuna ukabila na Museveni yeye anataka kuwa raisi wa nchi itakayo kuwa East Africa, Rwanda nao ukabila nk. Kweli shirikisho lita fanikiwa kwa hali hiyo?
hiyo ni united snakes of east africa!Kenya please, watch ya back!!!1
 
Kwanza yalikuwa ni makosa makubwa ya serekali kuzikubali nchi za Rwanda na Burundi kuingia katika shirikisho nakumbuka wananchi tulipiga kelele lakini wanasiasa wanafikiri wao wana akili kuliko wananchi hawakutaka kutusikiliza.

Na kihelehele kikubwa kilitoka kwetu
 
Based on the current situation of EAC with lack of interactions between people and greediness of Kenya and Rwanda plus no economic ties between the members, I think the four countries will end up with Political Platform/PP (Jukwaa la Kisiasa), not Political Federation/PF (Shirikisho la Kisiasa). Political Federation/Union is also an ultimate goal of the European countries, however, they are still facing various challenges on the matter, how easily East Africa can reach such stage given that the EAC is almost depends on financing from Donors.

Political federation is a "political structure of economic integration" but it must be laid down by strong foundations of economic union which currently is not exist.
 
Back
Top Bottom