Tanzania yamkataa Balozi wa Ujerumani

Tanzania yamkataa Balozi wa Ujerumani

Moja ya sababu za Balozi kukataliwa Tanzania ni kama anajihusisha na masuala ya ushoga. Inawezekana huyo akawa na hiyo sifa.
Sio kweli ndugu yangu. Kama hilo ni tatizo, basi tungeishaambiwa. Kakataliwa kwa sababu hapendi ukiukwaji wa haki za binadamu na pia anapenda vyama vya upinzani. Hivyo viongozi wa CCM walishajua wanakoelekea sababu kwenye haki za binadamu, wao ni zero. Swala kubwa lilikuwa ni kwa huyo balozi kupenda vyama vya upinzani, basi na ndo maana viongozi hawaelezi sababu.
 
Hao si ndo wanaofinance maandamano,tena ikibidi tuvunje tu uhusiano nao maana hakuna kitu tunanufaika nao.
Wewe watu wakiandamana unapoteza nini? Yaani watu wa Bukoba au Mwanza wakijipanga wakaingia barabarani kupinga kitu, inahitaji finance?
Hivi mmeanza kukosa busara kiasi hiki nyie watu? Mtakuwa mzigo mkubwa kwa taifa.
 
Moja ya sababu za Balozi kukataliwa Tanzania ni kama anajihusisha na masuala ya ushoga. Inawezekana huyo akawa na hiyo sifa.
''Anadaiwa kutokuwa na uhusiano mzuri na Serikali ya Kenya kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto kushtakiwa kwenye Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Kimataifa huko The Hague, Uholanzi kutokana na kuhusishwa na vurugu za uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya""

Ndugu sababu kubwa ni hiyo hapo juu hakuna kingine na kumbuka barua ya AG wetu kwenda mahakama ya Kimataifa kuwatetea Lutto na Kenyatta
 
David cameroon
eenhee
mwanaume ukiwa mvivu,
bora acje labda ataleta hayo mambo.
 
Moja ya sababu za Balozi kukataliwa Tanzania ni kama anajihusisha na masuala ya ushoga. Inawezekana huyo akawa na hiyo sifa.

Hapana, huyu inasemekana ana misimamo ya kutetea haki za binadamu. serikali yetu ya sasa inaogopa kuandamwa kutokana na ukiukwaji wake mkubwa wa mambo haya.
Serikali haitaki kuweka bayana ili kuweka hisia hizo unazodhani wewe, lakini kumbuka kuwa kwa wenzetu ushoga sio jambo la ajabu, hivyo kama angekuwa shoga ingekuwa inajulikana tu.
 
Balozi huyo Amekua na mahusiano ya karibu sana na chama kimoja wapo hapa Tanzania chenye sera na mlengo wa kikristo! Kwa habari za intelijensia balozi huyu ndie alie mleta yule naibu waziri wa maendeleo wa Ujerumani hapa nchini na kukutana na viongozi wa chama hicho hapa Tanzania mkoani kilimanjaro eneo la marangu,pia balozi huyo na naibu waziri wake baada ya kukutana na viongozi wa chama hicho alitaka kuonana na Membe,membe akawakatalia kuonana nao! Alivyo rudi kenya alisema maneno ya hovyo juu ya Tanzania!
Mkuu ukristo hapo unatoka wapi? Mbona miradi mingi iliyofadhiliwa na ujeruman haijakataliwa? au ndo ule msemo wa baniani mbaya kiatu chake dawa unafanya kazi
 
Mbona hawajamkataa Magufuli aliyeenda kumfagilia Odinga kwenye kampeni?...
magufuli alitumwa na serikali ndo maana kenyatta hataki uhusiano na viongozi wa tanzania sababu ya ushabiki wa kinjinga wa ccm
 
ni vyema coz anahusika vilivyo na chadema na ninaskia alikua anahudhuria mikutano ya siri ya chadema...so akafie mbali

Unataka anaekuja wakilisa ccm?hii nchi ni ya ccm pekee au acha uhasidi.
 
Tumemkumbatia Balozi wa China anaeshiriki kampenzi za ccm za ndani na za majukwaani wazi kabisa, lakini tumemkataa anaesimamia ukweli na haki kwakuwa atatuharibia sie watawala,

Hii ndio Tanzania inayomilikiwa na CCM kwa nguvu!

huyu balozi hata kukanyaga tzn bado.. weye unasema anasimamia ukweli na haki... ni ukweli gani na haki alivyosimamia tzn ?

hivi kazi ya balozi nchi husika ni kusimamia ukweli na haki katika masuala ya nchi nyingine,,?
 
Unataka anaekuja wakilisa ccm?hii nchi ni ya ccm pekee au acha uhasidi.
tatizo lako unafikri kwa kutumia ma...ko ungekuwa unafikri vizuri kwa kuipenda nchi yako huyo balozi hafai yaani ni mbaya kuliko hata hao KKK
 
Hapana, huyu inasemekana ana misimamo ya kutetea haki za binadamu. serikali yetu ya sasa inaogopa kuandamwa kutokana na ukiukwaji wake mkubwa wa mambo haya.
Serikali haitaki kuweka bayana ili kuweka hisia hizo unazodhani wewe, lakini kumbuka kuwa kwa wenzetu ushoga sio jambo la ajabu, hivyo kama angekuwa shoga ingekuwa inajulikana tu.

Mkuu jMali nikukumbushe tu au kukuelimisha kwamba wote,wakiwamo NGOs, wanaotetea haki za binadamu wanatetea haki ya binadamu kuchagua kuwa shoga. Watetea haki za binadamu wanatetea ushoga kwa 100%. Hivyo kama huyo balozi Ni mtetezi wa haki za binadamu lazima atakua mtetezi wa mashoga. Haki za binadamu ni pana mno na zinajumuisha sexual orientations.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom