Tanzania yaishitaki Malawi UN | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanzania yaishitaki Malawi UN

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 30, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145

  [h=2]Tanzania yaishitaki Malawi UN[/h]JUMAPILI, SEPTEMBA 30, 2012 09:49 NA MWANDISHI MAALUMU, NEW YORK

  HATIMAYE Tanzania ’imeishitaki’ Malawi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusisitiza kuwa haina mpango wa kuingia vitani kwa ajili ya kugombania mpaka ndani ya Ziwa Nyasa.

  Badala yake imesema itawasilisha madai yake katika Mahakama ya Kimataifa yenye dhamana ya utatuzi wa mgogoro iliyo chini ya umoja huo ambayo itakuwa na uamuzi wa mwisho wa mpaka huo.

  Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alitoa kauli hiyo wakati akihutubia Mkutano Mkuu wa 67 Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.

  Alisema Tanzania imekuwa mpatanishi mkuu wa migogoro mbalimbali duniani ukiwamo wa Burundi uliokuwa ukisimamiwa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na kamwe haitakuwa kielelezo kibaya cha kudai inachokiamini kwa kutumia nguvu.

  “Ushiriki wa marais wetu wastaafu kuanzia Hayati Nyerere, Benjamin Mkapa na sasa Rais Jakaya Kikwete katika kutatua migogoro mbalimbali, ni sababu tosha ya kuifanya duniani iamini njia sahihi kwa Tanzania kutatua mgogoro ni kwa diplomasia tu,” alisema Waziri Membe.

  Kuhusu migogoro inayoendelea sehemu mbalimbali duniani, Membe alisema kushindwa kuvumiliana kwa wanaopingana katika nyanja tofauti kumekuwa sababu kuu ya kuzidisha migororo, jambo ambalo linahatarisha usalama wa watu na mali zao.

  Membe ameuomba Umoja wa Mataifa kutafuta njia ya dharura ya kutatua mgogoro unaoendelea Syria kati ya majeshi ya Serikali na yale yanayompiga Rais Bashar Al Assad, kutokana na athari kubwa iliyojitokeza katika taifa hilo.

  “Mheshimiwa Rais wa baraza hili, wote tunajua madhara ya migogoro na vita hasa maazimio ya Umoja wa Mataifa yanapokiukwa kama tunavyoona Syria.Hii ni moja kati ya mifano lazima tuwe makini kufikiria mapema njia za kutatua migogoro kabla ya madhara kutokea,” alisema.

  waziri Membe pia alisema kuwa Tanzania na nchi nyingine 12 zinazounda Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), zimekubaliana kuunda jeshi la pamoja na kukituma kikosi cha askari 4,000 kwa ajili ya kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).


   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  nngu007 Membe anapwaya sana katika hii nafasi ya mambo ya nje. Kwa nini hahoji dhamira ya Wamalawi ya kuvamia mpaka?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. a

  artorius JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 758
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbona bungeni alitumia lugha ya tofauti?huyu membe vp tena?ukisikia serikali imemeza moto ndo hii issue
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kwamba umetatua migogoro mingi ya nchi za jirani siyo utetezi kwamba huwezi kukalia ardhi ya mwingine isivyo halali.
  Pia sioni mantiki ya kushitakiana hapa, cha msingi ilikuwa ni kuita mataifa ambayo kwa namna moja au nyingine yalishiriki ktk zoezi la kugawa na kuandaa ramani ya mipaka.
   
 5. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,249
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Hakukuwa na njia mbadala hasa baada ya wenzetu kususia kikao kilichopangwa kufanyika Dar 10-14 mwezi wa tisa.

  Maadhimio ya Mzuzu yalikuwa ni kama hatutaelewana/kufikia mwafaka, basi kwa pamoja tungetafuta msuluhishi (nchi yoyote ya jirani Afrika) kisha nae akishindwa ndipo twende UN.

  Sasa wao wamesusa hasa baada ya ujumbe wetu makini ulioongozwa na Mh B. Membe na Prof A. Tibaijuka kuwamwagia vielelezo lukuki kiasi chakuwaacha midomo wazi.

  Sasa naamini haki ya kila mmoja itaamuliwa na jicho la dunia.
   
 6. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wamalawi hawataki suluhu kwenye suala la mpaka ndani ya ziwa Nyasa. Membe yuko sahihi, watanzania ni lazima tuwashitaki wamalawi ili tupate sababu ya kuwachakaza bila kuingiliwa na watu wa nje. Tanzania ikilipeleka suala hili kwenye mahakama ya kimataifa itashinda kesi. Ikishashinda kesi, au wamalawi wakakataa kuhudhuria kwenye ile mahakama, basi sasa sababu za kuingia vitani zinakuwa ziko wazi na tutakuwa tunapigana vita vya haki - Tutashinda tu.

  Malawi hawataki kwenda kwenye mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa migogoro ya mipaka kwa sababu wanajua wakienda kule hoja yao ni chapati, itamezwa asubuhi tuu. Sasa wanajaribu kutumia nguvu ya wakoloni waliowatawala ili kuwabeba au kuwatisha watanzania.
   
 7. n

  ngomicom Senior Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nahisi wewe ndo umemeza moto tena kaa la moto kwani unafikiri kwa kukurupuka na unaitaka nchi nayo ikurupuke. Membe fanya kazi, kila taasisi inamfumo, fuata mfumo unaokuongoza baba, tumekutuma kazi sio kukurupuka
   
 8. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  umenena vyema!


   
 9. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,462
  Trophy Points: 280
  mkuu unaongelea tu kushinda,vipi tukishindwa tuchukue uamuzi gani.?
   
 10. Sabayi

  Sabayi JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 2,321
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Sioni ni jinsi gani tunaweza kushinda hii kesi tukienda kwenye mahakama ya usuluhishi ile Heligoland treaty imetubana sana dawa ilikuwa ni vitisho na ubabe tu
   
 11. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2012
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mkuu hatuwezi kushindwa. Kesi hii iko wazi mno ndo maana membe anakimbilia huko, wewe unafikiri yeye mjinga. Wote wanaozungumzia kesi hii wanasema Tanzania imesimamia kwenye sheria ya kimataifa, kwa maana kuwa ikiwa sheria ya kimataifa itatumika ushindi wa Tanzania uko wazi.

  Malawi ndo maana wanakataa sheria ya kimataifa na kung'ang'ania wakoloni. Maana yake ni kuwa Malawi wameshapima nguvu ya kesi yao kwenye sheria za kimataifa wakaona haiwezi kushinda. Ndo maana hawataki kwenda huko na hawataki majadiriano. Wanasema ziwa ni lao, full stop. Wanasema hivyo sababu baba yao wa Taifa, Kamuzu Banda alishawaambia hivyo. Na walipooneshwa mkataba wanaodhani umewapa ziwa lote wakagundua kuwa kumbe mkataba ule hauwapi ziwa ndo kabisa wamezidi kuchanganyikiwa.

  Ila wanasiasa wa Malawi wanajua kitu kimoja; atakayewaambia wamalawi kuwa ziwa lote si la kwao, yaani wamelichangia na Tanzania na Msumbiji, atakuwa amejinyima kura. Na siasa za malawi unazijua. Ndo maana kina Chiume baada ya kuona hoja zao ni dhaifu wameamua kugomea majadiriano. Kwa ujumla suala hili linachukua uzito mno kwenye siasa za Malawi. Hakuna mwanasiasa aliye tayari kuwaambia wamalawi kuwa msimamo wa Banda si sahihi.
   
 12. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #12
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  nadhani hiyo ndio njia pekee iliyo salia,hatutawapiga maana uwezo tunao,ila tunataka mgogolo uishe kwa majadiriano
   
 13. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  Sikuona sababu hasa ya Tanzania kufungua hiyo kesi, maana tutakuwa Kama tunatapatapa, Tanzania ndio tuliowazuia Malawi kutumia hicho kipande chetu, sasa wao ndio wangefungua hiyo kesi,
   
 14. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  natamani kuona kauli yetu UN ikisisitiza kuwa kitendo cha nchi jirani kuvamia mipaka yetu kitajibiwa vikali.
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  mabingwa wa kutatua migogoro ya wenzenu sasa ngondo iyooooooooooooooooooooooooo
   
 16. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Duh! uchumi wenyewe wa kupigana vita ukowapi? vita ya Uganda tu zaidi ya miaka 30 na bado tunadaiwa na akina Ghadafi ingawaje wameshakufa, yaani uchumi wa kuexport kahawa, tumbaku na chai tena ghafi wala sio processed ndio unajigamba kwamba utapigana vita? Hao wanajeshi tu wenyewe, mabuti na kombati zina viraka hamna hela ya kununua zingine itakuwa vifaru!

  Sahau mambo ya vita hatuwezi, tumechoka sana tena sana, kwangu mimi bora hata walichukue hilo Ziwa kama ikibidi kuliko kuingia vitani, hailipi kabisa bado tuna mengine mengi tu akina Ziwa Rukwa, Natron, Tanganyika, Nyanza na hayo yote yana utajiri wa kufa mtu, ukienda Natron hapo kuna Magadi (soda Ash) ya kufa mtu, Tanganyika Mafuta ya kufa mtu, Ziwa Nyanza nao maji na samaki wa kufa mtu mito mikubwa ambayo karibu yote ipo ndani ya mipaka yetu kabisa
  mingine haikauki mwaka mzima akina Ruaha, Rufiji, Pangani n.k
   
 17. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Ujinga mtupu hakuna sababu ya kuwashitaki wamalawi, Tanzania inatakiwa ku-develop kwa nguvu ukanda wa ziwa upande wetu na kuweka vitega uchumi vya kukata na shoka kama vile usafiri wa majini katika vijiji husika, uvuaji wa kisasa kwenye eneo letu na kuweka kituo cha manoari za kivita kwenye eneo letu then tuone huyo kimburu anayetaka kuleta chokochoko. Actions speaks louder.

  Wakati umefika kuondoa mizoga ya CCM.
   
 18. Highlander

  Highlander JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 3,094
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  sikiza: tufanye una kijipisto kina risasi nane, na mwenzio unajua ana kijipisto kama icho, alafu unahisi ugomvi wenu hauna suluhu ya karibu na rahisi isipokuwa kumalizana, unafanyaje? si unatangulia kupiga wewe? he !, we vipi...   
 19. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  How comes akiwa UN anaongea with a light touch wakati alipokuwa bungeni aliongea kwa maneno makali huku povu likimtoka!! Watz bwanaaaaaa, kazi kwelikweli.
   
 20. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  well said mkuu,hakuna haja ya kuzunguka mbuyu!kama ziwa ni letu tuwekeze na sio kuleta porojo.ni kweli ccm ni mizoga yafaa kufukiwa.
   
Loading...