Harvey Specter
Member
- Jun 26, 2024
- 33
- 46
Wanasheria Tito Magoti na Bob Chacha Wangwe kupitia Kesi Na. 59 ya mwaka 2025 wameishtaki Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ), wakilalamikia vitendo vya ukiukwaji wa taratibu za Uchaguzi, kushindwa kusimamia, kuongoza na kutizama uchaguzi katika viwango vya kisheria vinavyokubalika.
Katika kesi hiyo waleta maombi wanapinga uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 kwa misingi ya uvunjifu wa Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Treaty), hususan:
1) Kifungu cha 6(d) – uchaguzi na matukio baada ya hapo havikuzingatia misingi ya utawala bora, demokrasia, utawala wa sheria, pamoja na haki za binadamu na za watu.
2) Kifungu cha 7(2) – vitendo vya mamlaka kabla, wakati na baada ya uchaguzi vilikosa uwazi, uadilifu na kuheshimu haki za kisiasa, kinyume na kanuni shirikishi za uendeshaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
3) Kifungu cha 8(1)(c) – usimamizi wa uchaguzi na hatua za baadaye za dola ulidhoofisha demokrasia, haki za binadamu na utawala wa sheria, na hivyo kuhatarisha malengo na utekelezaji wa Mkataba ambao nchi wanachama wanapaswa kuepuka vitendo hivyo.
Katika Kesi hiyo Waleta Maombi wanaomba Mahakama husika itoe matamko yafuatayo;
Pamoja na hayo wameomba Mahakama itoe AMRI kwamba:
1) Uchaguzi wa tarehe 29/10/2025–01/11/2025 ulikuwa na kasoro za msingi na hivyo ni batili chini ya viwango vya EAC.
2) Uchaguzi mpya ufanyike kwa kuzingatia kikamilifu Mkataba wa EAC, kanuni za uchaguzi za EAC, na viwango vya uchaguzi wa kidemokrasia vya AU na SADC.
3) Uchaguzi wowote mpya uendeshwe kwa kuzingatia kikamilifu viwango vya kikanda vya uangalizi wa uchaguzi na kanuni za demokrasia.
4) Uchunguzi wa haraka ulio wazi, huru na usio na upendeleo, ufanyike ukisimamiwa na vyombo vya EAC kuhusu ukiukwaji wote wa uchaguzi, kabla, wakati na baada ya tarehe 29/10/2025, na wahusika wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
5) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilipe fidia, malipo ya madhara na marekebisho (reparations) kwa waathirika.
6) Tanzania ichukue hatua stahiki za urekebishaji, ikijumuisha huduma za kitabibu, kisaikolojia, kisheria ana kijamii kwa waathirika na jamaa zao.
7) Dola iombe msamaha wa wazi kwa manusura na familia zao.
8) Dola ifanye mageuzi ya kisheria na ya kitaasisi ili kuzuia kutokea tena kwa uvunjifu kama huo wa taratibu za uchaguzi.
Katika kesi hiyo waleta maombi wanawakilishwa na Mawakili Waandamizi wakiwemo Donald Deya, Arnold Tsunga, Jeremiah Bamu, na Jebra Kambole.

- Kwamba, vitendo na uzembe wa Tanzania vinavyohusiana na uchaguzi wa tarehe 29/10/2025 vimekiuka Mkataba wa EAC.
- Kwamba, mchakato wa uchaguzi wa tarehe 29/10/2025 na matokeo ya tarehe 01/11/2025 havikutimiza viwango vya lazima vya uchaguzi wa kidemokrasia chini ya sheria na miongozo iliyokubaliwa ndani ya EAC, AU na SADC.
- Kwamba, uvunjifu mkubwa wa haki kabla, wakati na baada ya uchaguzi kulifanya mchakato huo kuwa “siyo uchaguzi,” kinyume na Mkataba wa EAC na kanuni za kidemokrasia.