Tanzania yashika mkia viwango vya furaha duniani

Tanzania yashika mkia viwango vya furaha duniani

Ukiendesha gari unapigwa faini ,kila eneo ni 50km/hr ,Ukipanda basi mwendo wa kobe.Kila sehemu asikari anauliza stika.Furaha itatoka wapi?
 
Mhh ukweli upo wapi hapo hadi Nchi zenye vita nazo zipo juu yetu Iraq na Sudan zote hapo hapana au Malawi
 
Huu utafiti ni uchwara ni Sawa na ule wa taasisi ya Twaweza ya hapo Tanzania inayotoa tafiti kulingana na upepo.

Wazungu ni wapuuzi tu sina hata muda wa kuwasikiliza.

Mfano, wanyarwanda wamehojiwa na BBC Swahili, wanyarwanda wote wamekataa na wamesema wao wana furaha. Amani na kila Raha.

Hata hapo Tanzania wamesema wanafuraha. Sasa wao walihoji watanzania au wanyarwanda wa wapi?

Je, hapo furaha inazungumziwa ya aina gani mfano, nchi zenye vita zinakuwaje juu ya Tanzania
Watafiti hao je, walihoji watu wa Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Iraq, Libya, Syria, na zingine kama hizo wakaiona furaha huko?

Huu ni utafiti uchwara na wazungu pori kutuona waafrika kama vile sisi sio viumbe.

Mi kwa kifupi niseme, naishi na wazungu ni wanafiki Sana sana.
 
Ukiendesha gari unapigwa faini ,kila eneo ni 50km/hr ,Ukipanda basi mwendo wa kobe.Kila sehemu asikari anauliza stika.Furaha itatoka wapi?
Na wengine mlishazoea spidi kuanzia 120!
 
Taarifa hii imetangazwa na BBC jioni ya leo kutokana na utafiti uliofanywa imeonyesha kuwa Tanzania ni nchi ya tatu duniani kwa watu wake kuwa na uzuni, nchi nyingine ni Rwanda na Burundi.

Hii inatokana na uendeshaji wa nchi awamu hii ya tano, uliosababisha vipato vya wananchi kushuka sana na kusababisha ugumu wa maisha.

Matumizi ya nguvu za vyombo vya dola na mabavu yanatumiwa na watawala kiasi cha kuwanyima wananchi uhuru wa kutoa mawazo na hisia zao kiasi cha kusababisha msongo wa mawazo

Hii ni hatari sana kwa taifa. Huzuni nikijaa ndani ya moyo wa mwanadamu husababisha matokeo mabaya sana maana mwanadamu hupata kitu kinachoitwa kisaikolojia burn out na kufanya mambo yasiyotarajiwa.

Hii ni hatari tunakoelekea ni kubaya
 
Source CNN &Millard Ayo
Screenshot_2017-03-20-20-23-53.png
 
Wananchi watakuwaje na furaha rais Baba Jesca Mkuu wa Mkoa Dar Bashite?
 
Kwa matamko kama ya Leo furaha inatoka wapi.kila kitu chuki ubabe kiburi na kujikweza
 
Mh hadi Syria wanafuraha zaidi yetu? Lakini vile vile kuna watu tena wasiostahili kuwa na raha humu nchini wanafuraha zaidi hata ya raia wa Norway (walioshika namba 1 kwenye hiyo orodha). Halafu unamuona mtu anasimama kwenye jukwaa anasema hii nchi ni yetu sote.🙄
 
Hiyo CNN yenyewe hata rais wao kaipiga ban kuandika habari za ikulu! We kwa Akili yako ya kawaida tu bila kushawishiwa, hivi unaamini nchi iliyojaa alshabaab na nchi iliyoja boko haram inaweza kuwa na Furaha kuliko Tanzania?
 
Taarifa isiyokuwa na mashiko hiyo.maana ktk vigezo vya furaha ni pamoja na kipato cha mwanainchi kwa mwaka.GDP

Watanzania na Imani Tuko fine pamoja na hali ngumu tuliyokuwa nayo kiuchumi.

Kitu kikubwa chetu ambacho sasa ndiyo kinazidi kukua siku hadi siku ni ushabiki wa siasa na kuacha kufanya kazi
 
Huyu mkuu wa mkoa kafanya watz wote tumekua hatuna furaha ila nadhani inachangiwa na naniliu..
 
Back
Top Bottom