Tanzania yaitaka CNN kuacha upotoshaji juu ya mpaka wa Tanzania na Malawi

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,564


Troubled water: Oil search fuels tension over Lake Malawi - CNN.com


Serikali ya Tanzania imekitaka kituo cha televisheni cha Kimataifa cha CNN kusahihisha taarifa potofu ilizotoa kuhusu mgogoro wa mpaka unaoendelea kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa.

Taarifa hizo zinaonyesha kwamba mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa upo kwenye ufukwe wa Pwani ya Tanzania jambo ambalo Serikali imesema siyo sahihi.

Akiongea na waaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Assah Mwambene amesema Serikali ya Tanzania imesikitishwa sana na taarifa hiyo na kuitaka CNN kuisahihisha mara moja.


“Tumesikitishwa sana na taarifa hiyo na tunashangaa kuona chombo kikubwa kama CNN wanaweza kutoa taarifa za uongo kwa kiasi hicho” amesema Bw. Mwambene.

Amesema ukweli ni kwamba unapozungumia eneo la Tanzania kilometa za mraba 947,300 (947,300 sq km) ikiwa ni pamoja na nusu ya eneo la ziwa kaskazini mwa mpaka wa Tanzania na Msumbiji na kwamba mpaka upo katikati ya ziwa kama ilivyo kwa mpaka wa Malawi na Msumbiji.

Kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 24 Novemba, 2012, CNN International yenye makao yake Makuu nchini Marekani imekuwa ikiendesha kipindi kuhusu mgogoro wa Tanzania na Malawi na kuonyesha kwamba mpaka uko pembezoni mwa ufukwe wa Tanzania.

Bw. Mwambene amesema kuwa suala hilo hivi sasa linatarajiwa kupelekwa katika Baraza la Marais wastaafu wa Nchi za Umoja wa SADC kwa ajili ya kulitafutia ufumbuzi.

Wakati huo huo, Sherehe za miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania bara zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9 mwaka huu.

Kauli mbiu za sherehe za uhuru mwaka huu ni uwajibikaji , uadilifu na uzalendo ni nguzo ya maendeleo ya Taifa letu.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI
 

Attachments

  • Screenshot.png
    Screenshot.png
    428.5 KB · Views: 406

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,435
3,636
Magharibu ndo wamemtuma Joyce na hili walilifanya baada ya Tz kutumika kwa nembo ya taifa kusafirisha meli za Iran.
Sinema ndo inaanza hivyo.
.
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,042
36,832
Nimeipenda hiyo, ngoja waje wataalamu wa siasa za kimataifa watudadavulie sababu ya CNN kutumia nguvu nyingi kupotosha dunia juu ya swala hili.!
 

Mupirocin

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,740
742
Tanzania sasa imekwisha itapigwa vita baridi kila kona coz ya uzembe wa Mkwe.re, wamesafirisha mafuta ya iran, lakini still wanasafirisha Wanyama hai kwenda huko Uarabuni hivyo huu mgogoro utakuwa mtata sana. Kuna kila dalili kuwa USA, na UK kuisupport Malawi. Malwi watatumia mwanya huu kuendelea kukwamisha ili tujifanye tunapigana ili UK na USA waje kumsaidia na CCM kwa ujumla imechokwa na mataifa mengi duniani coz haipo kwa maslahi ya wananchi ila kwa watu wachache. Let see time will tell
 

kinja

Senior Member
Oct 10, 2010
199
25
Tanzania sasa imekwisha itapigwa vita baridi kila kona coz ya uzembe wa Mkwe.re, wamesafirisha mafuta ya iran, lakini still wanasafirisha Wanyama hai kwenda huko Uarabuni hivyo huu mgogoro utakuwa mtata sana. Kuna kila dalili kuwa USA, na UK kuisupport Malawi.
hao malawi ni vibaraka wao
 

Swat

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,198
1,944
Taasisi za serikali zinazohusika na ulinzi na usalama wa nchi na zile zinazohusika na International relation,zijaribu kuwa pro active na si reactive. Wafanyakazi wa taasisi hizi wanalipwa mishahara ambayo ni kodi za wananchi kwa kazi hiyo. Nashangaa kama CNN walirusha habari hizo toka tar 14 Nov tena kwa siku tatu mfurulizo mpaka leo huyu msemaji alikuwa wapi. Ilitakiwa awakemee toka kipindi cha kwanza tu kurushwa!. La pili watanzania tuwe makini na hawa wamalawi kwani kuna propaganda nyingi wanafanya kuhusiana na suala hili na inawezekana hata producer wa hiyo CNN amelipwa kwa habari hiyo!.Tuwe makini na ikiwezekana hata sisi tufanye hizo propaganda!:sleepy:
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
17,415
25,386
Hawa enzi za mwl angeomba mwenyewe mahojiano nao wajiandae na maswali yote awachachafye kwa hoja hadi wajione choo! Siku hizi sasa nani akapige kiinglishi? J.K ? aaaah wapi!
 

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,919
19,627
Makutano ya Joyce Banda na wanadhimu wa Jeshi la Marekani yalikuwa na sauti kuu, na sasa ndicho tunachokiona leo!

Diplomasia ya Dar es Salaam iliyotukuka itawale mgogoro huu!

Tumemsihi JB arejee mezani na jitihada zinaonyesha kuzaa matunda, lakini harakati za propaganda za kijasusi za Joyce Banda zinataka kutulazimisha tubadili mfumo wausakaji amani ya suala hili.

Tukiwa kama taifa lenye nguvu kusini mwa jangwa la sahara na taifa lenye nguvu kidiplomasia duniani, tutamjibu kwa diplomasia tuitakayo!
 

Mkwai

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
307
96
Kwenye hili la mpaka nadhani viongozi tuliowapa dhamana ndio wamelifikisha hapa, tujiulize ni miaka mingapi ramani ya tanzania inaonyesha kuwa mpaka ni ufukwe wa upande wetu, hata kwenye Google Earth mpaka sasa ni hivo. Ni leo ndio tunakuja kustuka hili? miaka yote tulikuwa wapi? Nadhani hatuna sababu za kutafuta mchawi hapa.
Na kwa sheria na taratibu tulizonazo za mtu mmoja kuwa na mamlaka ya kuteua kila amtakaye;awe ana sifa au hana... hakika tutarajie mambo mengine ya ajabu zaidi kujitokeza siku za usoni.
 

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,931
8,178
Mkwai Huu ndio utaratibu wetu, tunashituka kujifunika shuka asubuhi, kuna watu wanakula mishahara tu hata kwenye wikipedia kuna habari kibao zinapotoshwa lakini hakuna kinachochangiwa
 
Last edited by a moderator:

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,931
8,178
wawakemee na google map

Ndo zetu kukanusha, ukija Kenya utauona mlima Kilimanjaro lakini wao badala ya kujibu ukija Tanzania utapanda mlima kilimanjaro, wao wamekaa kukanusha tu mlima Kilimanjaro haupo Kenya, sasa hivi imeangukia kwenye ziwa. Nadhani tuna uzoefu kwenye haya mambo maana hata Idd Amin aliwahi kuzuka na kusema mpaka wa Uganda ni mto Kagera sema tukamshinda lakini vinginevyo zile kilometa 27 toka mto Kagera angezichukua kama angekuwa ana evidence kwani mto unamwaga maji upande wa Uganda.
 

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,931
8,178
Tanzania tukishinda hii kesi, itabidi na wale waliovunjiwa nyuma zao wakati wa ujenzi wa Morogoro road kwa sheria iliyotungwa na mkoloni wafikiriwe, serikali ilivunja na inavunja nyumba za watu barabarani kwa sheria iliyotungwa enzi za ukoloni lakini Malawi anatumia sheria ya enzi zile (Heligoland treaty), serikali inakuja juu which means hata wana nchi wake kuna haja ya kuwasikiliza kwa kuwa sheria za kikoloni zimewakandamiza kama vile malawi inavyotaka kuikandamiza Tz
 

Pharaoh

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
843
157
Watanzania hatujawa teyari bado, tunalala sana, sasa bora tutulie mpaka aingie Eduardo Lowa halafu baada ya miezi mitano tu ya utawala wake tuanze kudai ziwa kwa nguvu ya aina yoyote
 

Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
9,467
9,828
Makutano ya Joyce Banda na wanadhimu wa Jeshi la Marekani yalikuwa na sauti kuu, na sasa ndicho tunachokiona leo! Diplomasia ya Dar es Salaam iliyotukuka itawale mgogoro huu! Tumemsihi JB arejee mezani na jitihada zinaonyesha kuzaa matunda, lakini harakati za propaganda za kijasusi za Joyce Banda zinataka kutulazimisha tubadili mfumo wausakaji amani ya suala hili. Tukiwa kama taifa lenye nguvu kusini mwa jangwa la sahara na taifa lenye nguvu kidiplomasia duniani, tutamjibu kwa diplomasia tuitakayo!

Well said mkuu, mimi niliwahi kuonya kwamba yule mama hawezi kwenda 4 a photo op. bure, kuna ujumbe alikuwa anataka kuionyesha Tanzania kwamba she's not alone katika mgogoro huo kuna maitaifa ya magharibi ambayo yako nyuma yake - hata majibu jibu yake ya jeuri yanaonyesha hilo - Tatizo la nchi yetu ni kwamba mambo ambayo yanaonekana obvious inatuchukua ages kuyatafakali. Kwa kawaida i.e kiprotokali Raisi ukutana na Raisi mwezake, sasa kwa nini Mama Banda anakwenda kukutana na Military top Brass, kwani kazi ya waziri wa ulinzi ni zipi? Haya mambo ya softly softly approach yatakuja kutu-cost dearly.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom