Tanzania yatengwa EAC community

Tanzania yatengwa EAC community

Ni vema hiki kitu kinachoitwa EAC kivunjike mara moja kwani kinachoendelea ni unafiki. Museveni anataka kutengeneza CV ya kuzikiwa kwamba aliwahi kuwa Raisi wa Afrika Mashariki!
 
Kama wana haraka ya kuungana waache waungane, mwisho wa siku bomu likilupuka ni wao watakao umia. Kama wanaona maswala ya kuungana ni ya mzaha mzaha na Tanzania ina wachelewwsha basi haiko waendelee na mikakati yao.

Ukweli unabaki kwamba Tanzania ina uzoefu ya mambo haya kutokana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndio maana tuna sita. Pili nchi zote za Afrika Mashariki zina matatizo ya ndani ambayo mkiungana nchi zote shiriki mtarithi. Kenya kuna ukabila, Uganda kuna ukabila na Museveni yeye anataka kuwa raisi wa nchi itakayo kuwa East Africa, Rwanda nao ukabila nk. Kweli shirikisho lita fanikiwa kwa hali hiyo?
Mgonjwa jumlisha Mgonjwa jibu ni Mahututi
 
kitendo cha kufukuza raia wao kama wanyama kimewauzi sana,moyoni kimewauma sana,na uwezi kushirikiana na mtu aliofukuza ndugu zako

Wacha waanze safari yao mpya. Watanzania tunawatakia kila la heri katika hilo shirikisho lao jipya la chapuchapu🙂. Tuwaambia hivi... 'Huko Wanakokwenda Watatukuita tumefika'...na hatuna wasiwasi..

Mwisho, Kwa maoni yako walitaka tuwalele (baby sit) raia wa nchi zao mpaka lini? Na Je, mzigo wa raia wetu anatusaidia nani kutulelea?
 
Weee vp? Tuwaombe radhi kwa lipi? Tanzania as a sovereign state can exist on its own! Let them do what thei can! Lakini nyota ya tanzania itaendelea kuwaka
 
Tanzania is not in a hurry for the integration of EAC until Museven is ready to step down and allow term limits, Kagame stop using the 1994 genocide to capitalize his power for permanent victimazation of tuts and criminalization of hutus and Kenya should elect their leaders based on issues not vesting on big tribes like the way Uhuru Kenyatta ascended to power in the last election.

Tanzania can stay alone without EAC, is better to be alone than joining the axis of evils who use violence and force to grab power and later manipulate constitution to hang on power exactly what Kagame and Museven did previous years ago and later changed constitution to rule for life. The EAC is nothing than a stepping stone for Kenya, Uganda and Rwanda to invade Tanzanian land since their overpopulated in their own countries now their looking for scape goat to release their pressure and that scape goat is Tanzania

DRC refused to join the EAC because they knew exactly what Rwanda, Uganda and Kenya were looking for, just to benefit by grabbing DRC and Tanzanian lands under the name of free movement of people. Tanzania to be in EAC is like a one way traffic since the other countries will benefits from Tanzania than what Tanzania will benefit from them, with abundance of water bodies, immense minerals, huge everlasting land Tanzania needs nobody for its own development, it's good for the weak like Kenya, Uganda and Rwanda to unite for their own development. Tanzania got many friends like DRC, Mozambique, Zambia and Burundi if we need to unite not necessary to be with Kenya, Rwanda or Uganda
 
Kuna principle ya UMOJA NI NGUVU, UTENGANO NI UDHAIFU. Mwalimu Nyerere alikuwa tayari kuchelewesha Uhuru wa Tanganyika ili Afrika Mashariki tupate Uhuru pamoja na kuwa nchi moja.

Kuogopa kuungana kwa sababu una ardhi ni mediocrity; kwani ukiwa na kitu ukaungana kinaacha kuwa chako? Kama kuna mtu au kijiji chenye ardhi ekari elfu moja sasa hivi, tukiungana hizo ekari elfu zinaacha kuwa mali ya hicho kijiji? Au kijiji hicho kitalazimishwa kuiuza hiyo ardhi? Kuna mediocrity hapo.

Serikali ya CCM imeshindwa vibaya kudumisha hali nzuri kati yetu na majirani zetu wa Malawi, Rwanda na hata Kenya na Uganda. Ila kuna tumaini: wakiingia wapinzani serikalini 2015, watazawasisha hii hali. Wataaminiwa na majirani zetu.

Ile kanuni ya mwasisi wa CCM kwamba "Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja" imekufa naye?
 
Ambae simuelewi vizuri ni Kenyatta. Anaelekea kuwafanyia makosa makubwa sana wakenya!
 
Binafsi nimefurahi kusikia habari hii.
EAC ya kwanza ilituumiza sana hatuko tayari kuumia mara ya pili.
SADC ni nzuri zaidi kuliko EAC, nategemea kwenye hotuba ya mwezi JK atafanya conclusion ya kujitoa rasmi ktk hiyo iliyoitwa EA.
Tunawatakia heri na fanaka huko mwendako ndugu zetu EAF = East Africa Federation
 
tofauti ya Tanzania na nchi nyingine wanachama ilianzia kwenye suala la ardhi miaka mitatu iliyopita. nchi 4 zilipendekeza kuwa wananchi wa EAC wawe huru kununua na kumiliki ardhi ktk nchi yoyote ile mwanachama. Tanzania ndiyo nchi kubwa kuliko zote na ndiyo iliyo na angalau ardhi ambayo haijawahi kanyagwa na binadamu. Tanzania iliogopa pendekezo hili kwa kuamini kuwa raia wa nchi nyingine zitavamia ardhi na kuinunua kwa pupa! jambo hili liliwakera wanachama wengine na ndiyo chanzo cha kuiona Tanzania kama kikwazo kwa umoja wa EAC. je kuhusu hili la Tanzania iko sahihi au la?

IKO SAHIHI KABISA.Tusipoteze dira ya mustakabali wa maendeleo wa wananchi wetu,kwani pasipo ardhi hakuna maendeleo yoyote ya maana kwa wananchi wetu.Kumbuka hao wameishamaliza ardhi yote kwa masetla na viongozi wa juu kisisa na kwa matajiri wachache.Vurugu zinaweza kuwalipukia wakati wowote dhidi ya wanainchi wao wenyewe,maana bila ardhi hakuna uhai.Sasa wananyemelea ardhi yetu ili wapate pa kupumulia(internal conflicts) zinzoweza kuwakumba wakati wowote.Tuwe wavumilivu tusihamaki wao kututenga bado msimamo wetu ni thabiti na wenye manufaa kwetu zaidi kijamii,kisiasa,na kiuchumi.TUWE WAANGALIFU TUSIJE KUUTUPA URITHI WETU WATANZANIA.
 
nakumbuka wananchi walikataa na walisema ni mapema mno lakin mchakato wa kuwaweka ukaenda fasta fasta wakajiunga
Wamejiunga kwenye nini hasa? Hapo kila mmoja ana ajenda yake: Kenya ni kimaslahi zaidi i.e biashara specifically bandari ya M'SA : Uganda- M7 alisha sema siku nyingi kwamba anataka kuwa Rais wa kwanza wa Est Africa na ndie alikuwa anampigia debe PK (Rwanda) ajiunge na Shirikisho, lakini hao wawili i.e PK na M7 wana ajenda zao za siri zaidi kuhusu East Africa: Rwanda, inacho tafuta zaidi pale ni kutaka ahungwe mkono na nchi hizi kama usalama wa nchi yake utakuwa mashakani, he (PK) knows suala la Wahutu kutaka kuchukuwa tena madaraka nchini mwake (Rwanda) alijafa, wapinzani wake watajipanga kurudi Rwanda kwa style ile ile aliyo itumia PK kuingia madarakani: Burundi - kisakolojia sioni Burundi kama inachangamkia sana suala hili la kutenga nchi mwanachama, wanaudhulia mikutano kama geresha tu hawana interest sana na jambo hili, Mh.Nkuruzinza inajua yaliyo wapata Marais wenzake Wahutu walio mtangulia na anajua wahusika wakuu walikuwa wakina nani - sio mjinga. Kwa kifupi: Kenya - biashara: Uganda - Urais wa East Africa na kuendeleza ndoto za HIMA Empire wakishirikiana na PK. : Rwanda - ina nia ya kuhungwa mkono kijeshi just in case, wako paranoid wanafikili WATAVAMIWA na wapinzani wa regime ya Kagame, PK anajua fika wapinzani wake wengi wao ni Wahutu na moderate TUTSIS wapenda amani, anajua vile vile kwamba historia inaonyesha hakuna nchi yoyote duniani ambayo Minority walifanikiwa kuwatawala majority 4 ever - Demise of Omnipotent Apartheid South Africa should serve as awake up call 4 PK and his regime.
 
kitendo cha kufukuza raia wao kama wanyama kimewauzi sana,moyoni kimewauma sana,na uwezi kushirikiana na mtu aliofukuza ndugu zako

Lazima ujifunze kukua na kuacha ujinga,haya mambo huyajui kwa undani,you better shut up!hujui laiti ungelijua ungewashauri hao wapuuzi,au uwe na ajenda ya kutumwa,Kenya ardhi yote imeibwa na skins Uhuru na matajiri wachache,Uganda marafiki WA karibu WA Museveni na wahindi wamechukua ardhi yote,Rwanda ni mkoa tuu kieneo lakini nchi kimamlaka hakuna ardi,Tanzania ni nchi pekee ambayo Mtanzania yoyote anaweza kuamka Leo kutoka Ushirombo akaenda Tabora kujikatia ardhi na kulima bola bughudha,tunaharakia nini kuingia kwenye Federation wakati Economic intergration haiko stable?hujui motive behind this preside,pls,Shut Up
 
Watanganyika mtakimbiwa na kila mtu coz roho zenu mbaya a.k.a mafisadi.
 
Mimi nafikiri MMEPANIC kusikia wenzetu wanatumwaga!Ukweli ni kwamba Tanzania ndio imekuwa kikwazo kikubwa kwa kuharakisha soko la pamoja la shirikisho la Africa mashariki.Kulikuwa na sababu kadhaa zilizosababisha kutokuharakisha huko ikiwemo elimu kuwa watanzania wengi hawana elimu hivyo watakuwa manamba wa wageni.Pia kulikuwa na hoja ya ardhi kuwa wenzetu wanahitaji ardhi yetu.Na pia kulikuwa na hoja ya ukabila kuwa wenzetu ni wakabila sana kuliko sisi hivyo kuungana nao ni kujifunza Yao.

Kiukweli watanzania tuna USHAMBA na UBINAFSI Fulani hvi,ambao unasababisha watu wadumae kifikra.Sasa kama watu hamsomi na kuzingatia elimu wakenya wakija Tanzania si ndo watawa-mobilize msome?Au kama mataifa mengine Yana ukabila si ndio tutaupunguza huo ukabila kwa kuchangamana nao(refer hotuba za Nyerere),au kama ni issue ya ardhi si ndio tutakuwa makini na kuchangamkia fursa za kumiliki ardhi na kuacha kushinda vijiweni kunywa ghahawa na kucheza draft huku tukiacha ardhi kubwa bila matumizi?

Kwanza hata yale yote tuliokuwa tunajivunia yote tulishayaacha,sasa hivi watanzania ni WADINI,WAKABILA na WABAGUZI kupita maelezo.Ni mara ngapi humu ndani tunapost thread za kibaguzi za KIDINI na KIKABILA?

Mie naona ni wakati wa kuwa waungwana na kuwaomba radhi wenzetu ili tujenge shirikisho letu vyema!Haiwezekani tunahubiri shirikisho wakati huo huo tunawafukuza nchini wenzetu na kuwaita wakimbizi na kuwaacha raia wa Oman,Syria na Egypt wamejazana pale kariakoo wakiwa n pasipoti feki!

TUACHE UNAFIKI!

Nadhani wewe unahitaji kujifunza zaidi kuhusu masuala ya uhusiano wa kimataifa maana unachanganya hoja nyingi zisizoendana na pia umekariri tungo zisizo na kichwa wala miguu kutoka nchi fulani ya jirani. Watanzania si kwamba wanaogopa shirikisho kwa kuwa woga ila ni kwa kuwa hawaoni kama wao wanaweza kufaidika zaidi na shirikisho hili kulingana na UFINYU was fursa katika nchi nyingine. Nchi karibu ya zote ukiacha Tz ziko 'saturated' kwa idadi ya watu, ajria na resources nyingine, kwa hiyo zinatafuta mahali pa kupumulia. Kwa hiy lazima tujiulize sis tutapata nini? Hii ni akili ya kawaida tu wala haihitaji kusoma saaana kulielewa.

Halafu wimbo wa kikasuku mliokaririshwa kuwa eti Watz ni wavivu umepitwa na wakati. Kama labda kuna ukweli labda unazungumzia Watz wanaokuzunguka wewe (labda mtaa, kabila au eneo). Kwa sisi Watz halisi tutakushangaa maana kijijini kwetu sis tunashinda shamba tukilima au kuvuna acha hizi kazi zenu za kushinda mnachezea facebook, kwa hiyo ukiniambia sisi ni wavivu sikuelewi kabisa. Nchi yetu ndio ina- food security imara zaidi kuliko hizi nchi zinazojidai eti ni za watu wachapakazi wakati njaa kwao haibanduki.

Mwisho, muungano haulazimishwi, na isitoshe sisi na mabingwa wa miungano na ndio tunaopaswa kutoa elimu kwa nchi hizi zote zinazokumbuka shuka wakati kumekucha. Kumbuka, once beaten, twice shy ni msemo ambao ni relevant mno kwenye hali ya sasa ya jumuia hii
 
Hata mwl nyerere alipoona muungano wa Africa mashariki hauna tija aliuvunja we can not sell out our dignity for the name of unity!
 
Kuna principle ya UMOJA NI NGUVU, UTENGANO NI UDHAIFU. Mwalimu Nyerere alikuwa tayari kuchelewesha Uhuru wa Tanganyika ili Afrika Mashariki tupate Uhuru pamoja na kuwa nchi moja.

Kuogopa kuungana kwa sababu una ardhi ni mediocrity; kwani ukiwa na kitu ukaungana kinaacha kuwa chako? Kama kuna mtu au kijiji chenye ardhi ekari elfu moja sasa hivi, tukiungana hizo ekari elfu zinaacha kuwa mali ya hicho kijiji? Au kijiji hicho kitalazimishwa kuiuza hiyo ardhi? Kuna mediocrity hapo.

Serikali ya CCM imeshindwa vibaya kudumisha hali nzuri kati yetu na majirani zetu wa Malawi, Rwanda na hata Kenya na Uganda. Ila kuna tumaini: wakiingia wapinzani serikalini 2015, watazawasisha hii hali. Wataaminiwa na majirani zetu.

Ile kanuni ya mwasisi wa CCM kwamba "Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja" imekufa naye?
kwa nini tulaumiane na kuilaumu Ccm hata katika swala ambalo hawapaswi kulaumiwa? ni tangu lini Tanzania ama Ccm walikataa kushiriki katika jumuiya ambayo Tanzania ndo ilikuwa kinara wa kuanzishwa kwake hiyo jumuiya? hapa kunayo vita ya kiuchumi kati ya Tanzania na kenya hilo ni moja na la pili kunayo vita Kati ya Rwanda na Tanzania kwa habari ya Ardhi Rwanda inaunyemelea sana Ardhi ya Tanzania ndiyo maana walikuwa wanataka maswala ya umiliki wa Ardhi kwa raia wanaotoka Ktk nchi jumuiya yawe ni yawekwe free raia wa nchi mwanachama amiliki ardhi kwa nchi yeyote bila kuweka mpaka serikali ya Tanzania ni makini ilikataa kuuweka huo mkataba saini kwa maana ya kwamba mtanzania hatafaidika na mkataba huo bali nchi kama Rwanda ambayo ardhi yake ni ndogo sana ndo watakaofaidika.jambo hili lilizusha hasira sana kwa serikali ya Rwanda na hata Uganda hivyo wakawa wanalalamika ya kuwa Tanzania itengwe nao hao wamepiga kampeni kwa misingi hiyo.kw upande wa kenya ilionekana kuwa Tanzania itampa upinzani kwenye maswala ya bandari na usafirishaji kwani nchi za Rwanda,Burundi na Uganda hazina bandari na zitahitaji kutumia mojawapo Kati ya bandari ya Mombasa ama Dar es salaam na kwa uwezekano mkubwa Dar ndo bandari ambayo ingekuwa na nafasi nzuri zaidi ukizingati ya kuwa bandari hiyo ndiyo iliyopo karibu zaidi na nchi hizi kwa hapo ndipo kenya nayo ikafanya fitna ili nchi ya Tanzania iwekwe kando kwenye jumuiya na hivyo iwe rahisi kwa kenya kufanya biashara na nchi hizo kwa maana ya kuwa ni jumuiya . hizo ndo sababu za hayo yaliyotokea.sasa kwa hapa sioni sababu ya kuilaumu serikali yetu katika hili maana wangeingia kichwakichwa wakati Ardhi ingepokonywa tungewalaumu ya kuwa serikali imeshindwa kuwalinda watanzania kwa kutokujali maslahi yao
 
Mimi sioni ajabu. Kwanza tungeli tatua suala la muungano wetu kabla kupapia ya EAC. Tuanze na hili la Tanganyika na Zanzibar. Tanzania wanakabiliwa na suala gumu la muungano japokuwa serikali ya CCM hawaelezi raia wake. Mambo yamejaa ulimwenguni. Macho ya wafadhili yanaangalia Tanzania . hahahhahaha
 
Back
Top Bottom