Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,221
- 2,425
Wanafunzi na wakufunzi toka vyuo vikuu nchini Tanzania wameibuka washindi wakuu katika mashindano ya Masuala ya Teknolojia ya Huawei ICT ya mwaka 2024 - 2025 wakiwashinda washiriki wengine zaidi ya 210,000 toka Ulimwengu kote Duniani.
Ni fainal ambayo iliweza kufanyika Kwenye nchi ya China kupitia Jiji la Shenzhen ambapo wanafunzi Toka DIT, UDSM na UDOM wamefanikiwa kujishindia tuzo Baada ya kushika nafasi ya pili.
Ni mashindano ambayo yako chini ya Huawei Technologies yanayolenga kuwapa wanafunzi mafunzo ya ujuzi kwa vitendo kupitia Teknolojia ya akili bandia (AI) , Big data na cloud's storage.
Pamoja na kukuza ubunifu wa kutatua changamoto halisi kupitia sekta ya kilimo, afya na elimu.Washindi hao wameonyesha kuwa mafanikio hayo yanaonyesha uwezo wa Tanzania kushindana kimataifa katika sekta ya Teknolojia.