Makutano ya Joyce Banda na wanadhimu wa Jeshi la Marekani yalikuwa na sauti kuu, na sasa ndicho tunachokiona leo! Diplomasia ya Dar es Salaam iliyotukuka itawale mgogoro huu! Tumemsihi JB arejee mezani na jitihada zinaonyesha kuzaa matunda, lakini harakati za propaganda za kijasusi za Joyce Banda zinataka kutulazimisha tubadili mfumo wausakaji amani ya suala hili. Tukiwa kama taifa lenye nguvu kusini mwa jangwa la sahara na taifa lenye nguvu kidiplomasia duniani, tutamjibu kwa diplomasia tuitakayo!