Tanzania yamkataa Balozi wa Ujerumani

Tanzania yamkataa Balozi wa Ujerumani

Tanzania imemkataa Balozi mteule wa Ujerumani ambaye alitakiwa kuja kufanya kazi nchini. Balozi huyo, Margit Hellwig-Boette alikuwa amemaliza muda wake nchini Kenya na alitakiwa kuja kuiwakilisha nchi yake Tanzania.
Balozi Hellwig-Boette alikaririwa na Gazeti la Standard la Kenya akieleza kuwa anajipanga kurudi kwao baada ya kukataliwa na Serikali ya Tanzania.

Alipoulizwa juu ya suala hilo, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alikataa kuzungumzia suala hilo akisema: "Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje ndio wanaoshughulika na hayo mambo, waulizeni."

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mkumbwa Ally alisema wizara yake haijapata taarifa za kukataliwa kwa balozi huyo.

"Suala hilo linahusu ofisi ya Rais, mambo ya uteuzi ni ya Rais. Wizara ya Mambo ya Nje haina hiyo taarifa na hata kama ingekuwapo hiyo taarifa siyo ya `public'.

"Siyo taarifa ya umma kwa maana kwamba, mchakato wake ni wa siri na hayo mambo hayana kuuliza kwa nini. Ukileta jina la mtu unayetaka aje kuwa balozi likikataliwa, hakuna kuuliza eti ni kwa nini.

"Unachofanya ni kuleta jina jingine, hata Rais hapa akipeleka jina la mtu kwenye nchi nyingine lisiporudi, hakuna kuuliza unachofanya ni kuteua tu jina jingine," alisema Mkumbwa.

Alikariri Kifungu cha Nne cha Azimio la Vienna ambacho kinaruhusu nchi kukataa balozi wa nchi nyingine bila ya kutoa sababu.
"Nchi inayopeleka balozi katika nchi nyingine inatakiwa kutoa jina mapema kwa nchi nyingine. Hata hivyo, nchi hiyo ina uwezo wa kumkubali au kukataa uteuzi," kinaelekeza kifungu hicho.

Gazeti hilo la The Standard, lilimkariri Balozi Hellwig-Boette akisema kuwa amekataliwa kuja Tanzania bila ya kuelezwa sababu.

"Ndiyo, Tanzania imekataa uteuzi wangu. Kwa mujibu wa itifaki za kidiplomasia, nchi husika ina haki ya kumkataa mtu aliyeteuliwa kwenda kuwakilisha nchi yake au kumkubali.

Tanzania imenikataa lakini haijatoa sababu yoyote ya kufanya hivyo. "Nitaondoka Nairobi kurudi Berlin Alhamisi (leo) asubuhi ili nikapangiwe sehemu nyingine," lilieleza gazeti hilo.

Hivi karibuni aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga aliandaa chakula cha jioni, lengo likiwa ni kumuaga balozi huyo baada ya kumaliza kipindi cha miaka minne akiwa anaiwakilisha Ujerumani nchini Kenya.
Misimamo yake imemponza

Gazeti hilo limesema Hellwig-Botte ambaye alikuwa Balozi wa Ujerumani nchini Kenya tangu mwaka 2009, alikuwa anajulikana kutokana na misimamo yake na hasa kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu na mara nyingine kuunga mkono vyama vya upinzani.

Anadaiwa kutokuwa na uhusiano mzuri na Serikali ya Kenya kutokana na msimamo wake wa kuunga mkono Rais wa nchi hiyo, Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto kushtakiwa kwenye Mahakama ya Makosa ya Jinai ya Kimataifa huko The Hague, Uholanzi kutokana na kuhusishwa na vurugu za uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Source: Mwananchi
 
ni vyema coz anahusika vilivyo na chadema na ninaskia alikua anahudhuria mikutano ya siri ya chadema...so akafie mbali
 
Nani kakwambia Tz tunapenda mabalozi wenye misimamo kama huyo,sie type zetu
ni juopinq...kama nimekosea erase my case
 
ni vyema coz anahusika vilivyo na chadema na ninaskia alikua anahudhuria mikutano ya siri ya chadema...so akafie mbali

naona mwezi umeandama kifafa kinakusumbua
 
Hao si ndo wanaofinance maandamano,tena ikibidi tuvunje tu uhusiano nao maana hakuna kitu tunanufaika nao.
 
Nani kakwambia Tz tunapenda mabalozi wenye misimamo kama huyo,sie type zetu
ni juopinq...kama nimekosea erase my case

hujakosea mkuu,sisi tunataka mabalozi wa kupanda majukwaani ili kukisaidia chama chetu kisikumbwe na tsunami 2015
 
"Siyo taarifa ya umma kwa maana kwamba, mchakato wake ni wa siri na hayo mambo hayana kuuliza kwa nini. Ukileta jina la mtu unayetaka aje kuwa balozi likikataliwa, hakuna kuuliza eti ni kwa nini.

"Unachofanya ni kuleta jina jingine, hata Rais hapa akipeleka jina la mtu kwenye nchi nyingine lisiporudi, hakuna kuuliza unachofanya ni kuteua tu jina jingine," alisema Mkumbwa.

Source: Mwananchi
sasa angalau kupitia jf naanza kuelewa mambo ya protokali pia, ina maana Tanzania pia tulipeleka jina la Mzee Abdulahaman Shimbo China kabla ya kuteuliwa!?
 
nasikia balozi huyu ni waajabu sana pia mtu hatari kwa taifa.
 
hata kenya alikuwa anatumika kuchota siri za serikali ya kenya na kupeleka ujerumani.
 
Mbona hawajamkataa Magufuli aliyeenda kumfagilia Odinga kwenye kampeni?...
 
hata kenya alikuwa anatumika kuchota siri za serikali ya kenya na kupeleka ujerumani.

Mzee Yusufu leo unamwakilisha kazini kwake? lakini hapa si mahala pa mipasho, tafadhali
 
Tumemkumbatia Balozi wa China anaeshiriki kampenzi za ccm za ndani na za majukwaani wazi kabisa, lakini tumemkataa anaesimamia ukweli na haki kwakuwa atatuharibia sie watawala,

Hii ndio Tanzania inayomilikiwa na CCM kwa nguvu!
 
Mkuu kufanya mikotano ya siri na vyma vya upinzani ndio kusimamia ukweli? Kosa la balozi wa China halihalishi hili la huyu mteule wenu.
 
Mimi sitaki.....una kingine?

kwani kakuambia nai lazima utake ndio matakwa yetu yaende..?Sikuwa nakubembeleza nilikuwa nakuambia straight....Kinakuwasha nini mambo ya wengine?
 
Mkuu kufanya mikotano ya siri na vyma vya upinzani ndio kusimamia ukweli? Kosa la balozi wa China halihalishi hili la huyu mteule wenu.
Taratibu ...CCM wanapata kichaa..wa china hana ya siri nao?Mlitaka mikutano ya CDm nayo iombe ruhusa CCM?what if walikuwa wanjadili vipengele vya mahusiano ya taasisi za nchini kwao ambazo zilideligate mamlaka kwao km ilivyo kwa nchi nyingine ambazo huwa zitatumia balozi zao nchi nyigine au nchi rafiki?

Kuna ushirikiano na ujerumani ktk kuwezesha vyama ili kukua democrasia CCM huwa nao wanapokea.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom